Tafakari ya kiutendaji: Yesu Kristu na "baba" yake Yohane Mbatizaji: Magufuli na Wapwake zake.

Ujinga huo,taifa ni letu sote kuwekeza kwa kusema MTU anayemwamini ni aina ya Uafrika wa karne ya 12
Mkwawa aliyemwamini ndiye aliyemsaliti.
Tutengeneze Taasisi Imara ili kila mtz ajiamini mwenyewe na sio aaminiwe na Magu au yoyote yule

Taifa lilipofika lilifikishwa na nani mbona Magu hakuwa miongoni mwa waliokuw wanalalamikia mikataba na utendaji wa hovyo ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa kama ni letu sote hata hao waliopewa nafasi nao nilao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Loh! Kukufuru? Kumbe wale wachungaji "wanaojibatiza" majina mazuri na ya kusisimua kama vile "Mtume na Nabii", " Bwana wa ufufuo na Uzima", nk nao wanamkufuru Mungu na Yesu maana hata Yesu pekee anastahili kujiita hivyo.Someni maandiko Matakatifu kwa utulivu.Sisi tunajiita Wakiristu kwa sababu tunamufuasa Kristu.Tunaalikwa kujifunza kwa Kristu.Kwa hiyo kueleza kuwa hata Yesu aliishi na kufanya kazi na ndugu ni Kufuru? Kumbe ndiyo maana Yesu hakukosea kuacha kazi ya kufundisha Imani yake mikononi mwa Petro na Wenzie.Wengine mumedandia Maandiko Matakatifu kwa mbele na hivi mumevunjika meno na ndimi zenu.
ukabila, chuki na kiburi cha madaraka kinawasumbua, watu wanalipa kodi mara mbili mbili, maendeleo kwao hawayaoni, haki zao za msingi kama malipo ya uhamisho nyongeza za mishahara, hawapati, mazingira magumu ya kazi, kunyima haki za kikatiba za kufanya mambo mbalimbali huku jamii au kundi lingine ndani ya nchi hii linaruhusiwa, kutoa madaraka na kazi mbali mbali zinazotokana na jasho la wote kindugu na kikanda. HALAFU UOVU HUU UNAFANANISHWA NA MUNGU! NARUDIA TENA HII NI KUFURU! SHAME UPON YOU
 
Wakati CHADEMA wamejazana kwenye nafasi za uongozi ndugu, marafiki hawa wapenzi, Lissu hajalikemea hilo. Labda amefanya hivyo kwa kuchokonoa upande usiomhusu asije akashushiwa rungu!

Hivi ni sehemu gani, katika nchi hii, na duniani kote, ambapo ndugu husahauliana! Hata kwenye biblia, Nuhu aliwakusanya ndugu zake wakati wa gharika. Kwenye ofisi za umma, ndugu wamejazana. Kwenye shughuli za kutafuta maisha, ndugu tunabebana. Kwenye maeneo ya makazi, ndugu tunapeana maeneo.

TUACHE SIASA ZA UNAFIKI, UZANDIKI NA UCHOCHEZI. HAKUNA ATAKAYESALIMIKA.


Nafikiria baadhi ya wasomaji na wachangia hoja hawana kumbukumbu sahihi na baadhi ya matukio ikiwemo huu mfano wa tukio la Nuhu na Gharika.Kama ni watu wa kutaka kujifunza sasa watamakinika.
 
Huyu ni ndugu yake na Bashite.

Kwa asili sote ni ndugu.Matatizo mengi tunayoyapata wanadamu yanatokana na kutokuwa na mwono huo.Kule kuumbwa na kuwekwa katika Sayari moja ni ishara kuwa sisi ni wamoja.Tukiongozwa na tamaa hiyo ya kuwa wamoja tutaifanya dunia kuwa sehemu salama nzuri sana ya kuishi.
 
Kwa asili sote ni ndugu.Matatizo mengi tunayoyapata wanadamu yanatokana na kutokuwa na mwono huo.Kule kuumbwa na kuwekwa katika Sayari moja ni ishara kuwa sisi ni wamoja.Tukiongozwa na tamaa hiyo ya kuwa wamoja tutaifanya dunia kuwa sehemu salama nzuri sana ya kuishi.
Hata wanyama kama fisi, chui tunao sayari moja, kwa hiyo nao ni ndugu zetu?
 
ukabila, chuki na kiburi cha madaraka kinawasumbua, watu wanalipa kodi mara mbili mbili, maendeleo kwao hawayaoni, haki zao za msingi kama malipo ya uhamisho nyongeza za mishahara, hawapati, mazingira magumu ya kazi, kunyima haki za kikatiba za kufanya mambo mbalimbali huku jamii au kundi lingine ndani ya nchi hii linaruhusiwa, kutoa madaraka na kazi mbali mbali zinazotokana na jasho la wote kindugu na kikanda. HALAFU UOVU HUU UNAFANANISHWA NA MUNGU! NARUDIA TENA HII NI KUFURU! SHAME UPON YOU

Tumeacha hoja sasa naona tunatalamba kuelekea kusikojulikana! Kwa hiyo,haya malalamiko ndiyo mambo yanayofanywa na wapwa zake Magufuli? Tumesema hoja isiwe undugu wa Magufuli bali hao ndugu wanatumiaje ofisi waliyopewa na mjomba wao.Hoja iwe: hao wapwa wanao uwezo kwa nafasi hiyo? Malalamiko haya ya kutoongezwa mishahara na mengineyo,je hao wapwa za Magufuli ndio wamekataa kuongeza hiyo mishahara? Wao ndiyo wanasababisha mahangaiko unayoyaongelea?
 
Unahalarisha utawala wa kifalme kwa kutumia maandiko! Yesu Kristo hakuwa na maslahi binafsi wala hakuwa analipwa, hakuwa na familia, hata wasaidizi wake viyo hovyo. Acha kupotosha jamii, hapa kuna tatizo.

Sent using Jamii Forums mobile app



Kwa hakika ninaona kumbe Kanisa halijafanya kazi yake sawa sawa ya kuufundisha ukweli.Utakumbuka kazi hii alipewa Mtume Petro pamoja na Mitume wengine.Petro alikabidhiwa funguo za Ifalme wa Mbinguni.Ndio yale mamlaka ya kuruhusu jambo gani lifundishwe au lisifundishwe kwa waamini.

Katika mamlaka hayo ya kuruhusu au kukataza,ndiposa,Kanisa linafundisha kuwa Yesu Kristu alikuwa Mungu-mtu.Hili ni fundisho la imani.Yesu Kristu alikuwa na Umungu na Ubinadamu ndani mwake wakati mmoja.

Ukisoma Maandiko Matakatifu, Waenjili wote wanne na Nyaraka za Kitume,Umungu na Ubinadamu wa Yesu ni jambo ambalo limefunuliwa wazi.Na hata yeye mwenyewe Yesu, aliweka wazi kwa kujiita "Mwana wa Adamu".

Katika hilo,la Ubinadamu wa Yesu,ndipo tunakutana na yeye kuteua na kufanya kazi na ndugu wa damu au hata kuteua ndugu wengine wasio na udamu naye.

Hata katika Umungu,Yesu kama Mungu anapofanya kazi kwa ajili ya wanadamu,anafanya hivyo kwa kupitia mifumo yetu mitano ya fahamu.Ndio kisa,aliamua kushuka kati yetu katika ubinadamu.Mungu alijimwilisha kati yetu.

Kwa hiyo,tunapolinganisha utendaji wa Yesu kama Mungu-mtu na ule wa Magufuli,hatutendi dhambi yoyote.Kristu anatualika tujifunze kwake.
 
Ni vizuri tukaendelea kujadiliana kwa upole na kwa hoja kwa ajili ya kujenga afya ya Taifa letu.Hii ni kazi ya kila Mtanzania mwenye siha njema kichwani.Tundu Lisu,ametimua vumbi la mjadala,mintarafu "kumsonta kidole" Magufuli juu ya kuchkua ndugu zake wa damu ili wamsaidie kazi! Hili jambo ni la kujadiliwa kwa utulivu.Tujadili hoja tuache kumrukia mtoa hoja.Yawezekana kweli kawasilisha hoja nzuri kwa jaziba lakini tusiangalie tumeletewa chakula katika chombo gani.Madhali chakula ni kisafi hakina inzi nasi tuna njaa basi tule.Tujadili hoja kwa sababu suala kama hilo linatokea katika jamii yetu na inaonekana kuna watu linawakwaza.


Katika Maandiko Matakatifu,tunasimuliwa jinsi Yesu Kristu alivyozaliwa.Inasimuliwa Mara baada ya Bikra Maria kupashwa habari za yeye kubeba ujauzito kwa msaada wa Roho Mtakatifu na Malaika Gabriel,baada ya muda aliondoka kwenda kumsalimia Shangazi yake aitwaye Elizabethi ambaye alikuwa mjamzito wakati huo.Yeye (Elizabethi) alikuwa na ujauzito wa miezi sita.

Kadri ya masimulizi, Baadaye,Elizabethi alijifungua mwanaye ambaye ni maarufu kwa Wakiristu kwa jina la Yohane Mbatizaji.Huyu ndiye alifanya Maandalizi muhimu na ya kwanza kwanza kabisa kwa ajili ya Yesu kufanya kazi zake.Yesu alikuja kubatizwa na Yohane Mbatizaji katika Mto Yordani.

Kama ilivyo hapa Afrika,Katika zile familia extended, Bikra Maria alikuwa anamuita Yohane Mbatizaji Kaka.Ndio ni kaka yake maana ni mtoto wa Shangazi yake.Kwa hiyo Yohane walikuwa ni mtu na Dada yake.Je,kwa Mtiririko huo huo, Yesu alikuwa anamuita Yohane nani yake? Kwa Kabila langu la Kijita/ Kikerewe,Yohane Mbatizaji alikuwa Baba wa Yesu.Sijui Makabila mengine ikoje?

Kama nilivyodokeza hapo juu Yohane Mbatizaji ndiye aliyefanya maandalizi ya kazi za Yesu Kristu.Kwa hiyo "Baba" alimuandalia "mwanae" conducive invironment ya kuja kuwajibika na kutumika.Jambo kubwa sana bila shaka katika kazi ya Ukombozi wa Mwanadamu.Majalimu wa Theolojia wanayo mengi ya kusema juu ya suala hili.Kwa ufupi,Baba alimsaidia Mwana.

Wainjili Watatu,Katika Maandiko Matakatifu: Marko,Matayo na Luka wanatueleza hata baada ya Yesu kuanza kazi rasmi aliwachagua wanafunzi wa kumsaidia kazi.Ndio wale kumi na Wawili.Waenjili hao wote watatu wanabainisha kuwa wanafunzi wa kwanza kwanza kabisa kati ya 12, kuchaguliwa walikuwa ndugu.Wa kwanza ni Petro(Simon,Kefa) na kaka yake Andrea! Waliofuata ni watoto wa Zebedayo: Yakobo na Yohane.Dhana ya undugu inajitokeza tena katika utendaji wa Mungu hapa duniani na inaendelezwa na Yesu Mwenyewe!Ni kama Yesu alikazia jambo hilo.

Katika mabadiko mengi aliyoyafanyia kazi Yesu Kristu,hili la undugu, Maandiko Matakatifu hayatuelezi iwapo aliwahi kuliona kama ni "nongwa". Fundisho ni nini? Manga'muzi tunayoyapata ni haya: Undugu ni njia tu ya kueleza jinsi tunavyotokea duniani.Ni namna tu ya kutandika Biography ya jinsi tulivyotwaa uhai wetu wa kimwili toka kwa wazazi wetu wa mwanzo kabisa (Mume na Mke). Vinginevyo jambo hilo halina umaana wowote ule.Na ndiyo kisa katika mojawapo ya ufafanuzi wake Yesu,aliwahi kuweka wazi kuwa huko Mbinguni hakuna issues za undugu:"... hakuna kuoa wala kuolewa...".

Raisi Magufuli na wengineo ama kwa kufahamu au kutofahamu ukweli huu wamejikuta wanasaidiwa kazi na ndugu zao.Sio yeye peke yake.Kutoka Mwalimu Nyeerere hadi Kikwete wote wamefanya hivyo.Wabunge wana madreva ndugu.Wabunge na Mawaziri wengine wana wasaidizi ndugu.

Katika sekta binafsi,watu wana viwanda na ofisi zao.Baadhi wameajiri ndugu zao.Katika hili wamo Wahaya,Wanyakusa,Wachaga,Wasukuma,nk.Wamo Wahindi na Wachina mpaka Waarabu.

Ukiendelea na mkondo huo huo,katika dini wapo Mapadri na Wachungaji ndugu.Huko nyuma kabisa (wakati wa kipindi cha Giza katika Kanisa), Upapa ulikuwa unarithishwa hata kwa ndugu.

Sasa Lisu na CDM wametoa hoja hii ya "Usukuma,Usubi na au Uzirandekende" wa Magufuli katika Uongozi wa nchi! Je,Suala ni Undugu au suala ni ndugu anafanyia nini cheo au wadhifa aliopewa kwa sifa zake? Je,hoja ni uwezo alionao ndugu au hoja ni ipi hasa inapaswa kuwa?

Je,Kama Jamii tunaweza kujitenga mbali na suala la undugu hapa duniani? Mbinguni huko tayari angalau tumeshapewa "notisi" tujiandae Kisaikolojia kuwa kule hakuna cha mimi na watoto wangu,mjomba wala hubby au baby! Je,hapa duniani inawezekana?

Kwangu mimi hoja iwe: hao wasaidizi wa Raisi Magufuli wa Masuala ya fedha wana-misuse nafasi zao na wanapofanya hivyo wanajificha kwenye Ujomba? Hoja ikiwa hivyo,hapo kunakuwa na la kusema.Kama mambo hayako hivyo hoja hii inakosa cha maana.Inabaki kuwa mambo ya kurukiana tu.Je,hivi hao "wapwa" hapo Wizarani wanaogopwa na kila mtu? Je,hao wapwa Wizara ya Fedha nzima wanafanya maamuzi watu wawili tu ukiongezea na mjomba wao? Je,Wizara hiyo hata marafiki zangu wanaofanya kazi kwa siri nao wamekimbia baada ya timu "wapwa" kushika hatamu? Kama wapo si watupe madudu yao kama yapo.

Mimi sioni shida madhali hata Yesu alifanya kazi na ndugu zake,basi tukaze macho yetu kwa uwezo wa mtu na sio uzao wake.

Nawasilisha.
Imran (Baba yake Maryam) na Nabii Zakaria (Baba yake Yah'ya -Yohana Mbatizaji) ni mtu na kaka yake. Aliyetangulia kuzaliwa baina ya Yesu na Yohana, ni Yohana. Yohana na Maryam ni mtu na kakayake, Yohana ni mjombake Yesu.
Ref Qur'an; surat Imran, surat Maryam
 
Hata wanyama kama fisi, chui tunao sayari moja, kwa hiyo nao ni ndugu zetu?


Kwa taarifa yako,ni kwamba viumbe vingine vyote vitashirikishwa uzima wa Milele na mwanadamu.Katika umilele, miili yetu itaungana na Roho zetu ambazo zenyewe zinatangulia Mbinguni,Purgatory au Motoni.Miili yetu na Viumbe vingine vyote vinasaidia Roho zetu katika maisha yetu ya kila siku.Kwa hiyo ukiona Fisi,Kenge,Mbwa au Jongoo usione ni viumbe visivyo na maana.Mungu hawezi kuumba kitu pasipo kuona mantiki kwanza.
 
Hata wanyama kama fisi, chui tunao sayari moja, kwa hiyo nao ni ndugu zetu?


Kwa taarifa yako,ni kwamba viumbe vingine vyote vitashirikishwa uzima wa Milele na mwanadamu.Katika umilele, miili yetu itaungana na Roho zetu ambazo zenyewe zinatangulia Mbinguni,Purgatory au Motoni.Miili yetu na Viumbe vingine vyote vinasaidia Roho zetu katika maisha yetu ya kila siku.Kwa hiyo ukiona Fisi,Kenge,Mbwa au Jongoo usione ni viumbe visivyo na maana.Mungu hawezi kuumba kitu pasipo kuona mantiki kwanza.
 
Imran (Baba yake Maryam) na Nabii Zakaria (Baba yake Yah'ya -Yohana Mbatizaji) ni mtu na kaka yake. Aliyetangulia kuzaliwa baina ya Yesu na Yohana, ni Yohana. Yohana na Maryam ni mtu na kakayake, Yohana ni mjombake Yesu.
Ref Qur'an; surat Imran, surat Maryam

Bado hoja inayojitokeza ni kwamba wote ni ndugu: Yesu na Yohana ni ndugu.
 
Imran (Baba yake Maryam) na Nabii Zakaria (Baba yake Yah'ya -Yohana Mbatizaji) ni mtu na kaka yake. Aliyetangulia kuzaliwa baina ya Yesu na Yohana, ni Yohana. Yohana na Maryam ni mtu na kakayake, Yohana ni mjombake Yesu.
Ref Qur'an; surat Imran, surat Maryam

Hongera kwa kufuatilia hoja hii.
 
Mkuu hata pale Chadema Ndesa alikuwa bungeni na mwanae na mkwewe, Lissu na dada yake, Zitto na dada yake, Dr Slaa na mkewe, Mbowe na mzazi mwenzie na ilibakia kidogo mama Kafulila awe na mumewe. So hakuna tatizo hapo Tundu anazingua!
Sita na mkewe, Msekwa na mkewe, Ridhiwan na mamake
Kwa kuwa hatuko kwenye kisiwa sio vibaya tukajifunza pia wenzetu huko wanasemaje.

***********************
U.S. Code § 3110 - Employment of relatives; restrictions

(a) For the purpose of this section—

(1) “agency” means—

(A) an Executive agency;
(B) an office, agency, or other establishment in the legislative branch;
(C) an office, agency, or other establishment in the judicial branch; and
(D) the government of the District of Columbia;

(2) “public official” means an officer (including the President and a Member of Congress), a member of the uniformed service, an employee and any other individual, in whom is vested the authority by law, rule, or regulation, or to whom the authority has been delegated, to appoint, employ, promote, or advance individuals, or to recommend individuals for appointment, employment, promotion, or advancement in connection with employment in an agency; and

(3) “relative” means, with respect to a public official, an individual who is related to the public official as father, mother, son, daughter, brother, sister, uncle, aunt, first cousin, nephew, niece, husband, wife, father-in-law, mother-in-law, son-in-law, daughter-in-law, brother-in-law, sister-in-law, stepfather, stepmother, stepson, stepdaughter, stepbrother, stepsister, half brother, or half sister.

(b) A public official may not appoint, employ, promote, advance, or advocate for appointment, employment, promotion, or advancement, in or to a civilian position in the agency in which he is serving or over which he exercises jurisdiction or control any individual who is a relative of the public official. An individual may not be appointed, employed, promoted, or advanced in or to a civilian position in an agency if such appointment, employment, promotion, or advancement has been advocated by a public official, serving in or exercising jurisdiction or control over the agency, who is a relative of the individual.

(c) An individual appointed, employed, promoted, or advanced in violation of this section is not entitled to pay, and money may not be paid from the Treasury as pay to an individual so appointed, employed, promoted, or advanced.

(d) The Office of Personnel Management may prescribe regulations authorizing the temporary employment, in the event of emergencies resulting from natural disasters or similar unforeseen events or circumstances, of individuals whose employment would otherwise be prohibited by this section.

(e) This section shall not be construed to prohibit the appointment of an individual who is a preference eligible in any case in which the passing over of that individual on a certificate of eligibles furnished under section 3317(a) of this title will result in the selection for appointment of an individual who is not a preference eligible.

(Added Pub. L. 90–206, title II, § 221(a), Dec. 16, 1967, 81 Stat. 640; amended Pub. L. 95–454, title IX, § 906(a)(2), Oct. 13, 1978, 92 Stat. 1224.)
 
Haya tuambie yesu alishinda kwa kura ngapi za wizi? Ama huko halikutokea? Maana huku mpaka leo lowassa haamini kilichokea!
 
Back
Top Bottom