Tafakuri: Kuna faida gani kuishi maisha ya kifahari Sana huku mwisho wako ni kifo?

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,050
4,903
Wasalaaaam!

Kuna haja ya kujiuliza Kisha kupata jawabu sahihi.

Je, kuna faida gani kuwa na maisha ya kifahari sana huku ufahari huo utauacha ndani ya sekunde moja ya ukamilisho wa maisha yako?

Katika jamii yetu ya Kitanzania, kuna watu walio katika Magroup ya uhitaji na hawana msaada, mfano, machokoraa, yatima, walemavu, vipofu nk

Je, ni kwa Nini wewe uliyejaaliwa neema ya maisha ya ufahari, ukaishi kwa kiasi na Kisha ukawaangaliwa hao wenye uhiyahitaji maalumu?

Nakumbusha tu, ya kuwa Maandiko matakatifu yanatwambia, "Dini iliyosafi Ni ile inayowajali yatima na wajane"

Kwanini usiweke hazina yako mbinguni ambako hakuna kutu wala uaharibifu wowote?

#miaka inaenda kasi Sana, nasi tunatoweka mara moja, je, ufahali wako utamwachia nani?
 
Kifo kiko palepale tu hata kama unacho au huna, Binadamu tunajisahau sana, kila siku ni kujimbikizia tu wakati huo uwezi jua mwisho wako ni lini hapa duniani. Kutafuta mali za hapa duniani ni kama tunajilisha upepo tu, mwili wako ni ule ule tu, huwezi kuujaza kila kitu, uwe na magari na majumba, pesa nyingi bank yote hiyo ni kujilisha upepo siku ya siku utaona Mali zote ulizohangaikia hazina maana yeyote.

Ndo maana Kuna kabila furani wao pesa ndiyo kila kitu kwa kuua au dhuruma na ujambazi, wanapofika miaka 70 au zaidi huwezi kuwakosa kanisani kutubu dhambi zao wakati huo wanaona mali hazina thamani tena, wanatamani waliyowauwa au dhurumu mali zao wajitokeze waombe msamaha na kurudisha hizo mali kwao lakini inakuwa too late, ndo maana kila siku asubuhi saa 12 utamwona kanisani kutubu dhambi ndo aendelee na shughuli zingine.
 
Upo ushahidi kwamba dadika chache kabla ya kifo,roho ya mtu hujiinua nje ya mwili wa mwanandamu na kumrudishia ufahamu wake wote.

ndio dakika hizi,hutamani aombe msamaha kila aliyewahi kumkosea,hata kama ni kosa dogo kiasi gani.maana kwa wakati ule mtu huwa yuko ktk furaha isiyo kifani.

hukumbushwa kila mwisho wa mwanandamu ni hatua ile aliyopo,hivyo hutamani kumsihi kila mtu ajaribu kuwa mwema kwa kadri awezavyo,maana hakuna maisha marefu.

kwa wale wa imani hutumia muda huu kuomba msamaha kwa muumba wao,ni fulsa adimu sana hii huwapata wachache.

wakati huu ndio ule wakati ambao kila ulichokiona ni cha maana chenye uzito hasa katika mali,wanawake wazuri,elimu,nguvu za mwili,na pesa benki,utagundua ni upuuzi kabisa,maana havina kazi yoyote mbele ya safari inayokukabili mbeleni.

Neno la Mungu lasema,ni rahisi ngamia kupenya ktk tundu la sindano kuliko tajiri kuuona ufalme wa mbinguni,kwanini???
utajiri tafsiri yake ni ubinafsi.kama umepewa nguvu na akili ya kutafuta maana yake uwape wasio nazo,ila ulimwengu shujaa huu,wacha kila mtu afanye anavyoona inafaa.
 
Kifo kiko palepale tu hata kama unacho au huna, Binadamu tunajisahau sana, kila siku ni kujimbikizia tu wakati huo uwezi jua mwisho wako ni lini hapa duniani. Kutafuta mali za hapa duniani ni kama tunajilisha upepo tu, mwili wako ni ule ule tu, huwezi kuujaza kila kitu, uwe na magari na majumba, pesa nyingi bank yote hiyo ni kujilisha upepo siku ya siku utaona Mali zote ulizohangaikia hazina maana yeyote, ndo maana Kuna kabila furani wao pesa ndiyo kila kitu kwa kuua au dhuruma na ujambazi, wanapofika miaka 70 au zaidi huwezi kuwakosa kanisani kutubu dhambi zao wakati huo wanaona mali hazina thamani tena, wanatamani waliyowauwa au dhurumu mali zao wajitokeze waombe msamaha na kurudisha hizo mali kwao lakini inakuwa too late, ndo maana kila siku asubuhi saa 12 utamwona kanisani kutubu dhambi ndo aendelee na shughuli zingine.
Kwa hiyo unashaurije, tuachane na utafutaji pesa?
 
'msiwapangie watu jinsi ya kuishi maisha yao' Cc The Icebreaker
hapo ungeongeza kumtag Mfalme Suleiman aje ampe mwongozo mtoa mada jinsi Gani ya kula Raha za Dunia Kwa gharama kubwa.

Kama unayajua maandiko ya kiyahudi Mpe mwongozo juu ya menu ya chakula na vinywaji kwenye jumba la mfalme Kwa siku halafu na idadi ya pisi Kali za Kiyahudi,kihabesh,kirumi,kimisri

kigalatia,kiyunani,kisamaria nk nk alizochakata mfalme Kwa siku

Mtoa mada afanya masikhara

Ponda Raha kufa kwaja shekh!
 
Bila shaka,lengo la mleta mada ni kuikumbusha jamii ambayo ina maisha mazuri kuwakumbuka na wanao pata tabu kama vile watoto yatima.
Naungana nae katika lengo hilo lakini sioni kama alikuwa na haja ya kutumia kauli hiyo.

Kuna watu watasaidia hao mayatima na wasiojiweza na wajane lakini bado kasi yao ya kula bata itakuwa pale pale hutaona wamepungukiwa chochote.

Sasa mtu kama mtoa mada anaweza kuendelea kupiga majungu kwa kusema mtu huyu anakula bata huku kuna watu ni maskini wanapata dhiki kumbe kuna watu hawakaukiwi hata wasaidie vipi wengine.

Haya ni maoni yangu tu lakini
 
Hilo swali lako ni sawa na mtu aulize eti 'Kuna faida gani ya kula chakula kizuri wakati unajua mwisho wake utaenda kukiacha chooni?'
Mtu ule vitu vya ajabu wakati vitu vizuri vipo?

Mtu uishi maisha ya hovyo wakati maisha mazuri yapo?

Wewe pambana uwe na maisha mazuri, ukishindwa sasa matokeo yake zinakuja hoja kama hili swali lako.

Isitoshe Tatizo limekuja hapo kwenye 'kuweka hazina mbinguni'

Mimi siamini katika mbingu (kwenda mbinguni?)
 
Mungu anasema kuwa “Nitakupa hazina iliyofichwa gizani”
Ibrahim, Isaac, yakobo, Ayubu na wengine pia walikuwa ni matajiri sana idadi kubwa ya mifugo Ndo utajiri wenyewe.
 
Back
Top Bottom