Tafakari yangu juu ya umuhimu wa katiba katika transformation ya nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafakari yangu juu ya umuhimu wa katiba katika transformation ya nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shayu, Oct 31, 2011.

 1. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #1
  Oct 31, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  Katiba au constitution kwa lugha ya kiingereza ni Muongozo ambao taifa lolote limejiwekea jinsi ya kuendesha shughuli za kila siku za taifa lao.

  Katiba yeyote lazima iwe na malengo ya kuibadilisha jamii katika mwelekeo fulani ambao tunadhani utakuwa wenye manufaa na faida kwa jamii nzima. Katiba ndio kiini cha taifa lolote, Ni kama yai na Gamba lake.

  Order katika taifa inategemea sana jinsi taifa hilo linavyofuata na kutii katiba waliyojiwekea wenyewe. Katiba ndio inayounganisha jamii iliyoamua kuishi kama taifa kutoka katika makabila mbalimbali, dini mbalimbali na familia mbalimbali na kuwa kitu kimoja. Kuna umuhimu mtu akiapa lazima aitekeleze katiba hiyo ama sivyo taifa halitokuwa na mabadiliko yeyote, Katiba ni kama ‘’mould’’ au ‘’pattern’’ ambayo watu wa taifa wanataka kupitia , kuelekea katika actualization. Kuna umuhimu mkubwa sana wa kutii katiba ili kujenga taifa tunalolihitaji.

  Kwahiyo ubora wa taifa lolote unategemea sana akili za viongozi na utekelezaji wa katiba na sheria taifa lilizojiwekea. Hakuna transformation yeyote itakayo fanyika ya kimaendeleo au ya kijamii bila order na discipline katika jamii. Lazima I define our governing structures and how they operate and interact with each other. There must be a co ordination between our governing structures, in order for a government to be efficient and our society to be transformed. The whole structure must be acting as one just like car and other components inside the car but the principal governing structure must be constitution, The driver.

  Constitution must be executed faithfully, without doing that we can change nothing. it must be our driving force, without that we can’t reform our society. So the efficiency of any government depend mainly on the efficiency of the governing structures and the efficiency of it’s leaders, Commander in chief is the leader of the whole chain, so he is responsible for any failure within the system.


  Taifa ni imara linapokuwa na katiba imara na viongozi imara, wenye maono imara juu ya taifa lao. Taifa lazima lisimamie misingi ya haki na ianishwe katika katiba kwani ni haki pekee huleta watu pamoja, ufsadi utenganisha watu na kuharibu misingi ya utaifa. Familia zetu haswa za watu walioenda shule lazima zijengwe katika misingi ya utaifa na uzalendo. Tukiwafundisha watoto wetu juu ya taifa letu na wajibu wao kwa taifa, Lakini pia tukiwa na jukumu kila mmoja wetu wa kuwaelimisha wale waliobaki ambao hawajapata elimu juu ya umuhimu wa taifa na utaifa.


  Kila mmoja wetu ana wajibu kwa taifa hili, wajibu wa dhati kabisa kwakuwa tumeungana pamoja kuwa taifa ili kulinda haki za kila mmoja wetu na kujilinda na maadui wa nje, tukijua kwamba umoja wetu ndio nguvu yetu, tutengeneze taasisi zetu katika maadili na tujifunze moyo wa kujitolea na wa kizalendo kwa taifa letu.  Katiba yetu lazima ilenge katika kutuleta pamoja, ili tuwe na nguvu ya pamoja ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazotukabili. Taifa imara hujengwa katika umoja na mshikamano wa watu wake na sisi watu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, tulioamua kuwa taifa, tutambue hilo, uwepo wa taifa hili unategemea sana maamuzi yetu tunayoyafanya na si jambo la mzaha. Nchi haijiendeshi yenyewe. Inaendeshwa kwa busara na maono ya watu, bila hivyo tutasambaratika tusiwe na nchi. Amani yetu iko mikononi mwetu wenyewe, Busara ituongoze katika ujenzi wa taifa hili na isiwe uchu na tamaa zitakazo tugawa na kuharibu umoja wetu kama Taifa.


  Ninachoona sasa katika taifa letu ni mgawanyiko, wa dhahiri kabisa unaotukana na ubinafsi, ufisadi, utafutaji umaarufu wa kijinga, uwekaji pesa mbele kuliko maslahi ya taifa hasa katika yale mambo ya msingi yanayo tuleta pamoja, tumekuwa wabomoaji wa taifa na sio wajenzi, Vyombo vya habari ambavyo vingetumika kama tool ya kujenga utaifa vimekuwa vyombo vya kisiasa vinavotumiwa kufanya propaganda kwa maslahi ya magenge, Kumekuwa na uhuni mkubwa unaendelea katika taifa letu, Waliopewa dhamana wanaacha kufuatilia mambo ya msingi na kufuata starehe na anasa.

  Katika mazingira haya hatutaweza kutengeneza katiba ya maana itakayo transform jamii yetu. Kila mtu au kikundi kitaingiza ajenda zake binafsi na mchakato mzima utakuwa fujo na chanzo cha mgawanyiko ndani ya Taifa. Tulichokosa hapa ni uongozi na discipline katika jamii na jinsi tunapoelekea taifa letu litakosa viongozi wa kuaminika kabisa kwasababu vijana hawa tayarishwi, wanaachwa kwenye anasa za starehe bila kujengwa kimaadili ili wawe raia wanao wajibika na wazalendo. Kumekuwa na mgawanyiko wa makundi mawili waliopo madarakani wanaofaidi ufisadi na wanaona wivu kwa wanaofaidi ufisadi. tumekuwa kama mbwa wanaogombania nyama. Hakuna mtu anaye hubiri umoja, hakuna anaye hubiri uzalendo wala haki, tutasimamaje kama taifa?


   
 2. Mkasika

  Mkasika JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  The history of constitution making in peacetime demostrates that, unless concensus is built on the draft through realistic pre-negotiations by the protagonists in full realisation that whatever the results, the country has to move on, the process becomes flawed and counter productive. Observers of Tanzanians political scene fear that , unless the issue of the referendum is handled cautiously , the country might cease to exist as we know today. The fact that democratic traction has failed to hold and corruption in all its manifestation continue to drain national resouces, Tanzanians should brace for hard times.
   
 3. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #3
  Oct 31, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  I don know if i grasp your idea propely but what i observe today in our country ni kugawanyika kwa taifa letu na kukukosa mission ya pamoja kama taifa, na kwa mazingira hayo hatutaweza kutengeneza katiba ya maana itakayo transform taifa letu, kila mtu ataingiza agenda zake za ubinafsi na mchakato mzima utakuwa fujo! Tulichokosa hapa ni uongozi, kiongozi ambaye ataaminiwa kuongoza huu mchakato kwa sasa simuoni, na wasi wasi katiba hii inaweza kuwa mwanzo wa mgawanyiko mkubwa.
   
 4. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #4
  Nov 12, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  mmh tuna kazi sana na taifa letu
   
Loading...