TAFAKARI: Maduka ya dawa marufuku kuwa karibu na hospitali lakini biashara ya majeneza ruksa kuuzwa karibu na hospitali

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,085
34,980
Waziri wa Afya leo ametoa msisitizo kuwa ni marufuku maduka binafsi ya dawa kuwa karibu na viunga vya hospitali za umma hivyo yanapaswa kuwa umbali usiopungua mita 500 kutoka hospitali ilipo. Sababu kuu ni kuwa, huenda maduka hayo ya dawa yanahusika katika kuchochea upungufu wa dawa na vifaa tiba kwenye hospitali za umma hivyo kujenga taswira mbaya kwenye jamii.

Tukija upande wa pili, karibu hospitali zote kuu au kubwa za afya za umma hapa Tanzania zimezungukwa na utitiri wa biashara za kuuza majeneza, sanda na viambatanisho vyote vya mazishi. Hili halina mwongozo wala kauli mpaka sasa, hii ikiwa na maana limekubaliwa, kuhalalishwa na kuzoeleka.

Sasa tutafakari nini mantiki na faida katika yote mawili.
 
Waziri wa Afya anahusika vipi na suala la mipango mji? Ninavyojua mimi mamlaka yake yanaishia ndani ya mipaka ya hospitali na hana mamlaka nje yake. Kama anataka kuzuia maduka ya dawa nje ya hospitali aende akabadilishe Master Plan lakini hawezi yeye kutoa amri.

Ama sivyo waziri wa mambo ya ndani anaweza kutoa amri kuwa pasiwe na gesti jirani na polis post, waziri wa kilimo al kadhalika anaweza kulima mchicha katikati ya mji. Na tangu lini waziri anatunga sheria?

Amandla...

Kumbe ni suala la utoaji wa leseni ya kufanya biashara ya ufamasia. Lakini bado naona inaingilia suala ambalo lingeachwa kwenye mipango miji.

Kama mipango miji inaruhusu biashara basi serikali isingepanga aina ya biashara. Exceptions ni zile biashara zinazoweza kuhatarisha maisha ya raia wake au uwezo wao wa kuishi bila bughudha.

Cc. Nguruvi3 JokaKuu Mag3
 
Back
Top Bottom