Tafakuri Baada ya Mazishi ya Hayati Magufuli

Libya

JF-Expert Member
Nov 11, 2016
783
1,918
Kutoka Chato hadi Mwanza Distance yake ni 78.65 mi (126.58 km). Driving route: 148.32 mi (238.70 km). Mwendo wa saa ambazo sio zaidi ya 5 unakuwa umefika Mwanza ukitokea Chato. Ukipita Bwanga, Katoro, Geita, Kasamwa na Usagara unaingia Mwanza kuitafuta ilipo Airport.

Mishale ya saa 2 usiku baada ya "shujaa wa Afrika wa karne" kuzikwa nyumbani kwake, Chato, Geita, watu tuliokuwepo katika Jiji la Mwanza, tulishuhudia misafara mirefu ya V8 ambazo zilikua zinaelekea airport kwa kasi sana... Zilibeba mawaziri, manaibu, Viongozi wengine wa serikali, mahakama nk.

Msibani wapo wengi wanakuja kwa sababu waonekane kuwa wapo. Lakini fikra zao zipo mbali sio hapo msibani, wapo wanaokuja msibani kwa sababu ya fursa au kulipa fadhila. Ile misururu ya magari baada ya kuzikwa SHUJAA ikirejea Mwanza usiku ule, ilinithibitishia hilo.

Nimeelewa sasa, kwamba ukifariki hauna fungu lako tena hapa duniani na kuna mpaka kati yako na watu wa duniani, usitegemee sana kama wale wasio wa kwako kwa ungano la damu basi watabakia hapo. Hilo nimeamini jana. Watu wengine walipochoma mafuta kurejea Mwanza na maeneo mengine, wanafamilia walibaki.

Maisha yanatafakarisha sana... Jinsi unavyoona maisha yakiwa yanaendelea wakati umewapoteza rafiki ama ndugu zako wapendwa kabisa... Ndivyo maisha yatakavyoendelea kwa wengine pindi utakapolala mauti... Watalewa ukiwa hujazikwa, watakula na kushiba, baada ya kuzikwa, kaburi lako litapewa mgongo na wanaweza wasirejee tena hapo.

Tujipende tukiwa hai... Tuzipende familia zetu pia... Tuwapende watu wetu sana. Tuutumie muda wetu kuishi vizuri na watu. Hesabu baada ya kufa ni kidogo sana kwa wanadamu. Mtu aliyezaliwa na mwanamke, siku zake za kuishi ni chache sana na zenye taabu nyingi.

Ungeweza kudhani mawaziri aliowateua JPM, watu aliowaamini, aliofanya nao kazi kwa karibu na kuwapa nyadhifa kubwa.. Wengine aliolazimisha ushindi wao kwenye uchaguzi mkuu, wangetumia japo siku moja tu kuendelea kukaa Chato kwa ajili ya kutafakari upendeleo aliowapa wakati akiwa hai?

Ajabu ni kwamba wameshindwa kutumia angalau siku moja tu (anyways, saa moja tu) tu kuendelea kuwepo eneo alilozikwa.. Wote wamemuacha na wameondoka kuendelea na mambo yao, na wengi wao wanawahi mambo yao binafsi... Au ndio ile watu wanaita "hakuna kupoteza muda tena, yake yamekwisha?". Hili limenitafakarisha sana.

JPM amebakia na familia yake na ndugu zake pekee wakiomboleza kifo chake... Mkewe atalia sana hapo kaburini, wanae, dada na kaka zake wataomboleza hapo kwa siku 40. Mama yake pia akipata nafuu atalia sana msiba wa mwanae, ataumia wakati wote. Lakini wale mawaziri, wabunge, makatibu wakuu, wataendelea na mitkasi yao. LIFE!

Ukipata nafasi ya kuwasaidia ndugu zako fanya hivyo.. Angalau hawa ni watu pekee wanaoweza kuwa pembeni yako hadi unaiacha dunia... Usiache kuwasaidia ndugu zako, usiache kuwakumbuka ndugu zako, mama yako atalia na wewe tangu unazaliwa, unaishi hadi siku unafariki. Akiwa hai, atakuzika na anaweza kulia kila siku akikukumbuka mwanae.
 
NAMPA HONGERA JPM KAMA ALIJENGA NYUMBA YA MAANA KULINGANA NA WAKATI HUU.

Watanzania sio wa kuwafia kwa kuwa wamegawanyika ili kuwaunga utauwawa au kulaumiwa kwa kuwa ndan ya kujigawa kwao kuna wanaonufaika..

Ili uwakwamue yakubali makoozi yote wakutemeayo.
 
Sasa wote wangekaa Chato??Kwa siku ngapi?
Ndo mjiridhishe Wana uchungu?..

Aliekwambia JPM vyeo alivyowapa watu ni vyake binafsi nani?Ilikuwa lazima watu wamshukuru yeye binafsi?Au wajilize msibani siku kadhaa?

Rais ni cheo Tu cha umma..
Kila aliemteua aliteuliwa Kwa sababu nafasi
Ya kiserikali inahitaji mtu afanye hiyo kazi..

Wala sifa za kuteuliwa hazihusiani na
Kumpenda Rais na familia yake...
Kama Rais keshazikwa wakae Chato wanasubiri nini?
 
Tukaulizie Accra labda kuna jambo huyo shujaa uchwara wa Afrika amefanya

Hata jina la mtaa hana huko nje ya africa tofauti na mwl.Nyerere anaekumbukwa Dunia nzima
 
We jamaa ndio mara yako ya kwanza kwenda msibani nini? Watu ambao sio ndugu wa marehemu wabaki msibani kufanya nini?? Acha mawazo ya kitoto.
 
Back
Top Bottom