Tafakari yangu kuhusu Umuhimu wa maadili katika ujenzi wa taifa.

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,654
Maadili ni kama kingo za mto na binadamu ni kama mto, unaweza kufikiri madhara ya mto unapofurika na kingo zake kuharibika, au uhai wa mto pasipo kingo, nidhahiri kabisa hautokuwa na mwelekeo maalum, kwahiyo maadili yanatuelekeza sehemu tunapotaka kwenda na yanatukinga dhidi ya uharibifu, Maadili ni muhimu sana katika ujenzi wa taifa lolote lile, bila nidhamu taifa lolote halitoweza kuendelea. Maendeleo ya kiuchumi na ustawi wa jamii hauwezi kufikiwa pasipo nidhamu na maadili, Hatuwezi kuwa na jamii yenye mpangilio mzuri pasipo maadili. Maadili ni kitu ambacho kiko ndani ya binadamu kinachomwelekeza kati ya sahihi na potofu.

Taifa lazima lijengwe kwenye misingi ya nidhamu na maadili ndipo maendeleo ya kiuchumi yatakapokuja.Maadili ni jambo la msingi sana katika taifa, lazima tujenge maadili ya familia zetu, lazima tujenge maadili ya vijana, taifa na maadili ya viongozi.

Tunaweza kusema maadili si muhimu kwa mfano, tuwafundishe watoto wetu elimu tu ya kawaida, wafike chuo kikuu wapate ujuzi wao, wakipenda starehe kupita kiasi tuwaache, wakiwa wazinzi na walevi tuwaache, Mimi sifikirii kijana mwenye tabia kama hizi , unaweza kumpa majukumu akawa mwaminifu na mchapa kazi hodari, nara nyingi vijana wa namna hii akili zao hazijatulia, lazima tuwe makini jinsi tunavyolea watoto wetu na vijana wetu, tuwalee katika misingi ya maadili na utaifa, wajue, wanamajukumu binafsi, kwa familia, jamii na kwa taifa.

Mkandarasi tuliyemfundisha kwa pesa yetu, ile awe mwenye manufaa kwa jamii yetu, Kama tukimpa kazi anachakachua,hatakuwa na faida kwetu, na elimu yake itakuwa haina maana . Tulitegemea kwamba atawajibika kwetu katika kujenga jamii, yeye akiwa kama mmoja wetu anayeunda taifa hili, ili afanye taifa hili liwe bora na la kupendeza.

Katika historia ya mwanadamu amefikia mafanikio makubwa pale tu walipamoja kama jamii. Sisi sote ni wamoja na dhumuni letu liwe ni kujenga taifa hili kwa faida ya vizazi vyetu vijavyo, tunajukumu la kulilinda na kulijenga taifa hili kwa jitihada zetu zote kwa faida ya vizazi vijavyo.

Kuanguka na kunyanyuka kwa tawala yeyote ile kunategemea sana misingi ya kimaadili na kinidhamu ya taifa hilo, pasipo nidhamu taifa lolote halitoweza kupiga hatua ya kimaendeleo, Taifa lisilokuwa na nidhamu ni kama mbegu zilizomwagwa shambani bila mpangilio, haliwezi kuzalisha chochote, mimea itaota na kufa, utakuwa na watu upande mmoja wanajenga taifa na upande mwingine wanaiba kile tunachokijenga, utakuwa na viongozi wasiowajibika na wafanyakazi wanaofika kazini saa tatu, utakuwa na wabunge wanaochaguliwa vijijini na kuja mjini kustarehe na badala ya kuishi na wananchi na kujua matatizo yao na kuyatatua kwa pamoja, tutakuwa na taifa lisilokuwa na mpangilio wala heshima, hatutaweza kujenga taifa la watu wanaojitolea kwa dhati kwaajili ya ujenzi wa taifa lao wenyewe. Tutazaa watu wabinafsi na mantiki yote ya sisi kuishi kama taifa itafutiki, kutokana na huu ufisadi na ubinafsi utatupelekea tupigane vita na taifa tulilolijenga litafutika kabisa, ni lazima kila mmoja wetu katika taifa hili ajue ana jukumu la dhati kabisa katika ujenzi wa taifa hili, kwasababu maj aliwa ya taifa hili ni majaliwa ya kila mmoja wetu.

Elimu na sheria vina nafasi kubwa sana katika kujenga maadili ya jamii, katika mwelekeo tunaoutaka na katika kubadilisha tabia za watu, ili kujenga raia wema na kuunda taswira ya taifa tunalolihitaji, kulinda utaratibu na muundo mzima wa taifa, pasipo sheria hatuwezi kuwa na kitu kinachoitwa taifa, ni kama yai na gamba lake, Taifa lisilotii utawala wa sheria kunauwezekano mkubwa taifa hilo likasambaratika, sheria ndizo zinazolinda taifa, Ni jukumu la kila raia kuzitii, KWani tumejiwekea sisi wenyewe kama muungozo wetu, zinalinda haki za kila mmoja wetu na mahusiano yetu kama binadamu. Tumeunda mahakama, bunge, polisi nk Lengo letu ni kujenga jamii bora yenye nidhamu na utaratibu, amani yetu itakuwepo ikiwa vyombo hivi vitafanya kazi yake kikamilifu na kwa uaminifu na kwa mashirikiano bila kuangalia vyama bali vikisukumwa na uzalendo na hamu ya kuona taifa hili likiendelea, lazima tutamue sisi ni watu wamoja na lazima tuwe na malengo kama taifa.
 
Bila neno HAKI na USAWA katika jamii, suala la neno MAADILI bado ni msamiati unaojulikana tu katika sayari nyinginezo tu huko angani.
 
Mkuu uliyoandika ni kweli kabisa na ninauhakika viongozi wetu wa ccm wanaisoma hii habari japo hawatabanilika kwani 'sikio la kufa halisikii dawa' hii kwao ni kama kumpigia nguruwe gitaa kwani kamwe hatocheza
 
Unajua tatozo tulilonalo katiak nchi yetu ni la maadili, mtu mwenye maadili lazima atazinagatia haiki za wengine.
Bila neno HAKI na USAWA katika jamii, suala la neno MAADILI bado ni msamiati unaojulikana tu katika sayari nyinginezo tu huko angani.
 
Back
Top Bottom