Tafakuri juu ya picha ya Habari Leo na hatma ya Ikulu yetu

Chief Isike

JF-Expert Member
Jan 17, 2010
445
462
Wakuu nafikiri kuna umuhimu wa kufanya tafakari juu ya picha ya front page ya Gazeti la Habari Leo (state or public media?) toleo la leo. kuna picha pale na maelezo (caption) yafuatayo;

Mwakilishi wa Televisheni ya Emmanuel ya The Synagogue Church Of All Nations, Martha Harvey akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete mkoba wenye Sh. milioni 25 kwa ajili ya waathirika wa ajali ya Meli ya Mv Spice Islanders iliyozama na kusababisha vifo vya mamia ya watu hivi karibuni. Mchango huo ulikabidhiwa Ikulu, Dar es Salaam jana, ulitolewa na Kiongozi wa Kanisa hilo, Nabii Themitope Balogun Joshua, ambaye anaishi makao makuu ya kanisa hilo, Lagos, Nigeria (Picha na Freddy Maro)

Few concerns to start with in loud thinking/brainstorming

1. Kwa nini huo msaada umekabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Ikulu, kulikuw ana ulazima sana wa msaada huo kukabidhiwa kwa rais? Mbona tumeona misaada mingi tu imepelekwa kwa hao waathirika ama moja kwa moja au kupitia kwa viongozi wengine waandamizi na wasiokuwa waandamizi huko huko Zanzibar. Kwangu mimi hata kama huo msaada ungepelekwa Zanzibar si lazima (si sahihi) kuukubadihi Ikulu kwa Dkt. Shein. Hapa inatafutwa attention, Je ni ya kitu gani? Think loud. Je Rais anajua hilo?

2.Another thing very important to brainstorm too ni juu ya MTOAJI MSAADA. Jamani huyo si ndiye aliyetajwa kuwa amemtabiria na kumwombea Edward Lowassa kuwa rais wa nchi hii. Tena ikaelezwa kuwa waziri mkuu huyo wa zamani amemtembelea huyo kiongozi wa kanisa hilo huko Lagos, mapema mwaka huu I think. Huyo si ndiye alikuwa akizungumzwa katika kile kimemo cha B. Shellukindo kwenda kwa Pindi Chana? Tehe tehe tehe, so sasa ametuma msaada Tanzania na umepokelewa na rais. Tehe tehe tehe! What is he trying to introduce here, his influence or his church? Kwa mgongo wa Ikulu na Rais?

3. La mwisho kwangu, nalo la muhimu sana kujadili ni aina ya watu ambao Rais amekuwa akikutana nao Ikulu yetu. Wengi wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kujitangaza hivyo kumtumia rais wetu na IKULU YETU kwa matangazo na manufaa yao binafsi zaidi. I remember one of the very recent disgusting event ni ile ambayo Nizar Khalfan akiwa amevaa jeans, tena mlegezo nyuma, very informal, aliruhusiwa kuingia Ikulu, akapiga picha na rais kwa mkutano rasmi eti akimkabidhi jezi anayochezea katika klabu yake huko aliko! Haya bwana. Kuna mengi ya kujadili I think
 
3. La mwisho kwangu, nalo la muhimu sana kujadili ni aina ya watu ambao Rais amekuwa akikutana nao Ikulu yetu. Wengi wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kujitangaza hivyo kumtumia rais wetu na IKULU YETU kwa matangazo na manufaa yao binafsi zaidi. I remember one of the very recent disgusting event ni ile ambayo Nizar Khalfan akiwa amevaa jeans, tena mlegezo nyuma, very informal, aliruhusiwa kuingia Ikulu, akapiga picha na rais kwa mkutano rasmi eti akimkabidhi jezi anayochezea katika klabu yake huko aliko! Haya bwana. Kuna mengi ya kujadili I think
Rais wetu ni mtu wa watu hivyo hana ubaguzi kwa mtu anayeenda ikulu kukutana naye.
Juu ya Msaada uliotolewa kutoka kwa mchungaji kwenda kwa waathirika wa meli, sina hakika kama ni kosa kwa rais kupokea...
 
Yawezekana (RA)- CHEL anapiga ndogondogo ili asivuliwe gamba, kwani utabiri wake utakuwa kama wa Shekhe Yahaya.
 
Mbona hukuuliza uhalali wa rais kutangaza siku tatu za maombolezo???
Watoa misaada walimuona rais akiwa ameguswa na kutangaza maombolezo hivyo wakaona ni busara kumfariji kwa kutoa kwa wafiwa kupitia kwake, sioni cha kuanza kuhoji hapo........labda kama msaada hautafika hapo ndipo uhoji.
 
tb joshua ajitangaze bongo kupitia ikulu daaaaaaah. niliangalia ile misa yote hakuna sehemu tb joshua alisema lowassa atakuwa rais wa tz ni uzushi mtupu na huwa inarudiwa mara kibao tu emmanuel tv. Hilo la kutoa msaada ikulu na kuingia ikulu awamu hii ni juhudi zako tu mwenyewe wala usilalamike km hujaweza ingia huko usipike majungu JK hana hiana na ile nyumba ni ya wa TZ wote! so mkuu fanya research kwanza kabla hujaandika kitu TB Joshua and his ministries is larger than haka ka ikulu kenu ka bongo so kujitangaza eti kupitia huko ni kichekesho. hii yote inaonekana una chuki mbayaaaa tena mbayaaa na LOWASSA.
 
Ikulu si safi tena inanuka uvundo, hivyo kila mtu anaweza kuingia kama unakwenda ferry vile.
 
Kwani zanzibar na huku bara kuna tofautı ganı?
 
Duh! Huyu papa sijui atatufikisha wapi! Waacheni tu wajilimbikizie. Wao wana pesa Nasi tu MUNGU..
 
Jk hana la kufanya!rais picha tuu!matatizo kibao lakini hajajitokeza kuelezea jinsi ya kuyatatua
 
Kupokea msaada is not a big deal!! But,raisi wetu anatatizo la msingi sana kichwani,ni raisi cheapest never happened in this country and worldwide.Yaani wewe ukifanya upuuzi fulani tu nenda ikulu,mimi naona mwezi ujao nitaenda ikulu...Ni kweli raisi anapaswa awe mtu wa watu lakini kuna miiko ya uraisi...

Na ukweli ni kwamba kuwa mtu wa watu hakupimwi kwa kupiga picha na watu,ila unawatendea nini? Picha sio issue kabisa...

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere sijawai kuona akipiga picha na wahuni au kutembelewa na kila mtu pale ikulu...lakini kila mtanzania hata wa chekecheka anatambua mchango wake...na amekuwa mtu wa watu kwa ajili hiyo..JK ana tatizo..
 
Mie sioni sababu pia ya wewe kutupa attention ya issue hii, mawazo yako na fikira zako kuhusu EL inaonekana ndiyo yanayokupa utumwa wa kufanya negative kila kitu kutoka SCOAN, you just be objective in your thinking hutaona shida ya msaada uliotolewa. By the way, mbona watu wengi tu wametuma salaam za rambrambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano?
 
kama anapiga picha na 50cents itakuwa kupokea msaada wa waathirika?
 
Reginald Mengi alitoa mil 40,, lakini hakwenda Ikulu.

Huyo alikua anatafuta recognition na attention tu.
 
Back
Top Bottom