TAFAKULI YAKINIFU

900 itapendeza

Senior Member
Nov 17, 2017
114
103
Kwanza kabisa naomba nianze na salamu kuwajulia hali nyote ,pili naomba nichukue nafasi hii adhimu kutoa pole zangu kwa Wanzania wote kwa misiba iliyotusibu hivi karibuni
Twende katika maada ndugu wanajamvi nipende kuwajuza yakuwa nimekuwa mfuatiliaji wa mijadala mbalimbali iletwayo humu jf toka mwaka 2013 mpaka dakika hii.Miaka ya 2013+ kulianza kuibuka wimbi kubwa katika siasa zetu za ndani ,wimbi hilo lilikuwa likipambwa na nomino mashughuri sana ndani na nje ya Tanzania .Kulianzishwa mijadala kemkem ikiwajadili miongoni mwa wanasiasa nguli nchini.Katika mijadala ile ilipelekea kuibuka kwa kambi mbalimbali ndani ya vyama vya kisiasa.
Mwanzononi kabisa mwa miaka ya 2015 kulianza kutokea cheche za kuwania nafasi adhimu ya kuwa muwakilishi wa binadamu milion 45+ kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012.Cheche zile zilipelekea kutokea wa vitimbwi na vimbwanga visivyo na ukomo katika kipindi kile cha mpito na chenye umuhimu mkubwa wa kuibadili historia ya kaya yetu kwa kumtafuta mtu anaefaa kuwa kiongozi wetu.
Mchakato ulifanyika na yaliotokea yalitokea na maisha yaliendelea.Leo tukiwa tunaianza robo ya pili katika mwaka, masikio na macho ya watanzania wengi yakielekezwa katika matukio makuu mawili ambayo ni mosi msiba wa kaka yetu na mpambanaji mwenzetu ,pili hatima ya hukumu ya rufaa ya mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo pamoja na mbunge wa jimbo la tarime( v) ambapo masaa machache baadae kuliibuka kwa shangwe na furaha kubwa baada ya taarifa kutoka yakuwa kesi hiyo imetolewa maamuzi yenye haki na weredi kama ilivyotarajiwa.Masaa machache baadae pia kuliibuka taarifa iliyo ibua sintofahamu na ngumnzo kubwa pale tulipo alifiwa kuwa shujaa wa chama fulani alie jiunga na kambi ya wavaa ngwanda amerejea nyumbani kwao.
TAFAKULI INAKUJA
Je kinachoendelea ni msukumo wa nini ndani yake?
Mkululu wa matukio ambayo yamekuwa yakisawili mfumo wa panya ya kung'ata na kupuliza nini hasa lengo lake?
Je tutarajie nini katika siasa za Tanzania?
Je TL anajiandaaje kisaikorojia ili kuendana na siasa za dhama hizi
Je mh balozi Silaa atarejea nae nyumbani kwake kimkakati zaidi?
Kama wafuatiliaji wa siasa nchini tumejifunza nini?
Maswali haya yanaibua tafakuli yakinifu ambayo majibu yake yaweza kuwa nuru kwa mustakabali wa siasa za kizazi chaleo na kijacho
Ahsante na wasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom