Tafakuri: Hatma ya Tanzania mikononi mwa Watanzania

vasilius

Member
Feb 28, 2017
10
17
Tanzania haiwezi kuendelea na kamwe haitoendelea muda wa kuwa CCM ndio inaongoza Dola. Kwa nini nasema hivi?

Kwasababu Dola imefunga ndoa na CCM na CCM imefunga ndoa na Dola. Kumbuka mtoto wa nyoka ni nyoka. CCM wanajiona wao ndio wenye Dola na waliopo kwenye Dola wote wanajiona ni CCM.

Watanzania ndio wanatakiwa kuivunja ndoa ambayo isiyo halali kati ya CCM na Dola na wala sio vyama vya siasa vya upinzani kama wengi wanavyotegemea.

Watanzania wanatakiwa wawe na Imani Dola iliyopo madarakani ni kwa ajili yao na waliopo madarakani wajue wajibu wao ni kwa Watanzania na sio chama chochote.

Hapa nazungumzia kupigania kuwa na KATIBA ambayo inampa Mtanzania nguvu ya kuisimamia nchi yake. Kuwa na Bunge ambalo litaishauri na kuiwajibisha serikali pale inapokosea na sio kupongezana au Bunge lenyewe kuwa sehemu ya serikali.

Kuwa na Mahakama huru na sio kuwa na Majaji ambao wanateuliwa na kupewa maelekezo na viongozi wa serikali. Katiba ambayo pia itaweka tume huru ya uchaguzi na sio viongozi wa tume kuteuliwa na mtu ambaye yeye mwenyewe ni mgombea.

Rais kuweza kushtakiwa akivunja katiba au kufanya kosa la jinai na kupunguza madaraka ya yake ya ufalme. Kuondosha uongozi ambao hauna tija kwa wananchi isipokuwa kwa chama (Mfano: Wakuu wa mikoa na wilaya. Kama itakuwa ni muhimu kuwepo basi wachaguliwe na wananchi). Na mengineyo ambayo yataimarisha demokrasia na kuleta, haki za binadamu, uhuru wa kutoa maoni na kuleta maendeleo.

Tofauti na hapo tutaendelea kulaumu na kulaani kila siku. Tutawalaumu vyama vya upinzani hawajatumia nguvu ya kutosha kupigania #katibampya na tumehuru ya uchaguzi wakati sio wajibu wao peke yao.

Pia tutaendelea kulaumu CCM kwa kuuwa demokrasia nchini na kukandamiza vyama vya upinzani wakati wanajua wao wafanye hivyo wasifanye hivyo hamuwezi kuwafanya chochote kwa sasa.

Sasa hivi katika Dola kila kitu ni CCM na kila mtu ni CCM. Narudia tena kila kitu ni CCM. Imefikia wakati sasa hivi huwezi kupewa cheo chochote bila kuwa CCM. Hata vile ambavyo havihitaji siasa pia huwezi kupewa bila kuwa CCM, mfano kuwa injinia wa manispaa pia kwa sasa huwezi bila kuwa CCM. Ndio maana miradi mingi inakuwa chini ya kiwango.

Tunachoweza kupata kwa sasa kutoka ni unafuu tu wa kupata kiongozi mwenye busara tunapiga hatua moja mbele. Ila tukipata kiongozi mpumbavu tunarudi nyuma hatua mbili.

Katika hali kama hii je Tanzania itaendelea? Watanzani wenzangu kutegemea viongozi wa dini, wasanii na viongozi wastaafu tena wale wa CCM kukemea kila baya na ovu linalofanywa na serikali ni sawa na kusubiri gari la kwenda Zanzibar ukiwa Dar es Salaam.

Kuna ambao wanashangaa kuna Watanzania wanafurahia utawala wa CCM wakati muda na maendeleo yaliyopatikana haviendani. Ukweli ni kwamba kila kinachokunufaisha lazima ukifurahie.

Ukweli wao wananufaika na CCM kuwepo madarakani. Isipokuwa mwenye akili tu ndio hupima je kila kinachomnufaisha kina manufaa. Kama jambo ni la umma linakunufaisha wewe binafsi halina manufaa.

Lakini kama ni la umma linanufaisha umma basi lina manufaa.

Mwisho kwa wale ambao wanaona siasa haiwahusu. Pambana tafuta mali mwisho ukishazipata katika utawala dhalimu watakunyang’anya tu.

Utanyang’anywa kwa njia ya kodi isiyostahiki au kwa njia ya mashtaka ya kuhujumu uchumi. Hii ni tafakuri yangu tu. Nawe pia haukatazwi kutafakari. Je ndoa ya CCM na Dola iendelee au ife tuwe na ndoa kati ya Dola na Watanzania?

Ahsanteni,
Wako Tafakuri ya kina.
 
Hakuna tatizo, wananchi wameridhika ndo maana kuna utulivu. Haijalishi ni nn serikali inafanya, ukiona utulivu ujue watu wameridhika. Siku wasiporidhika utaona tu matokeo wala hata hutatumia nguvu za kuandika makala. Cc'm baba Lao.
 
Hakuna tatizo, wananchi wameridhika ndo maana kuna utulivu. Haijalishi ni nn serikali inafanya, ukiona utulivu ujue watu wameridhika. Siku wasiporidhika utaona tu matokeo wala hata hutatumia nguvu za kuandika makala. Cc'm baba Lao.
Siamini kama wakati mwingine utulivu huletwa na kuridhika. Kuna wakati utulivu huletwa na kutojitambua. Naheshimu mawazo yako lkn hata sasa wapo wengi tu wasioridhika na bado wametulia. Mimi situmii nguvu sana kuandika, nguvu yangu ya kuandika jambo km hili ni sawa na chozi la samaki ktk bahari. Kwa hiyo usiumie sana kuandika kwangu huku endelea kukatika viuno na kuimba ccm baba lao, hao unao waimbia wanakula nchi na wewe utabaki kuimba tu.
 
Mku jaribu pia kutafuta ushauri kwa Mze Sumaye uone ana lipi la kusema huko upinzani kama Demokrasia ipo au wote wanasiasa ni walewale.
 
Siamini kama wakati mwingine utulivu huletwa na kuridhika. Kuna wakati utulivu huletwa na kutojitambua. Naheshimu mawazo yako lkn hata sasa wapo wengi tu wasioridhika na bado wametulia. Mimi situmii nguvu sana kuandika, nguvu yangu ya kuandika jambo km hili ni sawa na chozi la samaki ktk bahari. Kwa hiyo usiumie sana kuandika kwangu huku endelea kukatika viuno na kuimba ccm baba lao, hao unao waimbia wanakula nchi na wewe utabaki kuimba tu.
Tukiwapa Chadema mutarekebisha wimbo au itakuwa ni yaleyale?
 
Mku jaribu pia kutafuta ushauri kwa Mze Sumaye uone ana lipi la kusema huko upinzani kama Demokrasia ipo au wote wanasiasa ni walewale.
Upinzani ni nchi gani? Bahati mbaya mimi sipo huko nipo Tanzania. Kama ilikuwa unamaanisha vyama vya siasa vya upinzani pia bahati mbaya mimi sio mwanachama wao. Ninaumizwa na Tanzania inavyoendeshwa halafu tunategemea matokeo chanya. Naamini hata hao wapinzani siku wakichukua Dola na kufanya kama haya wanayofanya CCM nitaongea tu kwa sababu ni haki yangu.
 
Back
Top Bottom