Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,493
- 5,528
Naendelea na mada zangu za Kumuunga mkono Ndugu Tundu Antipasi Mughai Lissu kwa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali kwa sababu namuelewa. Ili kuweka kumbukumbu sawa mimi sio mwanachama wa CHADEMA wala CCM na wala mimi siamini katika ITIKADI za chama cha CHADEMA. Tofauti yangu ya kiitikadi utaipata kupitia jibu la swali hili.
JE, UKILALA NA NJAA KWA SABABU YA KUKOSA CHAKULA JE SERIKALI INASTAHILI KULAUMIWA? KAMA JIBU LAKO NI NDIO BASI TUKO KATIKA ITIKADI MOJA ILA KAM JIBU LAKO NI HAPANA BASI ITIKADI ZETU NI TOFAUTI. Sasa Tuendelee. Kodi nini?
Kodi ni Mchango wa Hiyari ya Lazima unaotolewa na wananchi na wakazi wa nchi kuchangia uendeshaji wa shuguli za serikali.Ni hiyari kwa sababu lazima wanachi wakubaliane kulipa mchango huo kupitia vyombo vya maamuzi na ni lazima kwa sababu ikishapitishwa usipolipa ni kosa.
Kwa misingi hio basi KODI ndio chanzo kikuu cha mapati ya serikali yoyote duniani. Katika malipo ya Kodi kuna aina mbili za kodi pamoja na nyingine nyingi humo ndani nazo ni KODI za MOJA KWA MOJA(DIRECT TAXES) na Kodi ambazo sio za moja kwa moja (INDIRECT TAX)
Katika mifumo hii miwili ya kodi msingi wa ukusanyaji na utoaji wa taarifa za kodi unazingatia vigezo mbalimbali ikiwamo vyanzo ya mapato na urahisi wa ukusanyaji kwa upande wa serikali na kwa upande wa mlipaji. Kwa kawaida gharama ya kulipa au kukusanya kodi inapaswa kuwa ndogo ili iwe na tija. Ni upumbavu wa kiwango cha lami kutumia Bilioni moja kukusanya kodi yenye thamani ya BIlioni moja. Kama unajua hesabu unaelewa huu ujinga unafanyika wapi.
Lakini pia katika mfumo wa ukusanyaji wa kodi kuna kodi zinatozwa wakati wa kupata kipato na kodi zinatozwa wakati kutumia kipato. Zote ni kodi ili kuna yofauti kubwa sana kati ya kodi hizi mbili na ufanisi wake.
Kwa mujibu wa uzoefu, KODI BORA kuliko zote ni kodi zilizounganishwa na huduma(Kwa mfano Kodi ya kusafisha mazingira na ukaona watu wanasafisha mazingira, Kodi ya Huduma za afya na ukapewa huduma ya afya, Kodi ya huduma ya elimu na ukaona huduma ya elimu, kodi ya matumiz ya huduma kama vile bandari, barabara, etc) Hizi kodi mlipaji anazifurahia wakati wa kuzilipa na ni rahisi kukusanya.
Kuna hizi kodi za kuwindana na kutafutana huku mtaani na makofuli eti sijui huna leseni tunakufungia Biashara.Hizi ni kodi kero na ni ama zifutwe au zibadilishiwe utaratibu wa kukusanya. Kwa mfano-Kusajili Biashara kuwe ni Bure halafu ada ya leseni iwe compounded kwenye system with penaltie kama ukcihelewa kulipa with options ya kulipa installments etc. Hakuna haja ya kufungia watu biashara.
Mkaguzi wa Kodi akija akikuta una deni kubwa akiweka kofuli kwenye biashara yako maana yake anakufilisi duka linakuwa Public Property. Kuna ugumu gani hapo?
Sasa niwaeleze vizuri kuhusu TUNDU LISSU
Akiwa Rais wetu huyu BWANA ndivyo atakavyofanya. Hutasumbuliwa Barabarani kuhusu leseni au kodi. Utapata TEX kwenye SIMU yako inakwambia unadaiwa leseni ya MIAKA 3 jumla deni lako ni Milioni 100, Iwapo unafikiri kuna makosa basi piga simu halmashauri/ofisi ya kodi/leseni upate msaada zaidi. Hii inaitwa kuendesha nchi kisasa.
Unaposajili Biashara yako unapewa mafunzo na fursa mbalimbali. Unawekwa katika orodha ya suppliers wa halamashauri husika ili kukiwa nakazi basi na wewe unaweza kuomba kuwa supplier kwa sababu una leseni na kodi unalipa. HAYO NDIO MAENDELEO YA WATU
Tuache kudanganywa na watu ambao hawajui hata wnachofanya. TUMCHAGUA TUNDU LISSU AWE RAIS WETU TUONE MAENDELEO YA KWELI
Nimeandika haya nikiwa katika UFUKWE Kimbiji,Kigamboni Jijini Dar es Salaama
Kizito S.