masatujr1985
JF-Expert Member
- Oct 27, 2011
- 1,980
- 780
Salaam ndugu wana jamvi,
Naandika andiko hili kwa kujaribu tu kutafakari ni kwa namna gani Mh. Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli atakavyokuwa anahangaika kupanga safu ya kiutendaji katika kutimiza muhimili wa tatu wa serikali yaani Baraza la Mawaziri lakini wale wanaosubiri kuteuliwa wakiwa matumbo joto kubaini kama wamo ama la!!!.
Ninachokiona hapa ni kuwa wakati Mh. Rais akiendelea na zoezi hilo gumu, upande wa pili wa wanasiasa ambao wamekaa mkao wa kusubiri ni nani atatangazwa hasa hasa wale wa chama tawala nauona kama ni mgumu zaidi hata ya mteuaji mwenyewe. Kwa nini nasema hivyo, ni kutokana na muda uliopita sasa toka Mh. Rais aingie Ikulu na kumteua Waziri Mkuu na takribani siku 33 sasa fumbo la baraza halijafumbuliwa!!!
Sasa ninachokiona ni kuwa jamaa watakuwa wanahaha hapa, huku na kule kuulizia ulizia kama jamaa amewakumbuka kila uchao. Hii ni kawaida kwa mwanadamu anapokuwa anasubiria jambo positive ambalo anadhani anaweza kuwa muathirika kwa namna moja ama nyingine lakini akalikosa.
Nadhani kama Mh. Rais anakuwa accessed kwa simu basi natumai simu zile za naomba uniteue ama za kuombewa fulani ateuliwe zitakuwa ni nyingi ama zimepungua kutokana na kasi ya mapacha watatu (Rais, Makamu na WM).
Ni tafakuri tu juu ya purukushani za kuteuliwa kuwa mmoja ya mawaziri wa serikali ya JPM.
Wewe unatafakuri ipi?
Wakatabahu