Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
Kwa ukumbusho tu:
Rais wawili, Rais wa Muungano na Rais wa Zanzibar!
Serikali mbili, Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar
Vyombo vya uwakilishi viwili, Bunge na Baraza la Wawakilishi
Bendera mbili, Bendera ya Muungano na Bendera ya Zanzibar
Nyimbo za Taifa mbili, Wimbo wa Taifa na Wimbo wa Zanzibar
Kuna unyeti gani hapa?
Kitu gani kinafichwa hapa?
Kwenye Katiba hakuna kipengele chochote kinachozungumzia nchi itaendeshwaje kama vyama tofauti vitashinda bara na visiwani. Kwa hiyo ni dhahiri chama chochote nje ya CCM hakiwezi kutangazwa mshindi hata kikipata asilimia 95% za kura. Labda ni wakati muafaka wa kujiliza, je kwa nini tunahangaika na kupoteza pesa kugharamia uchaguzi usio huru?
Uchaguzi ambao matokeo yake hayana maana wala umuhimu wowote? Hii ni kwa sababu, kama chama chochote kingine kingekuwa na nafasi ya kutangazwa mshindi, Katiba ilitakiwa itamke wazi kabisa namna vyama tofauti vinavyoweza kuunda serikali na kuliongoza taifa. Bila hivyo ni ulaghai, hila na njama za kuwahadaa Watanzania kwamba nasi eti tuna uhuru!
Labda sasa ni wakati wa kujiuliza, hii CCM imewekeza nini hapa nchini hadi ionekani kwamba Tanzania haiwezekani bila CCM. Kwa sasa tunaona viongozi wanavyoshindana kurithiana vyeo kana kwamba wao peke yao ndio wenye haki zaidi nchini. Kwa mwendo huu hatufiki na ni lazima tubadilike, lazima tutazame mbele na kuachana na mazoea yasiyo na tija kwa taifa.
Mathalani kunaanza tabia ya kutoheshimu hata kanuni na sheria tulizojiwekea kama binadamu, tunaanza kuiona Katiba kama kipande tu cha karatasi kisicho na maana na bila kumung'unya maneno tunaanza kuwa na tabia za wanyama wa mwituni. Wanyama hawana sheria, hawana katiba, hawana ustaarabu...kama una nguvu, kama ni mbabe, kama ni mkatili, yote rukhsa.
Anayehoji unyeti wa Muungano na anayehoji tunakoelekea, si adui hafanyi hivyo kwa kutaka kuuvunja Muungano, hapana, anataka kuuimarisha Muungano kwa sababu anaona hitilafu ambazo zisiposhughulikiwa, Muungano wetu uko hatarini na kuna siku tutasambaratika na kila moja kubeba mbao zake. Amkeni Watanzania, tumedanganywa vya kutosha.
- Tuanze kwa kukiri kwamba zilizoungana zilikuwa ni nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar.
- Tukiri pia kuwa wakati zinaungana tulikuwa na vyama tawala viwili, TANU na Afro-Shirazi Party (ASP)
- Pia tukumbushane kwamba wakati zinaungana 1964 bado tulikuwa katika mfumo wa vyama vingi
- Awali nchini Tanganyika Tume ilikuwa imeundwa kuangalia uwezekano kufuta mfumo wa vyama vingi
- Baada ya Muungano hiyo Tume iliimarishwa kwa kuongezewa wajumbe kutoka Zanzibar nao washiriki
- Tume ilitoa ripoti yake tarehe 22/3/1965 na kuikabidhi katika vikao vya vyama viwili tawala, TANU na ASP
- Miezi minne baadaye muswada ukawasilishwa bungeni na sheria mpya ya chama kimoja ikapitishwa rasmi
- Katiba ya muda ndiyo ikatumika katika Uchaguzi Mkuu wa kwanza chini ya mfumo wa chama kimoja 1965