Tafakuri kuhusu MUUNDO, UJENZI na MWELEKEO wa Taifa letu (Part II) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafakuri kuhusu MUUNDO, UJENZI na MWELEKEO wa Taifa letu (Part II)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shayu, Feb 24, 2012.

 1. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  Sasa tunatambua kwamba Taifa linaundwa na watu wa aina mbalimbali kama nilivyoongea katika andiko la kwanza, Sehemu ndogo ikiwa familia, niliandika umuhimu wa familia katika ujenzi wa Taifa imara, nilizungumzia kuhusu maadili ya familia na umuhimu wake katika ujenzi wa Taifa. Nilisema kuna uhusiano mkubwa sana kati ya kumomonyoka kwa maadili katika familia na katika Taifa, Lakini pia order katika Taifa na katika familia.

  Matokeo ya familia zisizokuwa na maadili yanadhihirika katika jamii kutokana na malezi hafifu, Hivyo ni muhimu sana kwa viongozi wa familia kulea watoto katika maadili mema ili Taifa liwe na mwelekeo na maadili mema, Tusijidanganye kama tutapata viongozi wazuri pasipo maadili ya familia, wazazi lazima wawe na uwezo wa kuwatiisha watoto wao na kuwaonyesha mwelekeo.

  Lakini pia Jukumu la malezi ya watoto ni la wazazi wote walioko katika jamii, bila jitihada za pamoja za kuwatiisha kuwaonyesha mwelekeo hatutafanikiwa kama Taifa, Kwahiyo tunatambua kwamba familia ni taasisi ndogo katika Taifa na ina kiongozi wake, uimara wa serikali za mtaa unategemea sana uimara wa familia zinazounda mtaa huo na mahusiano yao katika malezi na shughuli mbalimbali za kujiletea maendeleo yao wenyewe, mlolongo huu unapanda kutoka chini kwenda juu. Bila order hii itakuwa vigumu mno kwa serikali kutawala nchi na kuwa yenye kuzalisha.

  Kwahiyo ni muhimu ku organize watu wetu ili Taifa liwe na maendeleo na organization hii inaanzia kwenye familia. Ni ukweli usiopingika mtu anayeharibu familia, huharibu kiini cha Taifa, Kama taifa likiwa na watoto wavuta bhangi, wahuni nk, ni nani atakayeendesha Taifa katika usalama? Kwahiyo familia ni kitu cha kulindwa na watu wote. Hali tuliyonayo sasa inachangiwa pia na kushindwa kwa uongozi katika familia na adhari hizi zinaibukia katika utaifa na tunashangaa ni nini chanzo.

  Familia yenye wazazi wawajibikaji na wanaotiisha watoto wao, familia yenye kuzalisha na kuwekeza ziada ndio msingi wa kwanza wa Taifa imara, tukiisha kuwa na familia za namna hii ni kazi ya serikali sasa ku organize familia hizo kuunda kitu kimoja kinachoitwa Taifa na kuwa na dira moja.

  Lakini ni muhimu pia kwa wazazi kuwafundisha watoto wao umuhimu wa Taifa hili, kuwafundisha kulipenda na kulitumikia lakini pia kuipenda miji yao na kuilinda. Kwahiyo tuna wajibu wa mzazi kwa familia na wajibu wake pia kwa Taifa na jamii. Na huu ndio uraia wa kweli uwajibikaji wa mawanchi katika ujenzi wa Taifa lake mwenyewe kwa faida ya watoto wake na vizazi vya Taifa kwa ujumla. Jitihada hizi za pamoja ndizo zitakazo nyanyua Taifa hili kutoka hapa lilipo.

  Nitaendelea na tafakari kuhusu ujenzi, muundo na mwelekeo wa Taifa letu kwa kuchambua nini ''MANTIKI'' watu kuishi katika Taifa.

  TAFAKARI KUHUSU MANTIKI YA TAIFA

  Nimekuwa nikisoma na kutafakari kuhusu asili ya watu kuishi katika Taifa, na ni nini faida za kuishi pamoja kwa muda mrefu sasa, sababu ya kufanya hivyo ni kutokana na mwelekeo wa Taifa letu ulipo sasa. Sitapenda sana kujadili matatizo bali njia ambazo zitatuwezesha kutoka hapa.

  Taifa ni kama organization ni mkusanyiko wa watu ambao wana malengo mamoja ambayo wanataka wayafikie kwa pamoja. Malengo hayo wanaamini yatabadilisha maisha yao kuwa mazuri zaidi, yenye amani na utulivu lakini pia tunaishi pamoja ili kujilinda na kuhifadhi vizazi vyetu hiyo ndio asili ya Taifa.

  Sioni kama kuna faida yeyote ile kama kuwepo katika taifa hakuna faida yeyote bali madhara. Kwahiyo uwepo wa Taifa lolote lazima uwe na malengo fulani ambayo watu hao wamejikusanya ili wayafikishe na malengo hayo lazima yawe ni mazuri yenye kujenga jamii yenye furaha na maendeleo.

  Nilizungumza hapo mwanzo Taifa ni kitu kimoja kikubwa, chenye sehemu ndogo ndogo ambazo zinahitaji kuunganishwa ili Taifa lifanye kazi katika umoja. Nimezungumza kuhusu familia kama sehemu ndogo katika Taifa ambayo watu ambao wamo humo wana makabila yao na dini zao ili Taifa lolote lifanye kazi lazima muundo wake uwe katika kuleta umoja na maendeleo ya watu wote.

  Maendeleo makubwa ya binadamu yamefikiwa pale tu binadamu walipoamua kuishi pamoja kama Taifa, lengo la Taifa ni kupunguza matatizo ya binadamu na sio kumwongezea kama kuwepo katika Taifa ni chanzo cha migogoro vurugu na vujo hakuna haja ya kuishi katika Taifa. Hii ni dhahiri maisha ya binadamu yamekuwa na ahueni baada ya kuishi katika jumia katika Taifa, wakisaidiana katika ujenzi wa jamii zao katika mwelekeo fulani ni lazima kuwe na mwelekeo katika Taifa.

  Nitaongea tena na tena katika maandiko yangu kuhusu ubinafsi ni kinyume na nature ya watu kuishi katika Taifa, ubinafsi unua bond ya watu walioamua kuishi katika Taifa kwa faida ya wote, Hatutaweza kuendelea kama kila mtu akijiangalia mwenyewe badala ya kukiangalia kile kilichotufanya tuwe Taifa, tutakosa mwelekeo tukiendelea kuwa hivyo na Mantiki yote ya sisi kuishi katika Taifa itatoweka. Mtu mbinafsi hawezi kuzingatia Haki, tunajua asili ya kutotenda haki ni kutenganisha watu lakini Haki huleta watu pamoja, huleta furaha na kuridhika.

  Mifumo yote tuliyounda ni lazima iwe ni kwa faida ya jamii, lazima muundo wote ufanye kazi kama kitu kimoja ili Taifa letu lisonge mbele, Mantiki ya kutumikia jamii ndio msingi lazima tujue kwamba sisi tuliopo duniani sasa hivi tunawajengea baadae watoto wetu, baadae ya watoto wetu inatutegemea sisi, ni lazima tuwe na ushirikiano katika ujenzi wa Taifa hili.

  Kwahiyo tumeisha tambua haki huunganisha watu na dhuluma hutenganisha watu na kwamba Taifa halitakuwa salama kama halitazingatia haki ni wajibu wa serikali kufuata utawala wa sheria ili watu wa taifa ili waendelee kuwa wamoja, ni wajibu pia wa kujenga usawa na haki kila mtu apate faida kutoka na na kazi na juhudi zake na sio ujanja ujanja na utapeli.

  Nilizungumza Taifa lazima liwe na dira, lazima liwe na mwelekeo lakini ili kufikisha malengo hayo na dira hiyo, Taifa lazima liwe na elimu itakayowezesha watu wake kufikia huko, ndipo inakuja mantiki ya kusomesha watu, Taifa haliwezi kumsomesha mtu ili apate faida binafsi bali awe na mchango katika jamii.

  Hatutaweza kukua na tukawa Taifa lenye nguvu kama tutaendelea na ubinafsi wetu na kusahau majukumu yaliyotufanya kuwa Taifa kama hatutajali hilo. Lakini hili tatizo madhara yake ni makubwa. Upendo na kujaliana kwa watu kunapopungua wakati kila mtu anapojiangalia mwenyewe huleta vurugu na fujo na madhara yake ni vita kile kidogo tulichokipata kwa kudhulumiana kitapotea nacho ni uchaguzi wetu kuchagua njia sahihi kufanya mapito yetu kama Taifa sio ufisadi na ubinafsi.

  Kwahiyo Taifa limesomesha watu sio kwa faida yao binafsi bali ni katika ujenzi wa Taifa hili kwa faida ya wote ama sivyo hakuna mantiki ya kumsomesha mtu, hakuna sababu hata moja. Kusomesha watu na kuwa waharibifu badala ya wajenzi hakuna mantiki, huu ni ujinga! na kusahau majukumu yetu kama watu wa Taifa moja. Kwahiyo tumesomesha watu ili wawe na faida kwa Taifa na kwa mtu mmoja mmoja kila mtu katika fani yake lazima tujenge taifa letu katika misingi ya maadili na ustaarabu ili tuendelee na tuwe na mwelekeo kama Taifa.

  itaendelea Tafakari mihimili mitatu ya dola katika kuleta mwelekeo wa TAIFA.
   
 2. M

  Madesa Member

  #2
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Double likes Shayu, nimependa ujengaji wako wa hoja na mafundisho/mada hizi ndo tunazozitaka kwa wingi humu, najiskia faraja kujifunza kitu baada ya kusoma mawazo ya mtu mwingine.
   
 3. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #3
  Feb 27, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  Pamoja mkuu nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu kutafakari na kuwa mzalendo''
   
Loading...