Tafakari Ya Kisiasa na kiroho Tanzania yangu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Wakijenga shule hawaingilii wizara ya elimu;

Wakijenga hospitali hawaingilii wizara ya afya;

Wakijenga kisima cha maji hawaingilii wizara ya maji.

Wakiombea mvua hawaingilii mamlaka ya hali ya hewa.

Wakihimiza kilimo hawaingilii wizara ya kilimo.

Wakitoa msaada wa dawa kwa mgonjwa, wanapongezwa.

Wakihoji kwa nini hakuna dawa hospitali, wanaambiwa wanachanganya dini na siasa.

Wakikosoa mfumo wa kisiasa, wanaambiwa wanaingilia siasa!!

Kuna kitu hakiendi sawa.
 
Back
Top Bottom