Tafakuri: Ni upi hasa unyeti wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar?

Kwa inavyoonekana huu Muungano uliundwa kwasababu za kimaslahi ya usalama wa Tanganyika, maana Zanzibar iko karibu mno na Tanganyika hvyo Kama kusingekua na Muungano basi ingekua njia rahisi mno ya adui zetu kuingia Tanganyika.

Aliyeuhimiza huu Muungano alijua Kama kusipokua na jeshi moja la kulinda kule Zanzibar na Tanganyika, siku tukiingia katika sintofahamu nao basi inaweza kuruhusu adui kuweka kambi pale na kujaribu kuingia kwa urahisi katika viunga vya Tanganyika.

Sina hakika ila naona lilikua Ni swala la kiusalama zaidi na ndio maana wakaipa kibali kua na Rais ama kiongozi wake ila jeshi liwe moja tu!!!

Na kwa nini adui aitumie Zanzibar asiitumie Kenya , Rwanda , Burundi, Uganda, Congo , Malawi, Msumbiji ambako ni rahisi zaidi kuingia kuliko Zanzibar.

Mimi naona kwa vile Nyerere na TANU yake walikuwa hawana uwezo wa kuiongoza Tanganyika. Ili apate kuendelea kuongoza kwa urahisi ilikuwa lazima aivamie Zanzibar na kuichukua , huku akitoa kauli kama hizo za kutishiwa usalama wake.

Pia kuwafanya Watanganyika wakati wote wawe na mawazo ya Muungano bila kuhoji nini kinafanywa kuleta maendeleo ya Tanganyika .

Na ndio CCM inavyoendelea na propaganda hii ya ulazima wa kuwepo huu UVAMIZI unaoitwa Muungano.
 
Mkuu, fikiria sasa, ndiyo Sieph kashinda uraisi, na wazanzibari wakavunja muungano,
Nitajie faida moja tu ya Lisu atakayoipata kutokana na kuvunjika muungano,

Nitajie pia faida ya ACT itakayopata kutoka Zanzibar kuja huku bara ikiwa muungano utavunjwa

Na kisha unitajie manufaa ya Chadema yatayapatikana huku bara Baada ya kuvunjika muungano
Muungano hauvunjwi bali unaboreshwa. Acheni kupotosha
 
Na kwa nini adui aitumie Zanzibar asiitumie Kenya , Rwanda , Burundi, Uganda, Congo , Malawi, Msumbiji ambako ni rahisi zaidi kuingia kuliko Zanzibar.

Mimi naona kwa vile Nyerere na TANU yake walikuwa hawana uwezo wa kuiongoza Tanganyika. Ili apate kuendelea kuongoza kwa urahisi ilikuwa lazima aivamie Zanzibar na kuichukua , huku akitoa kauli kama hizo za kutishiwa usalama wake.

Pia kuwafanya Watanganyika wakati wote wawe na mawazo ya Muungano bila kuhoji nini kinafanywa kuleta maendeleo ya Tanganyika .

Na ndio CCM inavyoendelea na propaganda hii ya ulazima wa kuwepo huu UVAMIZI unaoitwa Muungano.
Hoja zao zote za ccm zimeshafilisika.
 
Back
Top Bottom