Tafakuri: Ni upi hasa unyeti wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar?

Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,539
2,000
Kwa ukumbusho tu:
  • Tuanze kwa kukiri kwamba zilizoungana zilikuwa ni nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar.
  • Tukiri pia kuwa wakati zinaungana tulikuwa na vyama tawala viwili, TANU na Afro-Shirazi Party (ASP)
  • Pia tukumbushane kwamba wakati zinaungana 1964 bado tulikuwa katika mfumo wa vyama vingi
  • Awali nchini Tanganyika Tume ilikuwa imeundwa kuangalia uwezekano kufuta mfumo wa vyama vingi
  • Baada ya Muungano hiyo Tume iliimarishwa kwa kuongezewa wajumbe kutoka Zanzibar nao washiriki
  • Tume ilitoa ripoti yake tarehe 22/3/1965 na kuikabidhi katika vikao vya vyama viwili tawala, TANU na ASP
  • Miezi minne baadaye muswada ukawasilishwa bungeni na sheria mpya ya chama kimoja ikapitishwa rasmi
  • Katiba ya muda ndiyo ikatumika katika Uchaguzi Mkuu wa kwanza chini ya mfumo wa chama kimoja 1965
Nchi moja, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais wawili, Rais wa Muungano na Rais wa Zanzibar!
Serikali mbili, Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar
Vyombo vya uwakilishi viwili, Bunge na Baraza la Wawakilishi
Bendera mbili, Bendera ya Muungano na Bendera ya Zanzibar
Nyimbo za Taifa mbili, Wimbo wa Taifa na Wimbo wa Zanzibar

Kuna unyeti gani hapa?
Kitu gani kinafichwa hapa?

Kwenye Katiba hakuna kipengele chochote kinachozungumzia nchi itaendeshwaje kama vyama tofauti vitashinda bara na visiwani. Kwa hiyo ni dhahiri chama chochote nje ya CCM hakiwezi kutangazwa mshindi hata kikipata asilimia 95% za kura. Labda ni wakati muafaka wa kujiliza, je kwa nini tunahangaika na kupoteza pesa kugharamia uchaguzi usio huru?

Uchaguzi ambao matokeo yake hayana maana wala umuhimu wowote? Hii ni kwa sababu, kama chama chochote kingine kingekuwa na nafasi ya kutangazwa mshindi, Katiba ilitakiwa itamke wazi kabisa namna vyama tofauti vinavyoweza kuunda serikali na kuliongoza taifa. Bila hivyo ni ulaghai, hila na njama za kuwahadaa Watanzania kwamba nasi eti tuna uhuru!

Labda sasa ni wakati wa kujiuliza, hii CCM imewekeza nini hapa nchini hadi ionekani kwamba Tanzania haiwezekani bila CCM. Kwa sasa tunaona viongozi wanavyoshindana kurithiana vyeo kana kwamba wao peke yao ndio wenye haki zaidi nchini. Kwa mwendo huu hatufiki na ni lazima tubadilike, lazima tutazame mbele na kuachana na mazoea yasiyo na tija kwa taifa.

Mathalani kunaanza tabia ya kutoheshimu hata kanuni na sheria tulizojiwekea kama binadamu, tunaanza kuiona Katiba kama kipande tu cha karatasi kisicho na maana na bila kumung'unya maneno tunaanza kuwa na tabia za wanyama wa mwituni. Wanyama hawana sheria, hawana katiba, hawana ustaarabu...kama una nguvu, kama ni mbabe, kama ni mkatili, yote rukhsa.

Anayehoji unyeti wa Muungano na anayehoji tunakoelekea, si adui hafanyi hivyo kwa kutaka kuuvunja Muungano, hapana, anataka kuuimarisha Muungano kwa sababu anaona hitilafu ambazo zisiposhughulikiwa, Muungano wetu uko hatarini na kuna siku tutasambaratika na kila moja kubeba mbao zake. Amkeni Watanzania, tumedanganywa vya kutosha.
 

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
6,307
2,000
Umeandika vyema sana.

Najaribu kuufikiria "MWISHO" wa haya yote uliyoyaandika unaotangazwa na vyama vya ACT Wazalendo na CHADEMA kuwa ni uchaguzi huu.

Najaribu sana kufikiri na kujiuliza ni njia gani mbadala na maalumu ambazo wameandaa na zitatumika ili kuhakikisha MSHINDI HALALI wa uchaguzi wa mwaka huu anatangazwa.

I am so curious to know.

Nawaona kabisa kina Freeman Mbowe, Tundu Lissu, Maalim Seif Sharif Hammad, Zito Kabwe na Benard Membe wako very determined and confident kuhusu hili....

May be, kila kitu kitafunuliwa katikati ama mwishoni mwa kampeni hizi...

It's absolutely that, THE SYSTEM IS SHAKING!
 

Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,539
2,000
Umeandika vyema sana.

Najaribu kuufikiria "MWISHO" wa haya yote uliyoyaandika unaotangazwa na vyama vya ACT Wazalendo na CHADEMA kuwa ni uchaguzi huu...
Nchi mbili zikiungana na kuwa nchi moja ni kwamba ama serikali inakuwa moja au zinakuwa tatu. Haijawahi kutokea nchi mbili zikaungana na kuwa nchi moja halafu serikali zikabaki mbili kama ilivyokuwa awali. Hivyo hivyo haijawahi kutokea nchi moja ikawa na Rais wawili, huu ni ulaghai na ni mpango uliobuniwa na CCM ili kuhakikisha inabaku madarakani hata kama inashindwa uchaguzi.

CCM iliikataa rasimu ya Jaji Waryoba kwa sababu hiyo hiyo ya kuogopa uwepo kwa kipengele kwenye katiba kinachoruhusu uwezekano wa vyama tofauti Tanzania Bara na Visiwani. Njia iliyotumika kufanikisha hii ni kutoruhusu mtu yeyote kuhoji uenda wazimu huu na hivyo kupiga marufuku kuhojiwa kwa muungano huo ambao msingi wake umejengwa kwa mchanga tu bila mawe wala sementi.
 

Falconer

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
775
500
Asante Mag3, kueleza unaga ubaga kuhusu hali halisi. ilivyo. Kama binadaamu wenye akili, ni wazi kuwa mambo yanayoendelea hayana natiba kwa uhai wetu. Sisi wazenji tunafahamu sana ukorofi na ushenzi wa viongozi wa chama tawala na vishushuu vyao walioko zenji. Sauti ya mzanzibari haina thamani ndio maana mambo yote yanamaliziwa DODOMA.

Mwaka huu, kwa bahati nzuri tuna Mh.Lissu ambae nitegemeo kubwa upande wa bara, amefanikiwa pakubwa kuwafahamisha watanzania bara kuhusu usanii na ulimbukeni wa CCM. Kwa hiyo, macho yao watawala na vibaraka wao yanalenga kwa chadema na huku kwetu wamechanganyikiwa. Sasa, waikose zanzibar au wakose vyote?.
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
103,039
2,000
Mimi ni wa Bara lakini huu Muungano una kasoro nyingi sana. Mojawapo ni kukosekana kwa Serikali ya Tanganyika. Nyingine mambo mengi ya ndani ya Zanzibar kuamuliwa na watu wa Bara. Kwa mfano Marais wote wa Zanzibar tukianzia Mzee RUKHSA na huko nyuma with exception ya Abeid Amani Karume hadi hii leo wameamuliwa na watu wa Bara.

Uchaguzi wa 2015 Wazenj waliichagua CUF iongoze Nchi yao lakini kwa mshangao wa wengi Kikwete akaamuru matokeo yale yafutwe na kituko cha uchaguzi kikafanyika March, 2016.

Muungano huu una kasoro nyingi sana lakini maccm hayako tayari kukaa chini ili kujadili kasoro hizo na namna ya kuzitatua. Maccm yako radhi kutumia mtutu wa bunduki ili kuwanyamazisha Wazenj kudai uhuru na haki yao ya kujiamulia mambo yao bila kuingiliwa na watu wa Bara.

Nina hofu kubwa kwamba katika uchaguzi wa mwaka huu haki hiyo itapokwa tena na maccm hivyo badala ya Seif Shariff Hamad kuwa Rais atasimikwa Hussein Ali Mwinyi kama Rais uamuzi ambao unaweza kuwa chanzo cha machafuko makubwa yatakayosababisha umwagaji mkubwa wa damu ambao haujawahi kutokea katika historia ya Nchi yetu.
 

Dolla_Mbili

JF-Expert Member
May 28, 2017
233
1,000
Kwa inavyoonekana huu Muungano uliundwa kwasababu za kimaslahi ya usalama wa Tanganyika, maana Zanzibar iko karibu mno na Tanganyika hvyo Kama kusingekua na Muungano basi ingekua njia rahisi mno ya adui zetu kuingia Tanganyika.

Aliyeuhimiza huu Muungano alijua Kama kusipokua na jeshi moja la kulinda kule Zanzibar na Tanganyika, siku tukiingia katika sintofahamu nao basi inaweza kuruhusu adui kuweka kambi pale na kujaribu kuingia kwa urahisi katika viunga vya Tanganyika.

Sina hakika ila naona lilikua Ni swala la kiusalama zaidi na ndio maana wakaipa kibali kua na Rais ama kiongozi wake ila jeshi liwe moja tu!!!
 

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
6,364
2,000
Umejaribu kuandika, na kuweka hizo point , lakini hazina uzito wowote kuonyesha nini hasa umeandika, mtu anashindwa kupata "the gist of your point"

Ukizungumzia kwa mfano serikali moja ya muungano it is obvious mkiungana kunakuwa na nchi moja e.g. United kingdom or USA so is united republic of Tanzania na hii ndio inajulikana ktk vyombo vya kimataifa .

Kuhusu kuwepo kwa Raisi wawili au zaidi unatakiwa kuangalia vitu vingine , je hiyo structure in undermine upande mwingine , na huo upande unakuwa undermine unashindwa kufanya vitu vyake??

Na pia uiangalie structure ya USA na UK.

Apart ya kuwepo hiyo United kingdom , kuna serikali ya England, Scotland, Wales,na North Ireland , na kwa USA kuna Governor wa kila state.

Sasa unapojaribu kuonyesha wa kwetu unamapungufu makubwa na haufai , mtu anashindwa kupata hayo Mapungufu yako wapi .

Mfano sasa hivi UK au tuseme England anataka kutoka EU , lakini Scotland na North Ireland in one way or another hawataki , Scotland kwa sababu zao na Ireland kwa sababu ya Makubaliano ya amani Kati ya north Ireland na Ireland nyingine, Wales siku zote wamekuwa kimya.

Sasa tofauti wetu na hali ilivyo UK ni nini?? Hadi huku muufanye kama ni muungano wa ajabu , wa dhuluma n.k na waofanya hivyo ni wa Tanzania wenyewe.
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
1,704
2,000
Mkuu umegusia mambo ya msingi sana kuhusu muungano huu. Ni dhahiri kabisa ulianzishwa kwa ajili ya maslahi ya Tanganyika.

Ukichunguza vyema sababu zilizopelekea hizi nchi mbili kuingia ktk muungano huu, ni kuwa zimepitwa kabisa na wakati kutokana na mazingira ya sasa ya siasa za kimataifa. Hii ndiyo sababu hakuna nchi yoyote ile ama visiwa vya jirani ambavyo vimeonyesha kuvutiwa ili kuweza kujiunga na muungano huu.

Licha ya CCM kuujua ukweli huu, lakini wanaung'ang'ania kwa nguvu zote kwa sababu kubwa moja, wanatambua kasoro zilizopo ndani ya katiba ya JMT ndiyo salama yao ya kuendelea kubaki madarakani. Mtu yeyote yule mwenye kuzionyesha kasoro hizi, ni adui yao mkubwa. Na wanapenda Watanzania wabaki gizani ili wasiweze kuutambua ukweli huu mchungu kwao.
 

Falconer

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
775
500
Mimi ni wa Bara lakini huu Muungano una kasoro nyingi sana. Mojawapo ni kukosekana kwa Serikali ya Tanganyika. Nyingine mambo mengi ya ndani ya Zanzibar kuamuliwa na watu wa Bara. Kwa mfano Marais wote wa Zanzibar kwa tukianzia Mzee RUKHSA na huko nyuma with exception ya Abeid Amani Karume hadi hii leo wameamuliwa na watu wa Bara...
Hilo halina mjadala . Mwaka huu watapelekwa "the Hague". Wasifikiri wataua halafu tuta nyamaza. Kwanza tutauana halafu tutamalizikia the HAGUE.
 

Satu

Senior Member
Nov 22, 2013
154
500
Mtoa mada acha unafiki. Unahoji 'unyeti' wa Muungano wetu, wakati huo huo unajifanya kusema huna lengo la kuuvunja bali unataka 'kuuimarisha'. Unaweza kuimarisha kitu ambacho hata hujui 'unyeti' wake? Au hujui maana ya neno 'unyeti'?

Wewe ni miongoni mwa wale ambao mioyoni mwao wangependa Muungano uvunjike na usiwepo, lakini hadharani wanasema mengine -- mara serikali tatu, mara serikali za mikataba n.k. kwa maslahi yao na mabwana zao. Wengine wanatumika bila hata kujua.

Nikukumbushe tu kuwa kiasili kila kitu ni Muungano. Hata wewe mwenyewe ni Muungano wa yai na mbegu. Hizi ni zama za Muungano. Ulimwengu wenyewe umeungana na unazidi kuimarisha Muungano wake kila siku.

Ulishawahi kufikiri na kuhoji kwa nini Spain inapambana Katalonya isijitoe kwenye Muungano wao? Au Ireland kutoka UK?

Wanaoshabikia kuvunjiaka kwa Muungano, iwe hadharani au kinafikinafiki (kama wewe), katika ulimwengu wa sasa wanatumika vibaya (pengine bila kujua) na wanapaswa waone aibu.
 

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
40,573
2,000
Tuanze Tu kusema wazi huu Muungano uvunjwe.

Haiwezekani watu laki saba watoe wabunge 75.

Huu ni ukandamizaji wa wananchi wa Tanzania bara
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom