TAFAKURI CWT: Kwani umoja wa walimu hawawezi kumiliki kampuni/kitengo chao cha ujenzi wakawa wanajenga shule zao wenyewe kama wafanyavyo SUMA JKT?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,316
Habari zenu waheshimiwa wa humu jamiiforums.

Eti ndugu zangu;

Kwani umoja wa walimu hawawezi kumiliki kampuni/kitengo chao cha ujenzi wakawa wanajenga shule zao wenyewe (Primary & Secondary) kama wafanyavyo SUMA JKT?

Kwanini tenda apewe mkandarasi mwingine wakati walimu wanaweza kuunda umoja wao kisha wakafungua kampuni kuuuubwa sana ya ujenzi wakawa wanachukua tenda za ujenzi wa shule za msingi pamoja na secondary.

Kwani CWT si ni chama cha walimu Tanzania? Au mimi ndio sijui? Yale makato wanayoyapata kutoka kwa walimu si wanaweza kukusanya mtaji wa kutosha wa kufungua kampuni ya ujenzi na kuwa wanapiga pesa ya maana?

NB: Mimi Infantry Soldier sio askari jeshi wala mtumishi wa ofisi yoyote ya serikali bali ni raia mwema ninayeipenda sana Tanzania yangu.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Ni wazo zuri, ila litaendeleza kudidimiza sekta binafsi /kampuni za ujenzi.
Hata hivyo ni vigumu kwa kuwa CWT sio wamiliki wa shule bali ni waajiriwa/wasimamizi wa miradi katika shule tajwa kwa idhini ya kamati za shule /mabalaza ya kata /vitongoji /vijiji.
 
Haya ndio mawazo mazuri kwa kipindi hiki cha mfumo wa kujiajil mkuu umeona mbali na hii ndio tofauti ya jf na majukwaa mengine ya kijamiiii
 
CWT na SUMA JKT ni taasisi mbili tofauti zenye malengo tofauti.

Kazi ya CWT ambacho ni chama cha wakimu kilichoanzishwa na walimu ) ni kumtetea mwalimu na kuhakikisha anapewa haki zake kutoka kwa Mwajiri wake ( serikali ).

Wakati SUMA JKT siyo chama cha kiharakati ila ni Shirika la Uzalishaji Mali la JKT- SUMA JKT.
 
CWT na SUMA JKT ni taasisi mbili tofauti zenye malengo tofauti.

Kazi ya CWT ambacho ni chama cha wakimu kilichoanzishwa na walimu ) ni kumtetea mwalimu na kuhakikisha anapewa haki zake kutoka kwa Mwajiri wake ( serikali ).
CWT wanamiliki vitega uchumi kama vile jengo la ghorofa pale Ilala Dar hii ipo wazi na inajulikana na kila mtu...
 
Kila taasisi ya Serikali ikiamua kufanya hivyo kweli Wakandarasi tutapata miradi namna hiyo??

Mnataka tufe njaa

Hata hivyo si SumaJKT wala TBA wanaofanya kazi nzuri, mradi wa miezi 8 unafanywa kwa miaka 3 au zaidi mpaka inafikia kipindi Serikali yenyewe inaamua kuwavunjia mikataba.

Nje ya Mada
Hivi makato ya walimu kuchangia CWT yanawasaidia vipi Walimu???
 
Wanapewa t-shirt kwisha wanabaki wakichekelea kumbe wanapigwa.
 
Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom