Tafakuri: Kauli ya Rais Magufuli ni msumari wa moto kwa Wafungwa

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,491
26,977
Ndugu zangu!

Ni kweli kwamba wafungwa wanapaswa kuzalisha ili kujihudumia kwa kiasi kikubwa. Badala ya kuwa sehemu ya mateso na mzigo kwa serikali, mazingira wezeshi ni muhimu ili kufanikisha hilo.

Wafungwa ni watu wa aina zote, wenye kila aina ya ujuzi chini ya jua. Wakitumika vema ni rasilimali yenye manufaa, nami naunga juhudi kuwa washiriki katika shughuli za uzalishaji kila mmoja kwa ujuzi wake.

Pia ikiwezekana sehemu ya kile wanachozalisha wapatiwe ili kuhudumia familia zao, au wawekewe akiba ili siku wakimaliza kifungo kikawafae huko uraiani.

Lakini kwa kauli ya Rais kwa Askari Magereza sioni kama imetafsirika kwa usahihi.

Rais anawashangaa askari kushindwa "kunufaika" na uwepo wa wafungwa, kwamba wafungwa ni 'watumwa' wa bure.

Kwamba Askari wanakwama wapi, walipaswa kuwatumikisha watakavyo wafungwa kwa manufaa yao!

Akaenda mbali zaidi na kutamani angekuwa yeye Askari Magereza!

Nimetafakari kauli hii imeniacha na maswali mengi, nilichokiona hapa ni kwamba wafungwa wajiandae kisaikolojia, wanakwenda kukiona cha moto.

My take:
Jela ni kwa mtu yeyote, kwa wenye makosa ni sehemu ya kurekebisha... lakini pia cheo ni dhamana.

Ncha Kali.
 
Nimetafakari kauli hii imeniacha na maswali mengi, nilichokiona hapa ni kwamba wafungwa wajiandae kisaikolojia, wanakwenda kukiona cha moto.

My take:
Jela ni kwa mtu yeyote, kwa wenye makosa ni sehemu ya kurekebisha... lakini pia cheo ni dhamana.
Hivi yule mtoto wa dada yake Mkurugenzi Singida aliyeua mtu kwa risasi kanisani Sabato alifungwa miaka mingapi?
 
Back
Top Bottom