TAFAKARI: Nini hatma ya makontena ya makinikia?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,114
35,120
Ni zaidi ya miaka miwili sasa toka sekeseke la kuzuiwa kwa makontena ya mchanga wa madini pale bandarini litokee. Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote rasmi kutoka katika mamlaka husika inayotoa mwelekeo kuhusu kinachoendelea au kilichoendelea. Yaani kuna ukimya fulani hivi mzito mnoo wa kulisemea jambo lile. Nimeshindwa kujua ni kwanini?

Kwa niaba ya wazalendo wenzangu ningependa kufahamu yafuatayo:

1. Nini kimeendelea kuhusu yale makontena? Bado yapo? Mpaka lini yalikuwepo au yataendelea kuwepo?

2. Nini kimeendelea hapa nchini kuhusu usafirishaji wa makontena yenye mchanga wa madini kwa kipindi chote hichi cha miaka miwili?
Usifirishaji umeendelea au umesitishwa moja kwa moja?

3. Sisi kama taifa, tumepata nini au tumekosa nini katika lile sekeseke?
 
Back
Top Bottom