Tafakari siku yako ya leo: Tatizo la mwenzako leo, kesho laweza kuwa lako

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,688
26,796
Baada ya mwenye nyumba kuona panya anamaliza nafaka zake, aliamua kununua mtego na akautega.

Panya lile jambo lilimpa huzuni sana, akapiga mbiu kuwatahadharisha na wengine akina kuku, mbuzi na ng'ombe kuwa waungane kuutegua mtego huo._

Alianza kwa kusema"Jamani, kuna mtego humu ndani, baba mwenye nyumba kaweka mtego.."

Kuku akahoji:"Mtego wa nini?"

Panya akajibu: "ni wa panya"!!

Kuku akasema:"huo ni mtego wa panya mimi haunihusu.

Ng'ombe na Mbuzi nao walijibu kama kuku alivyojibu kuwa: kwa hiyo we panya pambana na hali yako kwani huo mtego hautuhusu sisi bali ni wako"

Basi panya hakupata msaada ilibidi ajihadhari mwenyewe kutokana na mtego husika.

Siku moja usiku nyoka alipita karibu na ule mtego na kuugusa ndipo akanaswa mkiani.

Mwenye nyumba akajua mhalifu wake ashampata, akapeleka mkono gizani achukue mtego pamoja na panya alienaswa, ghafla akang'atwa na yule nyoka.
_(Mwenye nyumba ilibidi kupelekwa hospitali kwa matibabu)

Wakati anaendelea na matibabu kuku alichinjwa kwa ajili ya kitoweo cha mgonjwa.
Baadaye mwenye nyumba alifariki, mbuzi na ng'ombe walichinjwa ili watu waliokusanyika kwenye ule msiba wapate chakula.

Mtego wa panya uliua ng'ombe, mbuzi na kuku.."Panya akabaki_

Hapa pana masomo mengi sana ya kujifunza._
1. Tusaidiane ukutwapo na shida.
2. Tuache ubinafsi.
3.Tatizo la mwenzako la leo, kesho laweza kuwa lako.
4. Tusifurahie matatizo ya wengine.
5. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.

Niwatakie tafakari njema.
 
Hiyo pombe ulionza kuinywa usiiache mkuu inakufanya unawaza sawasawa.. hongera kwa somo zuri.
 
Mkuu hujasema nyoka alibakia kwenye mtego au aliishia wapi? au ndiyo hivyo tena.
 
tatizo hata usimame juu ya anga useme hiki ulicho andika ni kazi bure mkuu, Binadamu hatujifunzi wala kushaulika
 
Back
Top Bottom