TAFAKURI: Mzee Mkapa ameharibu mambo matatu tu, kuna doa sugu la Zanzibar

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Watanzania wote tupoe kwa msiba wa Mzee wetu huyu muhimu katika Taifa letu. Mapenzi ya mungu hayana makosa.

Nikirudi kwenye mada, katika wiki hii ya maombelezo, kuna mengi yanaendelea kujadiliwa kumuhusu Mzee wetu. yameelezwa mazuri mengi na mapungufu vile vile.

Mimi tafakuri yangu imefupisha eneo la Mapungufu au maeneo aliyoharibu.

Wakati najaribu kutoa maelezo yangu sijasahau mafanikio ya Mzee kwenye kuasisi mifumo, kuijenga Tanzania kidiplomasia, Msingi wa uchumi wa kujitegemea, Kujiamini kama kiongozi, kuacha alama nyingi na kuitangaza Tanzania na Afrika.

Kwenye eneo nililokusudia la madhaifu nimeyaweka kwenye makundi matatu.

1. Madhaifu mtambuka: Yale yote yanayotajwa kama madhaifu yakiwemo lugha kavu, kuwadharau waandishi na kudhibiti vyombo vya habari, kutaifisha mashirika ya umma n.k.

2. Kosa la kihistoria: Hili ni kosa ambalo mwenyewe amekiri kwenye kitabu chake cha "My life, My purpose" kuhusu mauaji ya Wazanzibari wa Pemba yaliyotokea kwenye utawala wake mwaka 2001 Januari, 27. Kama kiongozi amekiri kutia doa utawala wake.

3. Kosa la kushindwa kuondoa doa: Hili ndilo kosa kuu alilofanya Mzee wetu. Licha ya kuandika kitabu na kukiri alishindwa kuomba radhi. Hapo ndipo alifanya kosa zaidi.

Niishie hapo kwa muhtasari.

Naambatanisha na shairi la Mshairi. Malenga wa VISIWANI "Nenda baba yetu nenda, pumziko upatiwe".

Kishada
 
Attachments

  • NENDA MKAPA.docx
    13.3 KB · Views: 21
NENDA BABA YETU NENDA, PUMZIKO UPATIWE.

Wewe ni baba kwa mwana, lazima tukuombee
Hapo hakuna hiyana, haki hizo upatiwe
Mkapa mwana tanzana , heshima yako upewe
Nenda baba yetu nenda pumziko upatiwe.

Nakuombea hatima, kama mwana binadamu
Machozi yalenga lenga, rohoni kuna shahamu
Kuna kovu inauma, kila nikitabasamu
Nenda baba yetu nenda, pumziko upatiwe.

Mazuri umeyatenda, mengi hilo twafahamu
Kuna moja mekuganda, doa jeusi kudumu
Nduguzo watu wa Pemba, faraja mewadhulumu
Nenda baba yetu nenda, pumziko upatiwe

Faraja inayonenwa si ndwele wala sitamu
Ilikuwa neno moja , “Kumradhi” wangu damu
Hiyo kwao ni faraja kuliko chama kidumu
Nenda baba yetu nenda, pumziko upatiwe.

Kukiri hatua moja, ya pili ungenawiri
Ngemaliza na lahaja , Kumradhi sio shari
Kitabu ngevishwa koja, maru maru na Hariri
Nenda baba yetu nenda, pumziko upatiwe.

Mbili saba Januari, doa sugu maishani
Yangefuata mahaba, na vitendo mari mari
Walau ngeleta toba, japo ya mali kauli
Nenda baba yetu nenda, Pumziko upatiwe.

Machozi yananitoka, nikikumbuka kauli
Ngunguri mwana Mahita, mdomo hauhiyari
Samehe yagoma toka, mdomoni kuna ngiri.
Nenda baba yetu nenda, pumziko upatiwe.

Ilikuwa ni furusa adhimu mwana kubiri
Maandishi meremeta, yangebaki kwa dahari
Na hiyo uliikosa, kabaki lugha kukiri
Nenda baba yetu nenda, Pumziko upatiwe.

By Malenga wa Visiwani.
 
Kuomba radhi ni kitu muhimu sana maishani. hiki ndio alikikosa Mzee wetu.

RIP Ben.
... Mkapa alikosa unyenyekevu kabisa; badala yake kiburi kilimtawala sana kikazaa dharau, jeuri, majivuno, na mambo yafananayo na hayo.
 
Muungano unalindwa kwa damu za watu wasio na Hatia
Jee mpaka lini? Twapaswa TUJIFUNZE YANAYOJIRI "KASHMIR, CHECHNYA, KURDSTAN, BAHRAIN..." IRELAND SIKU HIZI HATUISIKII!!
Hili lahitaji katiba ilee...
Kuvunjika muungano ni uongo na ngano za kusadikika...
Kuna wazanzibari wangapi maisha yao yote yako Tanganyika? Au tunajisahaulisha kuwa wako wazenji walioshiriki uhuru wa Tanganyika?
 
Watanzania wote tupoe kwa msiba wa Mzee wetu huyu muhimu katika Taifa letu. Mapenzi ya mungu hayana makosa.

Nikirudi kwenye mada, katika wiki hii ya maombelezo, kuna mengi yanaendelea kujadiliwa kumuhusu Mzee wetu. yameelezwa mazuri mengi na mapungufu vile vile.

Mimi tafakuri yangu imefupisha eneo la Mapungufu au maeneo aliyoharibu.

Wakati najaribu kutoa maelezo yangu sijasahau mafanikio ya Mzee kwenye kuasisi mifumo, kuijenga Tanzania kidiplomasia, Msingi wa uchumi wa kujitegemea, Kujiamini kama kiongozi, kuacha alama nyingi na kuitangaza Tanzania na Afrika.

Kwenye eneo nililokusudia la madhaifu nimeyaweka kwenye makundi matatu.

1. Madhaifu mtambuka: Yale yote yanayotajwa kama madhaifu yakiwemo lugha kavu, kuwadharau waandishi na kudhibiti vyombo vya habari, kutaifisha mashirika ya umma n.k.

2. Kosa la kihistoria: Hili ni kosa ambalo mwenyewe amekiri kwenye kitabu chake cha "My life, My purpose" kuhusu mauaji ya Wazanzibari wa Pemba yaliyotokea kwenye utawala wake mwaka 2001 Januari, 27. Kama kiongozi amekiri kutia doa utawala wake.

3. Kosa la kushindwa kuondoa doa: Hili ndilo kosa kuu alilofanya Mzee wetu. Licha ya kuandika kitabu na kukiri alishindwa kuomba radhi. Hapo ndipo alifanya kosa zaidi.

Niishie hapo kwa muhtasari.

Naambatanisha na shairi la Mshairi. Malenga wa VISIWANI "Nenda baba yetu nenda, pumziko upatiwe".

Kishada
Ni sawa ila pia kumbuka KIWIRA kule kusini.Ni doa kubwa kwa WaTZ.
 
Ni sawa ila pia kumbuka KIWIRA kule kusini.Ni doa kubwa kwa WaTZ.
Wakuu marehemu hatajwi kwa maovu yake. Hata angekuwa ana ubaya kiasi gani ni heri tukumbuke mema yake hata kama ni machache tumtaje kwa hayo.
Imebaki ni historia
 
Mwanadamu ana nongwa!! Kitendo cha kuandika kitabu na kukiri mauaji ya Wapemba ni kujutia. Yatosha kabisa kuwa ameomba radhi.

La waandishi wa habari wala siyo doa. Waandishi wa Tanzania walio wengi ni makanjanja na mbumbumbu sana, waache waendelee kuumia na kauli ya Mkapa mpaka watakapo jitambua
 
Back
Top Bottom