Tafakari yangu kuhusu wajibu wa kiongozi na wajibu wa raia. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafakari yangu kuhusu wajibu wa kiongozi na wajibu wa raia.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shayu, Sep 24, 2011.

 1. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #1
  Sep 24, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  [h=2]Tafakari fupi kuhusu wajibu wa kiongozi na wajibu wa raia katika taifa.[/h]  Taifa ni umoja pasipo umoja hakuna taifa, kwa kiongozi yeyote yule makini na mwenye nia ya dhati kwa nchi yake, atafanya kila liwezekanalo ili watu wake wawe wamoja, kwakuwa pasipokuwa na umoja taifa lolote halitaweza kufikisha malengo yake. Ni muhimu kutambua kwamba serikali haiwezi kujenga nchi peke yake pasipo jitihada za dhati na kujitolea kwa raia wanaojenga nchi hiyo, kiongozi mzuri ni yule mwenye uwezo wa ku organize na kuhamasisha watu wake katika kuleta maendeleo ya taifa lao wenyewe.


  Ni muhimu kwa kiongozi yeyote yule kujenga uzalendo kwa watu wake, kuwafanya watu wake wajitambue kwanini wao ni Taifa na wana malengo gani kwa wao kuwa pamoja, lazima kuwe na kitu kinachowaunganisha pamoja, lazima kuwe na dira inayowaongoza kama watu walioamua kuishi pamoja. Lazima wajue wanapotaka kuelekea, hii ni kazi ya kiongozi kuonyesha njia, lazima awe mtu mwenye kuaminiwa, mwenye hekima na busara za kutosha kuongoza watu, lazima watu wamuamini kutokana na matendo yake na maneno yake.

  Naamini sio kazi ya serikali kuwalisha watu wake, Nchi itajengwa kwa jitihada za kila mmoja wetu katika kufanya kazi, katika kufikiri na katika ujenzi wa taifa letu. Serikali kazi yake ni kutengeneza mifumo , kusimamia na kuratibu, mifumo itakayosaidia uchumi wa mtu mmoja mmoja na uchumi wa taifa, kulinda haki za raia miongoni mwetu na kulinda taifa dhidi ya maadui wa nje, ila ni wajibu wa raia anayeunda nchi yeyote kutumikia taifa lake kwa dhati na kwa moyo wake wote, serikali ni kiongozi wa mfumo tu hana wajibu wa kulisha watu wake. Raia wanawajibu wa kufanya kazi kwa bidii kwa kulima na kujishughulisha katika kazi nyingine za uzalishaji mali.

  Ni muhimu kwa serikali kuhamasisha watu wake katika kufikiri na kutafuta maarifa kwa juhudi, kuhakikisha wananchi wake wanathamini kujitegemea kwa kuwa wachapa kazi na wabunifu. Pasipo kufanya kazi kamwe uchumi wetu hautokuwa. Lazima akili zetu zijihusishe katika masuala ya uzalishaji mali kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa maarifa na kujishughulisha katika kufikiri na kuvumbua, ni juhudi pekee na umoja wetu ndio utakao nyanyua taifa hili, tukitambua wajibu wa kuondoa umaskini ni wajibu wetu binafsi.
   
 2. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #2
  Sep 24, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  Baba anaye itiisha familia yake huenda akawa pia kiongozi bora wa taifa, kwani ukishindwa kuongoza familia amabyo ni ndogo je utaweza kuongoza taifa?
   
Loading...