Tafakari namna Kigwangalla alivyowadhalilisha watendaji chini yake, kunyimwa Uwaziri ni adhabu ya kumtosha?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Huyu kijana aliwahi kufunga geti ya wizara kudhibiti wachelewaji akawadhalilisha watendaji wa afya bila kuwasikiliza walikuwa na matatizo gani makwao.

Aliwahi mdhalilisha mzee mmoja Askari tena kwenye mahafali natumai mbele ya familia yake kisa amekosa ukakamavu wa kiaskari. Amewahi kuwadhalilisha wananchi kwenye operesheni za misitu na hifadhi akiwa na kombati Kama Askari kabisa. Aliwahi mtunishia misuli Katibu Mkuu wa wizara yake.

Leo hii inabainika alikuwa anapiga piga na helkopta ya umma na kutumia mafuta ya umma huku akilipwa. Inabainika alitumia vibaya fedha za umma kulipa wasanii.

Alistahili zaidi ya kunyimwa uwaziri, alipaswa kufika Kisutu sema ndo hivyo ni mkubwa.
 
Alimdhalilisha pia na dokta mwaka kisa...

Mambo mengine bwana!! Hivi Mwaka udaktari kausomea wapi i.e ana cheti gani cha udktari wa binadamu - kusoma machapisho ya wikipedia na ku-google Encyclopidia Britanica ndio kumfanye Mwaka awe daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama na kuwachezea kisaikolojia?

Kigwangalla alikuwa sahihi kabisa kumvurumisha Mwaka, hata ingekuwa mimi ningefanya hivyo hivyo - kwa wale walio somea udaktari ukimsikiliza kwa umakini maelezo ya Mwaka kuhusu magonjwa ya binadamu, unabaini kabisa kwamba jamaa huyu anakalili tu anacho soma kwenye machapisho mtandaoni hana hand on experience yoyote kuhusu magonjwa ya binadamu specificaly akina mama in other words is not a trained medical doctor of any form or shape.
 
Uwazi ni kitu muhimu sana kwenye jamii. Acha media zifanye kazi za uchunguzi, serikali itapata faida kubwa zaidi ya hasara wanayoiona sasa
 
Huyu kijana aliwahi kufunga geti ya wizara kudhibiti wachelewaji akawadhalilisha watendaji wa afya bila kuwasikiliza walikuwa na matatizo gani makwao.

Aliwahi mdhalilisha mzee mmoja Askari tena kwenye mahafali natumai mbele ya familia yake kisa amekosa ukakamavu wa kiaskari. Amewahi kuwadhalilisha wananchi kwenye operesheni za misitu na hifadhi akiwa na kombati Kama Askari kabisa. Aliwahi mtunishia misuli Katibu Mkuu wa wizara yake.

Leo hii inabainika alikuwa anapiga piga na helkopta ya umma na kutumia mafuta ya umma huku akilipwa. Inabainika alitumia vibaya fedha za umma kulipa wasanii.

Alistahili zaidi ya kunyimwa uwaziri, alipaswa kufika Kisutu sema ndo hivyo ni mkubwa.
Kigwangalla ana tofauti na gani na yule DED wa Geita aliyenunua VX-R V8 ya TZS milioni 460 ilhali shule za wilaya yake hazina madawati na watoto wanakalia matofali? Yaani hawa jamaa ni kama ukoo wa panya. Chupa na kizibo
 
Back
Top Bottom