Tafakuri: Kuna faida gani kuishi maisha ya kifahari Sana huku mwisho wako ni kifo?

Wasalaaaam!

Kuna haja ya kujiuliza Kisha kupata jawabu sahihi.

Je, kuna faida gani kuwa na maisha ya kifahali sana huku ufahali huo utauacha ndani ya sekunde moja ya ukamilisho wa maisha yako?

Katika jamii yetu ya Kitanzania, kuna watu walio katika Magroup ya uhitaji na hawana msaada, mfano, machokolaa, yatima, walemavu, vipofu nk

Je, ni kwa Nini wewe uliyejaaliwa neema ya maisha ya ufahali, ukaishi kwa kiasi na Kisha ukawaangaliwa hao wenye uhiyahitaji maalumu?

Nakumbusha tu, ya kuwa Maandiko matakatifu yanatwambia, "Dini iliyosafi Ni ile inayowajali yatima na wajane"

Kwanini usiweke hazina yako mbinguni ambako hakuna kutu wala uaharibifu wowote?

#miaka inaenda kasi Sana, nasi tunatoweka mara moja, je, ufahali wako utamwachia nani?
We omba msaada utasaidiwa lakini usikae kutisha watu, Mungu alituumba ili tufurahie maisha na si kuteseka
 
Nimewasidia wengi lakini sasa nashangaa wamniacha au kunisahau but that's the story of life.
Kwanza kabisa , nikupe hongera Sana kwa kuwasaidia wale ulioguswa nao!

Pili, unaposaidia Usitegemee fadhira kutoka kwa uliyemsaidia!

Muhimu tukwamuane pale tulipokwama!
 
We omba msaada utasaidiwa lakini usikae kutisha watu, Mungu alituumba ili tufurahie maisha na si kuteseka
Nmezungumzia wale special needs, najua Mungu alituumba ili tufurahie maisha!

Lakini vipi, wewe ufurahie maisha na kunamtu ambaye Hana dira kabisa ya maisha Hana pa kula Wala kulala, Hana baba Wala Mama, kifupi Ni mtoto wa mtaani, unajisikiaje?
 
Kwahio mkuu unataka kusema tusifurahie maisha mpaka hao watu wenye special needs waishe duniani?

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Kifo kiko palepale tu hata kama unacho au huna, Binadamu tunajisahau sana, kila siku ni kujimbikizia tu wakati huo uwezi jua mwisho wako ni lini hapa duniani. Kutafuta mali za hapa duniani ni kama tunajilisha upepo tu, mwili wako ni ule ule tu, huwezi kuujaza kila kitu, uwe na magari na majumba, pesa nyingi bank yote hiyo ni kujilisha upepo siku ya siku utaona Mali zote ulizohangaikia hazina maana yeyote.

Ndo maana Kuna kabila furani wao pesa ndiyo kila kitu kwa kuua au dhuruma na ujambazi, wanapofika miaka 70 au zaidi huwezi kuwakosa kanisani kutubu dhambi zao wakati huo wanaona mali hazina thamani tena, wanatamani waliyowauwa au dhurumu mali zao wajitokeze waombe msamaha na kurudisha hizo mali kwao lakini inakuwa too late, ndo maana kila siku asubuhi saa 12 utamwona kanisani kutubu dhambi ndo aendelee na shughuli zingine.
Hao jamaa wa hilo kabila walikuambia hayo? Usihukumu, usije ukahukumiwa
 
Wasalaaaam!

Kuna haja ya kujiuliza Kisha kupata jawabu sahihi.

Je, kuna faida gani kuwa na maisha ya kifahali sana huku ufahali huo utauacha ndani ya sekunde moja ya ukamilisho wa maisha yako?

Katika jamii yetu ya Kitanzania, kuna watu walio katika Magroup ya uhitaji na hawana msaada, mfano, machokolaa, yatima, walemavu, vipofu nk

Je, ni kwa Nini wewe uliyejaaliwa neema ya maisha ya ufahali, ukaishi kwa kiasi na Kisha ukawaangaliwa hao wenye uhiyahitaji maalumu?

Nakumbusha tu, ya kuwa Maandiko matakatifu yanatwambia, "Dini iliyosafi Ni ile inayowajali yatima na wajane"

Kwanini usiweke hazina yako mbinguni ambako hakuna kutu wala uaharibifu wowote?

#miaka inaenda kasi Sana, nasi tunatoweka mara moja, je, ufahali wako utamwachia nani?
Mhubiri 3
1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.

2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa;

3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;

4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;

5 Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;

6 Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;

7 Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;

8 Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani.

9 Je! Mtendaji anayo faida gani katika yale anayojishughulisha nayo?

10 Nimeiona taabu ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake.

11 Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.

12 Mimi najua ya kwamba hakuna jema kwao kupita kufurahi, na kufanya mema maadamu wanaishi.

13 Tena ni karama ya Mungu kila mtu apate kula na kunywa, na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote.

14 Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele; haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu ameifanya ili watu wamche Yeye.

15 Yale yaliyoko yamekuwako; na hayo yatakayokuwako yamekwisha kuwako; naye Mungu huyatafuta tena mambo yale yaliyopita.

16 Zaidi ya hayo, nikaona tena chini ya jua ya kwamba, Mahali pa hukumu upo uovu, Na mahali pa haki upo udhalimu.

17 Nikasema moyoni mwangu, Mungu atawahukumu wenye haki na wasio haki; kwa kuwa kuna wakati huko kwa kila kusudi na kwa kila kazi.

18 Nikasema moyoni mwangu, Ni kwa sababu ya wanadamu, ili Mungu awajaribu, nao waone ya kuwa wao wenyewe wafanana na wanyama.

19 Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili.

20 Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena.

22 Hivyo nikaona ya kwamba hakuna jema kupita mwanadamu kuzifurahia kazi zake; kwa sababu hili ni fungu lake; kwa maana ni nani atakayemrudisha tena ili ayaone yatakayomfuata baadaye.
 
Wasalaaaam!

Kuna haja ya kujiuliza Kisha kupata jawabu sahihi.

Je, kuna faida gani kuwa na maisha ya kifahali sana huku ufahali huo utauacha ndani ya sekunde moja ya ukamilisho wa maisha yako?

Katika jamii yetu ya Kitanzania, kuna watu walio katika Magroup ya uhitaji na hawana msaada, mfano, machokolaa, yatima, walemavu, vipofu nk

Je, ni kwa Nini wewe uliyejaaliwa neema ya maisha ya ufahali, ukaishi kwa kiasi na Kisha ukawaangaliwa hao wenye uhiyahitaji maalumu?

Nakumbusha tu, ya kuwa Maandiko matakatifu yanatwambia, "Dini iliyosafi Ni ile inayowajali yatima na wajane"

Kwanini usiweke hazina yako mbinguni ambako hakuna kutu wala uaharibifu wowote?

#miaka inaenda kasi Sana, nasi tunatoweka mara moja, je, ufahali wako utamwachia nani?
Endeleza zaidi ya hapo
1. Kuna faida gani ya kusoma wakati utakufa!?
2. Kuna faida gani ya kutibiwa wakati unaumwa na huku una siku ya kufa!?
3. Kuna faida gani ya kula na huku utakufa!?

4. Kuna faida gani ya kuvaa nguo na wakati utakufa!?

5. Kuna faida gani ya kujenga huku una siku ya kufa!?

6. Kuna faida gani ya kuwa na marafiki wakati utakufa!?

etc
 
Wasalaaaam!

Kuna haja ya kujiuliza Kisha kupata jawabu sahihi.

Je, kuna faida gani kuwa na maisha ya kifahali sana huku ufahali huo utauacha ndani ya sekunde moja ya ukamilisho wa maisha yako?

Katika jamii yetu ya Kitanzania, kuna watu walio katika Magroup ya uhitaji na hawana msaada, mfano, machokolaa, yatima, walemavu, vipofu nk

Je, ni kwa Nini wewe uliyejaaliwa neema ya maisha ya ufahali, ukaishi kwa kiasi na Kisha ukawaangaliwa hao wenye uhiyahitaji maalumu?

Nakumbusha tu, ya kuwa Maandiko matakatifu yanatwambia, "Dini iliyosafi Ni ile inayowajali yatima na wajane"

Kwanini usiweke hazina yako mbinguni ambako hakuna kutu wala uaharibifu wowote?

#miaka inaenda kasi Sana, nasi tunatoweka mara moja, je, ufahali wako utamwachia nani?
Ukirejea maandiko matakatifu, utajiri halali hutoka kwa Mungu. Umeongelea kuwasaidia wahitataji (wajane, yatima, na wasiojiweza); kwa kutoa msaada kwa hawa, hapo umempendeza Mungu, kwani hiyo ni sadaka yako.

Kuanzia mababu zetu, Abrahamu, Isaka, Yakobo, mpaka vizazi vya akina Daudi (Solomoni), walikuwa matajiri, utajiri wao ulitoka kwa Mungu kwa kuwa walitimiza mapenzi ya Mungu kwa kumtolea matoleo.

Mungu anasema nijaribu (kwa kumtolea sadaka) uone baraka zitakavyomiminika juu yako. Kwahivyo, kuwa na utajiri utokao kwa Mungu sio dhambi maana Mungu amejaa neema na ndiyo hutushushia waja wake.

Mungu alimwambia mfalme Solomoni (mwana wa mfalme Daudi), kuwa aombe chochote anachotaka, naye atamjalia. Mfalme Solomoni alimwomba Mungu ampe hekima (nadhani ingekuwa kizazi chetu hiki, tungeomba mali), tazama, Mungu alimjalia mfalme Solomoni hekima na zaidi ya hapo alimpa utajiri. Kumbe tunaona kuwa, kuwa na mali nyingi alizotujalia mwenyezi Mungu sio dhambi.
 
Ni kweli kabisa!
Ukitaka kuliona Hilo,unapoanza kuzeeka! Hapa ndipo utaona kila ulichonacho ni upuuzi tu.
Ila ukitaka kufurahia maisha mkaribishe Mungu na Neno lake katika maisha yako! Kumbuka masikini kuwapa cho chote unapobarikiwa.
Baada ya maisha haya utaenda kupumzika katika maisha mengine mapya baada ya kutoka hapa duniani.
 
Kifo kiko palepale tu hata kama unacho au huna, Binadamu tunajisahau sana, kila siku ni kujimbikizia tu wakati huo uwezi jua mwisho wako ni lini hapa duniani. Kutafuta mali za hapa duniani ni kama tunajilisha upepo tu, mwili wako ni ule ule tu, huwezi kuujaza kila kitu, uwe na magari na majumba, pesa nyingi bank yote hiyo ni kujilisha upepo siku ya siku utaona Mali zote ulizohangaikia hazina maana yeyote.

Ndo maana Kuna kabila furani wao pesa ndiyo kila kitu kwa kuua au dhuruma na ujambazi, wanapofika miaka 70 au zaidi huwezi kuwakosa kanisani kutubu dhambi zao wakati huo wanaona mali hazina thamani tena, wanatamani waliyowauwa au dhurumu mali zao wajitokeze waombe msamaha na kurudisha hizo mali kwao lakini inakuwa too late, ndo maana kila siku asubuhi saa 12 utamwona kanisani kutubu dhambi ndo aendelee na shughuli zingine.
Wewe kama sio mlokole,utakuwa na matatizo ya akili.
Yaani tusitafute utajiri,pesa kwa vile Kuna kifo?!! Haya Mawazo wanayo watu wasio na kitu,babu,bibi walikuwa choka mbaya,baba,mama choka mbaya,ukasoma saint kayumba,sasa na wewe huna kitu,umri umeenda,watoto wako hawajuhi hata Zanzibar inafananaje,hawana toys,games,hawajuhi raha ya kupanda school bus,kwenda vacation south afrika,harafu unasema kutafuta fedha ni kujirisha upepo?
Uwe maskini,tajiri,lazima uzikwe Tena bila kitu,kwahiyo Kuna ubaya gani kuwa na mali ukafurahia haya maisha ya duniani,maaana uwezo wa kupata mali anatoa Mungu,
Diamond anaingiza zaidi ya milioni 200 kwa mwezi,wewe hata milioni moja huna,harafu unajifariji eti pesa ni kujirisha upepo,
Smart phone,magari,manyumba,yapo kufsnya maisha yawe poa,
Wewe upande daladala mpaka Kariakoo kutoka bunju,mwezio anawasha Benz,V8,unafikiri mpo Sawa?wote mtakufa,ila wewe utakufa ukiwa umeisha kongoroka kabisa kwa sababu uliishi maisha magumu!!
Na kumbuka maisha hayaishi wewe ukifa!!?yanaendelea,
Kulikuwa na watu hapa duniani 1884!!watakuwepo hata miaka 1000 ijayo!!swali kizazi chako kitakuwaje?
Wenzio wanaacha ramani Ili vizazi vyao viendelee kuwa matajiri,maraisi,ma CEO wa hapa duniani,wewe kwa uvivu wako,kizazi chako kitaendelea kuwa mama ntilie,wachoma mkaa,what a shame?!!
 
Kuntu kuntu,Watendee Watu wema ili upate malipo Mema mbeleni.
 
Wasalaaaam!

Kuna haja ya kujiuliza Kisha kupata jawabu sahihi.

Je, kuna faida gani kuwa na maisha ya kifahari sana huku ufahari huo utauacha ndani ya sekunde moja ya ukamilisho wa maisha yako?

Katika jamii yetu ya Kitanzania, kuna watu walio katika Magroup ya uhitaji na hawana msaada, mfano, machokoraa, yatima, walemavu, vipofu nk

Je, ni kwa Nini wewe uliyejaaliwa neema ya maisha ya ufahari, ukaishi kwa kiasi na Kisha ukawaangaliwa hao wenye uhiyahitaji maalumu?

Nakumbusha tu, ya kuwa Maandiko matakatifu yanatwambia, "Dini iliyosafi Ni ile inayowajali yatima na wajane"

Kwanini usiweke hazina yako mbinguni ambako hakuna kutu wala uaharibifu wowote?

#miaka inaenda kasi Sana, nasi tunatoweka mara moja, je, ufahali wako utamwachia nani?
Shida yako mtoa mada ni Pepo la Unyonge linakutawala, unapenda vitu vidogo na vya kawaida. Hata Mwanafunzi wa Yesu Petro alikuwa na pepo huyo ndio maana pale Mlimani alimuambia YESU wajenge vibanda vitatu badala ya Hekalu.
Utajiri ni jambo la Baraka na hakuna Msaada utakaofanya kwa kuishi kawaida zaidi utafanya watu washindwe kuuona Ufalme wa Mungu hapa Duniani kwa kukosa kuuona kwako tofauti.

Ishi vizuri watu watamani, toa Sadaka yako nzuri kama unaweza Wodi, Darasa, Barabara, Kanisa ili watu waone umuhimu wa kutafuta
 
hapo ungeongeza kumtag Mfalme Suleiman aje ampe mwongozo mtoa mada jinsi Gani ya kula Raha za Dunia Kwa gharama kubwa.

Kama unayajua maandiko ya kiyahudi Mpe mwongozo juu ya menu ya chakula na vinywaji kwenye jumba la mfalme Kwa siku halafu na idadi ya pisi Kali za Kiyahudi,kihabesh,kirumi,kimisri

kigalatia,kiyunani,kisamaria nk nk alizochakata mfalme Kwa siku

Mtoa mada afanya masikhara

Ponda Raha kufa kwaja shekh!
Umenichekeshaje mkuu tokea kukuche
 
Siku zote Maskini umuazia mabaya Tajiri..na siku zote Tajiri umuazia mema maskini..
 
Naunga mkono hoja.Naonaga ni umburula tu kujishindilia ukwasi wakati ukiisubiria ile siku iliyo kuu ya kufunga na iziraili
 
Tafuta pesa nyingi tu lakini kwa jasho lako ,hiyo pesa ni nzuri Sana haina majuto uko mbeleni, pia tuishi kwa kiasi kwa kuwasaidia wengine wenye uitaji. Usiibe,usiuwe,usidhulumu mali ya mtu mwingine. Majuto yake ni makubwa sana uko mbeleni.
Mkuu nimependa sana maelezo yako,naomba kuuliza je Ku bet/kamali unaiweka kundi gani.
 
Back
Top Bottom