Tafakari yangu juu ya vyombo vya habari kujenga taifa lililo imara.

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Vyombo vya habari vina umuhimu mkubwa katika ujenzi wa taifa imara na kujenga mawazo na mitazamo ya watu juu ya nchi yao wenyewe, NI chombo muhimu katika ujenzi wa taifa, ni chombo kinachotoa habari na kuelimisha umma, hivyo taifa inabidi lilipe kipaumbele eneo la habari, kwa kutoa elimu imara na kufundisha watu wetu katika uzalendo, tukiwatumia vizuri waandishi wa habari katika ujenzi wa taifa hili tutafika mbali, tutajenga uzalendo kwa watu wetu pamoja na uwajibikaji, ni chombo pekee kinachoweza kusambaza uzalendo kwa taifa letu a kuleta umoja wa nchi, ni watu ambao wanatakiwa wafundishwe kuijtolea kwaajili ya ujenzi wa taifa hili, lazima wajue jukumu lao katika ujenzi wa taifa na kuleta watu wetu pamoja, lakini pia wajue madhara ya kalamu zao kuleta athari kwa taifa.

Lazima viwe vyombo vya kizalendo, vitakavyohamasisha juhudi katika kazi, kutoa elimu na kuleta watu pamoja visiwe vyombo vya muziki tuu na kuacha mambo mengine ya msingi yanayohusu taifa letu hasa umoja wetu, ninaamini waandishi wa habari wakijitolea kwa dhati katika ujenzi wa taifa hili tunaweza kufika mbali na kuleta watu wetu pamoja katika masuala mbalimbali yanayohusu taifa letu, mchango wa vyombo vya habari na waandishi wa nabari kwa taifa ni mkubwa mno na wakuthaminiwa. Tukiuunda vyombo vya habari imara vyenye uzalendo na msimamo tutakuwa tumepiga hatua moja mbele kubwa ya maendeleo, wanahusika moja kwa moja katika ujenzi wa taifa letu na hasa makuzi ya vijana wetu, hivyo maadili kwa waandishi wa habari ni muhimu sana katika ujenzi wa taifa, wao wanaweza kufanya sauti zetu za pamoja zikafika mbali zaidi katika ujenzi wa taifa letu.

tuongee kwa sauti moja juu ya matatizo yanayotukabali kama taifa, tukusanye nguvu zetu kwa pamoja tukemee uovu ili kujenga taifa imara la watu wenye mashirikiano, upendo na umoja, ili kujenga baadae ya watoto wetu na misingi imara ya taifa letu. Amen.
 
Back
Top Bottom