Tafakari: Zanzibar kwanza vyama baadae

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
16,418
9,206
Kuwa na kichwa ni muhimu sana lakini sio lazima uwe na akili nzuri inawezekana ikawa hamna kabisa ndio maana wengi yetu kabla hatujanunua nazi utatuona huwa tuna itikisa tikisa hivi kuangalia kama wenyewe wamo au la,tuachane na hizi nazi na turudi kwenye vichwa vyetu haya yanayotokea.

Tumbatu hivi sasa mimi binafsi hapa nimekitaja sana hichi kisiwa wenzangu mnakumbuka nilifanya hivyo kwa kujua kuwa tukimaliza uhasama na Pemba tutahamia hapa Tumbatu, kwa sababu sio siri tena kuwa wananchi wengi wa kisiwa hiki na wao wameamua kutumia uhuru wao kutuacha mkono sisi CCM na kuhamia CUF hiyo ni haki na uamuzi wao unaopaswa kulindwa na kuheshimiwa sio kuchomewa moto nyumba zao na sehemu zao za biashara

Hawa ni ndugu zetu,wazee wetu,damu yetu na wazanzibari wenzetu.tukimaliza kuwadhuru wananchi wa kisiwa hiki tunaelekea wapi?nilisema kuwa hapa hatosalimika mtu hii sio “siasa” huu ni uhuni mtupu sikueleweka.

Wengi hatukichukii chama cha mapinduzi ndio maana bado tumebakia kuwa wanachama wake lakini tunawachukia viongozi wa chama chetu wanaodhalilisha watu kwa kutumia jina la chama chetu kiasi cha kuwafanya wananchi wanao athirika hivi sasa watuchukie sote tulio wanachama na wapenzi wa CCM kwa kuwa hawana muda tena wa kuchambua nani mtu au nani jibwa,chama ni itikadi na watu sio jengo au mtu mmoja au wawili hata wawe viongozi wa juu wao wataondoka wengine watakuja sasa chama gani kitaongozwa kwa itikadi ya CHUKI au UBAGUZI halafu kikapendwa na watu?

Unahitaji kichwa tu kupata jawabu sahihi sio lazima kiwe na kitu ndani lakini kwa bahati mbaya kwa sasa hata hivyo vichwa vitupu imekuwa adimu. Kuna sahib yangu mmoja mkubwa ambae namheshimu na nampenda kwa dhati kama kaka yangu miaka ya nyuma wakati Rais Sheni anaingia madarakani tu.

Kuwa rais wa zanzibar katika mazungumzo yetu ya siasa ya kawaida huwa tukikutana wakati wa jioni kwa kula au kuramba “ice cream”katika mgahawa wetu aliniuliza swali kama “namjua bwana sheni?” nikamjibu la hasha simjui ila namfahamu tu na nikamwambia nafikiri unaijua tofauti akanijibu ndio,akaniuliza

Tena unaonaje uongozi wake utakavyo kuwa kwa kipindi kimoja au viwili atakavyo kuwa rais? kwa kuwa huwa tuna desturi ya kuichambua siasa vilivyo siku zote na yeye ni msomi mzuri sana anae hodhi vyeti vyote vinavyotolewa nikamwambia kwa maoni yangu kiongozi huyu atakuwa na matatizo ambayo hayajawahi kufanya na wale marais wote walio mtangulia,niilitumia lugha ya kimombo kwa ufasihi sahihi na nilitamka hivi” he will be the worse president we have ever seen” kwa nini nilitamka haya au kwa ushahidi gani?

Niliyanena haya kwa kuwa simuelewi huyu muungwana lakini namfahmu tu kwa upeo wangu alio nipa Mola katika masuala ya kisiasa niliweza kuwa na ushahidi sio wa kisayansi lakini wa kinadharia tu kuwa kama unajua kuitumia saikolojia ya lugha maumbile yaani “body language” kila kitu kiko wazi au usoni kuweza.

Kumchambua mtu yoyote hasa viongozi wanao kuja mbele ya umma kwa kutathminiwa sio kwa kauli zao peke yake bali pia vitendo na yale wasio weza kuyazuwia kuficha dhamira halisi ndani ya mioyo yao basi huna sababu ya kuamini kinachotoka midomoni mwao ikiwa hakilingani na viungo vyao,ndio maana kwa kutumia sanaa hii nilisema kwa kujiamini kabisa kuwa huyu hatufai.

Ikiwa tunataka kuwa na uhuru na nchi yetu,uungwana na utu wake hivyo sina mashaka navyo lakini sisi kama wazanzibari hatu vihitaji hivyo katika kujinasua na ukoloni wa Tanganyika.

Nilishituka pale nilipomsikia maalim Seif akilalamika, aliposema baada ya uchaguzi wa mwanzo kuwa Rais Sheni sio au hakuonyesha uungwana kwa kuwa alitegemea mengi mema kutoka kwake labda baada na wakati wa mazungumzo yao alidhani atakuwa muungwana na kuheshimu walichoongea/ kukubaliana/maamuzi ya wengi, mimi nisingeliingia katika mazungumzo kwa kutegemea UUNGWANA wake kwa sababu huo kama nilivyosema hata kama unafurika katika kifua chake sisi wazanzibari tunahitaji maamuzi sahihi,umoja na kuwatendea haki watu wote ni lazima aelewe hivyo kukubali au kukataa hilo.

Juu yake hatutaki “feva-favour” ndio maana sihusishi uungwana na kudai HAKI kwa sababu neno uungwana linaweza kutumika sivyo katika harakati za kisiasa, ndio maana tuna baguana ovyo kwa sababu wengine wanaona kuwa wenzao hawana haki ila wanafanyiwa hisani tu kuwemo serekalini, au kuishi UNGUJA haya ndio matatizo ya waungwana.

Historia za nchi nyingi sio lazima zinukie asumini,vikuba au marashi ya karafuu kuna nyingine hunuka uozo wa ajabu lakini haina maana kila siku turudi kwenye harufu mbovu na kuyatumia kama manukato ili tuweze kuwakandamiza raia wetu kwa kisingizio kuwa nyinyi na chama chenu ndio wale wale tulio wapindua miaka ile sasa mnatunyima usingizi,hizbu na uchotara ni sehemu ya historia hii.

Afrika au duniani kote sio ajabu, siri au aibu kwa chama kilicho leta uhuru kukosa ushabiki baada ya muda na kuondolewa madarakani na watu au kizazi kile kile kilicho shiriki kumuondoa mkoloni mfano sitaki kwenda mbali nita azima ya karibu Kenya au Zambia majirani zetu, vyama vinavyo tawala hivi sasa sio vile vilivyopindua au kumuondoa mkoloni kwa karatasi na hawaja itumia historia yao iwe ya asumini au ya kuzibia pua kuwanyima haki.

Wananchi wao kwa kupitia masanduku ya kura kuchagua wapi wanataka kwenda na nani au chama kipi kiwaongoze, sisi tuna itumia historia yetu vibaya kwa manufaa ya wachache, maendeleo ndio tatizo kwa watu wetu sio watawala ikiwa hawa jaridhika nayo ni haki yao hata uwatoboe masikio kwa kuwanadia hayo mapinduzi na maendeleo wao hawa toyaona wala kusikia kamwe hili nali fananishana yule bwana/bibi aliependa penzi la kifo hata umtie ila mpenzi wake kwa sumu ya mamba harusi atakualika lazima.

Usia wangu wa leo waungwana tuvitumie vichwa vyetu vizuri visiwa hivi vitatutoka ikiwa tuaendelea kuchomeana nyumba badala ya kusaidiana kufyatua matofali na kuanza ujenzi mpya, mzuri na wa kudumu. makosa ya uchapaji naomba mnihurumie.

Zanzibar kwanza/vyama baadae.
Mzeekondo.
 
Back
Top Bottom