TAFAKURI CWT: Kwani umoja wa walimu hawawezi kumiliki kampuni/kitengo chao cha ujenzi wakawa wanajenga shule zao wenyewe kama wafanyavyo SUMA JKT?

Wanapewa t-shirt kwisha wanabaki wakichekelea kumbe wanapigwa

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Kwa kweli wanaonewa sana, halafu hawapati manufaa yeyote.

Imagine Mwl anakatwa 14,000 kwa mwezi manake ni sawa na 168,000 kwa Mwaka ambayo ni wastani wa mifuko 10 ya Cement

Hapo bado hawajakatwa na hela za Vyama vya wafanyakazi sijui TAGWLU na wenzao TUGHE yaani kote ni Mchwa tu.

Pole zao kwa kweli
 
Boss, hongera wewe kwa kuwa na kichwa kilichojaa ufahamu...
Dunia ina- operate kwa principles usidhani mambo yanaendaenda tu! Wewe unadhani kwa nini Tanzania tunasema uchumi unakua lakini Vijana wanalia ajira hakuna?!
Symptom kubwa ya uchumi ambao hau- perform ,mojawapo ni Unemployment.
Sasa mawazo primitive kama haya yako ndo yamekuza vitu vya ajabu ajabu kama "force account" ,"local fundi' , Suma JKT, TBA,NHC n.k kuwa Wakandarasi na kuminya ajira kwa watu walioelimika (wasomi).
Wekezeni katika kusaka maarifa na siyo kuwekeza kwenye mawazo ya kijinga!
 
Ushaona hesabu za SUMA?

Ulishaona hesabu za NSSF?

Ulishaona hesabu za mashirika yeyote ya serikali?

Nakusisitizia ni HASARA TUPU!

Nenda kasome financial reports halafu uje hapa
Na walipoona yule CAG makini na mtu wa Mungu wakaamua kumla kichwa ili kuondoa udhia...
 
CWT na SUMA JKT ni taasisi mbili tofauti zenye malengo tofauti.

Kazi ya CWT ambacho ni chama cha wakimu kilichoanzishwa na walimu ) ni kumtetea mwalimu na kuhakikisha anapewa haki zake kutoka kwa Mwajiri wake ( serikali ).

Wakati SUMA JKT siyo chama cha kiharakati ila ni Shirika la Uzalishaji Mali la JKT- SUMA JKT.
Kuwa na majengo makubwa pia ni malengo ya CWT? Kama jibu ni ndiyo basi wanaweza kuwa na kitengo cha ujenzi pia...
 
Kuwa na majengo makubwa pia ni malengo ya CWT? Kama jibu ni ndiyo basi wanaweza kuwa na kitengo cha ujenzi pia...
CWT imeshapoteza DIRA. Imekuwa ni kama BAKWATA.

Kupoza walimu ili mwajiri awe na amani huku wakiwapiga hao walimu. Ni mwendo wa kutafuta nafasi CWT upige.

Walimu nchi hii ni punching bag aka Kichwa cha mwendawazimu.

Kila takataka inaweza kujifunzia kunyoa.
 
Kuwa na majengo makubwa pia ni malengo ya CWT? Kama jibu ni ndiyo basi wanaweza kuwa na kitengo cha ujenzi pia...

Jengo la mwl house ule Ni mradi wa chama na ofisi za chama... CWT wameanzisha benki lkn nayo Ni njia ya upigaji tu...
 
CWT na SUMA JKT ni taasisi mbili tofauti zenye malengo tofauti.

Kazi ya CWT ambacho ni chama cha wakimu kilichoanzishwa na walimu ) ni kumtetea mwalimu na kuhakikisha anapewa haki zake kutoka kwa Mwajiri wake ( serikali ).

Wakati SUMA JKT siyo chama cha kiharakati ila ni Shirika la Uzalishaji Mali la JKT- SUMA JKT.
Kwanini wanajeshi wazalishe mali lakini walimu wasizalishe mali?
 
SUMA JKT hakuna faida mle

Mle ni kitengo cha wakubwa kujipigia

Suma JKT is a useless money burning department

Na huo ushauri unaotoa kwa CWT the same fate...mali ya jumuia si mali ya yeyote,watapiga kama ilivyo kawaida

NSSF ni kipigo kwenda mbele...

Kampuni zote za serikali ni hasara,vipigo vitupu hakuna kampuni inamilikiwa kijumuia au serikali ilishawahi jenga faida popote

Mahasara matupu haya
Umenikumbusha enzi za nyerere,,nilivyokula hela za mashirika ya umma,,asee nilipiga pesa hatari
 
SUMA JKT hakuna faida mle

Mle ni kitengo cha wakubwa kujipigia

Suma JKT is a useless money burning department

Na huo ushauri unaotoa kwa CWT the same fate...mali ya jumuia si mali ya yeyote,watapiga kama ilivyo kawaida

NSSF ni kipigo kwenda mbele...

Kampuni zote za serikali ni hasara,vipigo vitupu hakuna kampuni inamilikiwa kijumuia au serikali ilishawahi jenga faida popote

Mahasara matupu haya
Kumbuka pia CWT sio mali ya serikali mkuu bali kile ni chama cha kutetea haki na maslahi ya walimu.
 
Habari zenu waheshimiwa wa humu jamiiforums.

Eti ndugu zangu;

Kwani umoja wa walimu hawawezi kumiliki kampuni/kitengo chao cha ujenzi wakawa wanajenga shule zao wenyewe (Primary & Secondary) kama wafanyavyo SUMA JKT?

Kwanini tenda apewe mkandarasi mwingine wakati walimu wanaweza kuunda umoja wao kisha wakafungua kampuni kuuuubwa sana ya ujenzi wakawa wanachukua tenda za ujenzi wa shule za msingi pamoja na secondary.

Kwani CWT si ni chama cha walimu Tanzania? Au mimi ndio sijui? Yale makato wanayoyapata kutoka kwa walimu si wanaweza kukusanya mtaji wa kutosha wa kufungua kampuni ya ujenzi na kuwa wanapiga pesa ya maana?

NB: Mimi Infantry Soldier sio askari jeshi wala mtumishi wa ofisi yoyote ya serikali bali ni raia mwema ninayeipenda sana Tanzania yangu.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Mawazo ya kitoto haya.
Mwalimu atatumia hela gani na kwa msukumo upi
Halafu kwako wewe chakula chote unachokula kwa nini usilime mwenyewe?
 
Huo ni corellative example.
Kama waalimu inabidi wajenge shule, basi hata wewe ulime unachokula.
Mbona walipojenga jengo la kitega uchumi hamkuwapinga? Tena wakaamua kuweka na ofisi zao humo humo...!!!

Sasa inakuwaje wao kuanzisha kampuni ya ujenzi mnapiga kelele namna hii?

Katika suala la chakula mbona wanakijiji wanalima mahindi yao kama chakula huko vijijini?
 
Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom