Tafakari kuhusu UJENZI, MUUNDO na MWELEKEO wa Taifa letu part 1 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafakari kuhusu UJENZI, MUUNDO na MWELEKEO wa Taifa letu part 1

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shayu, Feb 11, 2012.

 1. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #1
  Feb 11, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 502
  Likes Received: 663
  Trophy Points: 180
  Napenda kuandika Andiko hili kuhusiana na mwelekeo wa taifa letu, hii inatokana na uzalendo na mapenzi ya dhati niliyonayo kwa taifa hili na watu wake, sehemu ya kwanza umuhimu wa familia na tafakari kuhusu elimu.


  Kutokana na moyo wangu wa unyenyekevu ningependa kwa dhati kabisa kuandika baadhi ya mambo ambayo nafikiri ni kikwazo kwetu kama taifa kusonga mbele ambayo nafikiri pia bila ya kuyafanyia kazi hatutapiga hatua kama Taifa.
  Mimi nimezaliwa katika taifa hili na nimekulia katika Taifa hili, ni mtoto wa taifa hili, nimelelewa hapa na kukulia hapa ardhi hii imenikuza kutokana na kila kitu inachozalisha, hivyo ni furaha kwangu kuitumikia.


  Lakini pia ninaishi na watu katika ardhi hii ambao tumeamua kuwa Taifa, tumeamua kuwa na malengo ya pamoja ndio maana tumekuwa Taifa. Ni ukweli usiopingika kwamba Taifa ni umoja na pasipo umoja hakuna Taifa. Kwa mantiki hiyo sisi ni ndugu na lazima tuunganishwe na dhamira moja ambayo ni ujenzi wa Taifa letu la Tanzania. Hii ni kwa faida ya vizazi vyetu wenyewe kwa kuwa sisi tuliopo duniani sasa hivi, tuna wajibu wa kutayarisha maisha kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo.


  Hili ni jukumu letu sisi tuliopo sasa hivi duniani na ni maamuzi yetu yatakayo jenga baadae nzuri kwa kizazi chetu au la. Kwa hiyo sisi sote tunaounda taifa hili tunatakiwa kuwa makini sana, Mwelekeo na dira ya Taifa letu unatutegemea sisi, na maamuzi yetu ndiyo yatakayo leta madhara au faida kwetu.


  Kuna umuhimu mkubwa sana wa sisi kuwa Taifa kwani maendeleo yetu kama mtu mmoja mmoja hayatofikiwa kwa haraka kama hatutaishi katika Taifa.


  Taifa ni msingi wa maendeleo ya binadamu na binadamu wamepata maendeleo makubwa sana katika historia pale walipoishi kama taifa wakiongozwa na dhamira ya kujiletea maendeleo na furaha.


  Kwa hiyo ningependa kuwakilisha andiko hili kuhusu UJENZI, MUUNDO na MWELEKEO wa taifa letu ili kusudi kila Mtanzania ajue kwanini tuko Taifa na jukumu la kila mmoja wetu katika ujezi wa taifa hili. ‘’ Ni muhimu sana kutambua umoja ni muhimu sana katika ujenzi wa Taifa imara ’’


  Kwa Uimara wa roho yangu na uzalendo wa roho na moyo ningependa kuandika kwa faida ya umma ili taifa hili tupate mwelekeo, tujue nini tunachohitaji kama taifa na nafasi yetu kama Taifa duniani.


  Mahusiano yetu kati yetu tunaoishi pamoja kama Taifa ni jambo la msingi, ndio nguzo ya kwanza katika ujenzi wa taifa imara pasipo kuwa na mahusiano mazuri miongoni mwetu kama watu wa Taifa hili tusitarajie kupata maendeleo, hata pengine hayo madogo tuliyonayo yakapotea.


  Ni muhimu kujenga mahusiano mazuri miongoni mwetu, watu wa taifa hili, ili kujenga taifa imara, siamini bila hili tunaweza kufanikiwa. Ni lazima tujenge mahusiano yetu upya kama binadamu tunaoishi katika taifa moja, tutengeneze nia zetu upya na mwelekeo wa mawazo yetu upya. Lazima tujue kila mmoja anajukumu katika jamii inayomzunguka na kila mmoja wetu anastahili heshima an kupendwa.
  TAFAKARI KUHUSU UMUHIMU WA FAMILIA KATIKA UJENZI WA TAIFA IMARA.
  Familia ni sehemu ndogo sana ya Taifa, lakini ni muhimu sana katika Taifa. Ni muhimu sana Taifa kuangalia taasisi hii ya familia kwa umakini mkubwa na kuipa umuhimu unaostahili. Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya ‘’familia na taifa’’ huwezi kutengenisha.


  Familia imara zenye maadili bora huzaa taifa imara, kupuuza familia sio jambo la busara, bila familia imara kamwe hatutaweza kujenga taifa imara. Bila kuwa na wazazi wanaojali familia zao kamwe hatutaweza kujenga Taifa imara, tutakuwa tunajidanganya. Kwa sababu kiini cha Taifa ni familia inayoundwa na mwanamke na mwanaume ndio chanzo chake, ukosefu wa maadili katika Taifa na katika uongozi mara nyingi unatoa taswira ya kutokuwepo maadili na uwajibikaji katika familia, hivyo kuna umuhimu wa familia kulindwa ili kulinda maadili ya taifa. Lakini pia ni kweli kama tukishindwa kuongoza familia zetu ambazo ni ndogo tutawezaje kuendesha Taifa katika maadili na misingi imara? Tusipo angalia maadili ya familia tusitegemee kupata viongozi wazuri katika Taifa hili watakaoleta order na mwelekeo wa Taifa.


  Uhusiano na maadili ya Baba na Mama katika familia ni muhimu kwakuwa pasipo wao kuwa na maadili na kuwa mfano ni vigumu kwao kuwatawala na kuwaongoza watoto na matokeo yake tutakuwa na watoto wasiokuwa na malezi bora, watakao kuja kuwa viongozi na watumishi wa umma na tutakosa mwelekeo kama Taifa.


  Ni muhimu sana kutilia mkazo katika familia na kuipa umuhimu mkubwa sana, pasipo kuwa na familia zinazowajibika hatuta songa mbele kama Taifa. Sheria lazima zitungwe kulinda maadili ya familia, ni ukweli usiopingika kwamba bila order katika familia ni vigumu kupata order katika Taifa. Lakini pia bila mahusiano mazuri ya wazazi wa Taifa hili ni vigumu pia kuwalea watoto wetu katika maadili bora.


  Hatutaweza kuwa na mwelekeo wa Taifa pasipo hili. Lazima tuwalee watoto wetu katika wajibu wa Taifa , binafsi na wa familia, Lazima tuwaangalie watoto kwa ukaribu sana ili kuwajengea nidhamu angali wadogo ambayo ni muhimu sana kwa maendeleo yao na ya Taifa.

  Tunapo tengeneza Taifa tunajenga kwanza msingi, na msingi wa Taifa lolote lile ni familia imara zenye malezi bora hatutaweza kufanikiwa pasipo hilo, pasipo nidhamu katika familia ambayo ni muhimu katika ujenzi wa Taifa imara.  TAFAKARI YANGU KUHUSU ELIMU


  Taifa litahitaji elimu ili liendelee. Madhumuni ya elimu ni kumkomboa mtu na kumuwezesha kuyatawala mazingira yake.
  Elimu ni nyenzo muhimu katika kuleta mabadiliko na kutatua matatizo yanayo mkabili binadamu katika dunia. Ni ukweli usiopingika kwamba Taifa lililo jishughulisha sana katika kutafuta maarifa ndilo lililopata uwezo wa kutawala mataifa mengine hivyo ni muhimu kwetu sana kutia bidii katika kutafuta maarifa ili kunyanyua Taifa letu.


  Elimu haina umuhimu kama haina uwezo wa kutatua matatizo yanayo mkabili binadamu, elimu yetu lazima iwe elimu yenye kutatua matatizo yetu yanayo tukabili na sio kwa dhana ya kupata ajira au hela.

  Hatutaweza kupata maendeleo makubwa kama tukiendelea na dhana hiyo vichwani mwetu. Na sidhani kama ndio lengo letu sisi kuwa Taifa, lengo la taifa lolote ni kufikia kilele fulani cha mafanikio na ndio furaha ya Taifa lolote.
  Hatutaweza kujivunia elimu yetu kama haitusaidii kufanya hivyo kama haina matokeo ambayo yataibadilisha Taifa letu ambayo kila mmoja wetu atayaona matunda yake.


  Swali ni kwamba kwanini Taifa kama Taifa linasomesha watu wake? Lengo kuu ni kunufaisha Taifa na sio watu binafsi pekee. Taifa lolote lazima liwe na malengo, na malengo hayo yatafikiwa ikiwa tu tutakuwa na elimu ambayo itatufikisha kufikia malengo hayo.


  Bila kuwa na elimu hatutafikia malengo tunayohitaji kama taifa, kwahiyo lazima tuwe na dira kama Taifa itakayo tuongoza wote.
  Kwahiyo Msingi wa elimu ni kumuwezesha binadamu aishi maisha mazuri zaidi, yasiyo kuwa na madhara kwake na jamii inayomzunguka, kumuwezesha kuufikia ustaarabu na kuachana na ujinga ambao una madhara makubwa sana kwa binadamu. Elimu lazima imbadilishe binadamu kutoka ndani ili kumfanya awe mwenye nidhamu na maadili na mwenye uwezo wa kuyatawala mazingira yake.


  Msingi wa elimu ni suluhisho ya matatizo ya binadamu bila hilo elimu haitakuwa na manufaa kwetu kama haitatuwezesha kuishi kwa pamoja kwa ustaarabu na busara na kusuluhisha matatizo yanayotukabili kama watu tunaoishi katika taifa moja.
  Elimu yetu haitokuwa na msingi kama haitawawezesha wazazi kulea watoto wetu kwa pamoja na kuwatawala katika misingi ya maadili na mwelekeo utakao leta tija kwa Taifa na kwa watu binafsi katika misingi ya wajibu na majukumu, tukishindwa kuwatawala watoto wetu, tutawezaje kutawala taifa? Hatutaweza kuendesha Taifa letu bila ya kuwa na mpangilio utakao leta manufaa, hatutaweza kutawala taifa letu bila nidhamu. Hatutaweza kuzalisha viongozi wazuri bila nidhamu na maadili. Elimu yetu lazima ilete relief kwa ‘’Taifa’’ na watu lazima itibu ujinga wetu ambao una madhara makubwa kwa Taifa na mtu mmoja mmoja na kutufanya tuishi kwa busara na amani miongoni mwetu lakini pia tuishi kwa haki na utaratibu.  Kwahiyo wazazi wakiweza kuwatiisha watoto wao itakuwa hatua moja kubwa kwetu kama Taifa na hili halitoweza kufikiwa pasipo juhudi za pamoja na kubadilika kwa wazazi wenyewe na kujua wajibu wao kwa kuwa mfano. Hatutoweza kuzalisha Madaktari wazuri, wahandisi wazuri na waandishi wa habari wazuri pasipo maadili, wazazi wana majukumu ya msingi kabisa katika ujenzi wa Taifa imara, wanahitaji kuwa wamoja katika malezi ya watoto lazima wajue tunajenga Taifa moja kwa faida ya wote bila hivyo hatutafanikiwa kama Taifa, tutakuwa na Taifa lenye fujo lisilo na mpangilio wala heshima miongoni mwa watu wake.


  Ni ukweli usiopingika kwamba hatutaweza kumwingizia maarifa yeyote yatakayoleta manufaa kwa binadamu bila kwanza binadamu kuwa na nidhamu ya akili na mwili, bila kumtengeneza akili yake katika mwelekeo fulani na kuacha mambo yasiyokuwa na faida na yenye madhara kwake na kutafakari mambo yenye faida kwake na jamii, bila nidhamu na maadili hatutaweza kupata maarifa yeyote yale na wala elimu yetu haitakuwa na tija ya aina yeyote ile ni lazima tu regulate behavior za watoto na vijana ili kuwaingizia maarifa kwenye akili zao.  Akili ya binadamu inayumba kila mahali ili iwe na manufaa kwa binadamu lazima ielekezwe katika mwelekeo fulani, binadamu anayefanya mambo yake bila discipline hawezi kuwa na faida katika elimu yake, hawezi kuota mizizi katika busara na maarifa, hawezi kwenda mbele kama mtu na kama Taifa.  Mawazo yetu kwa pamoja ndiyo yaliyojenga Taifa tulilonalo, Ni kutokana na aina ya mawazo yetu ndio yaliyo tufanya tuwe na Taifa la aina hii lakini ni mawazo hayohayo yanauwezo wa kubadilisha Taifa hili.


  Ni juhudi zetu na mawazo yetu ndio yatakayojenga Taifa hili inategemea sisi kama Taifa tuna strive katika mambo gani nature itatupa zawadi yetu kulingana na juhudi zetu na mawazo yetu, Taifa maskini ni zao la juhudi finyu na mawazo duni huu ni ukweli usiopingika kabisa lakini sisi kama Taifa, tunaweza kubadili hali hii ni juhudi zetu za pamoja na utayari wetu wa kuona mabadiliko yenye tija kwa watu wote.


  Tujiulize ni vitu gani tunaongea tukiwa nyumbani, bar na sehemu nyingine, kuhusu ujenzi wa taifa letu na kama vitu hivyo vina malengo chanya kuhusu ujenzi wa taifa letu? Kila wazo letu ndani ya vichwa vyetu lina faida au hasara katika ujenzi wa Taifa na mtu binafsi, hivyo ni muhimu sana kwetu kuangalia ni aina gani ya mawazo tunafikiri na kuyatamka kuhusu Taifa letu. Mawazo yetu ndio yanayojenga dunia tunayoiona kwa macho na kila kitu kilichopo kwahiyo watu wanaofikiri katika ujenzi ndio wenye kupata faida. Kwahiyo ni muhimu kwa Taifa kuwa na discipline ili kupata maendeleo yake. Kwahiyo bila kuwa na mpangilio kama Taifa hatutaweza kuendelea.  Walimu kuhusu malezi na discipline ya watoto wetu, wao wataendeleza discipline ya watoto waliyotokea nayo nyumbani ni lazima wawe wenye akili za kupevuka na waliojitolea kwaajili ya malezi na madili ya watoto kwakuwa ni vigumu kumpatia mtoto elimu pasipo discipline na elimu yake ikawa na faida kwa jamii na kwake mwenyewe, elimu ni muhimu katika makuzi ya akili na roho lakini haiwezi kufanikiwa pasipo maadili na nidhamu. Discipline ya walimu ni muhimu sana katika malezi ya watoto.
  Discipline ni uwezo wa ku control mwili na akili dhidi ya irrational behaviours or impulses ambazo zina mtofautisha kati ya binadamu na wanyama kwahiyo walimu wetu lazima wawe hivyo ili badala ya kuwa walimu wasije wakawa simba na kuharibu watoto wetu na moral behaviours zao. Lazima watoto wafundishwe elimu lakini pia moral behaviours ili wawe productive na wenye manufaa katika Taifa. Kwasababu hatutaweza kuendelea kama Taifa pasipo morals, hatutaweza kujenga Taifa hili likawa na nguvu na tija, kuna uhusiano mkubwa sana kati ya kuporomoka kwa morals katika watu wanaounda taifa na kuanguka kwa Taifa.


  Kwa hiyo walimu watawafundisha wanafunzi skills zitakazo wawezesha kuwa huru na raia wenye kujitegemea na wenye uwezo wa kuzalisha mali na kuiwezesha serikali kupata kodi kwa ajili ya huduma za jamii.
  Elimu itakayowawezesha kutambua uhusiano wao na jamii na majukumu yao katika taifa na kwao binafsi, lazima vitu hivi viingiliane na watambue hilo.

  Kwahiyo ni lazima tutilie maanani katika elimu ya msingi ambayo ni muhimu katika kukuza akili ya mwanafunzi lengo ni kukuza na kuingiza maarifa katika akili ya mwanafunzi ili awe na uwezo wa kufikiri na kujiamuilia maamuzi yake mwenyewe asiwe mtegemezi, na sio kunakili na kuweka kichwani maarifa bali kutafakari kufamu na kuendeleza maarifa aliyopewa kwahiyo msingi wa elimu uwe ni kukuza milango ya ufahamu ya mwanafunzi na uwezo wa akili yake katika kutafakari na kuchanganua mambo.


  Lazima tuangalie ukuaji wa akili yake na sio kuhifadhi maarifa pekee. Tunamjenga ili awe baba mzuri, mama mzuri na raia mzuri anayewajibika kwa Taifa lake jamii yake na familia yake na ili awe mzalishaji mali au kiongozi mzuri.


  Lazima tupime ukuaji wa akili yake kutoka shule ya msingi hadi chuo kikuu. Uwezo huu unakua hatua kwa hatu na bila umakini tunaweza kuzalisha watu ambao hawako mature na hatutaweza kuwa productive katika taifa.


  Hili sio suala la kupata ajira tu bali ni la ujenzi wa Taifa, ili Taifa letu liendelee, kwakuwa bila hivyo hatutapata watu waliopevuka kiakili watakaoweza kuendesha Taifa hili. Hatutaweza ku organize Taifa letu wala kuwa na discipline vitu ambavyo ni muhimu kwa Taifa.
  Elimu ni kama ukuaji wa mti unalishwa na kukua mpaka unapozaa matunda na binadamu ili azae matunda lazima ajengewe mazingira ya kufikiri mwenyewe na kuzalisha, kwahiyo elimu iwe ni source ya kumwezesha mwanafunzi akili yake ku develop na kujitegemea katika fikra ili atoe matunda na sio kuwa maktaba ya mawazo ya watu wengine.


  Elimu yetu lazima ilenge katika ujenzi wa Taifa na si vingine ili Taifa lizalishe na liwe kitu kimoja. Lazima tujenge muundo kati ya sekta binafsi na ile ya umma ili mfumo u operate kwa faida ya umma na sio kundi fulani kwa vile tuko Taifa kwa faida na furaha ya umma na sio watu binafsi binafsi, hatutaweza kuwa Taifa kama hatutakuwa na mfumo unao operate pamoja kwa faida ya wote.
  Tunaweka maindi kwenye mashine ya kusaga, kwenye mashine ya kusaga kuna components zinazofanya kazi kwa pamoja katika kusaga na kuleta faida na faida ni ”unga” pasipo hivyo Taifa letu halitoweza kupata faida nachelea ni naweza kwenda mbinguni miaka elfu moja na nikirudi nitakuta taifa hili halijaendelea au yale maendeleo kidogo tuliyo nayo yakapotea tukarudi nyuma.
  Kwakuwa ni ukweli usiopingika hatutaweza kujenga Taifa katika misingi ya ubinafsi na kutofuata sheria na Haki, tukasalimika kama Taifa, pasipo kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuharibu tayari mali tulizo nazo.


  Pasipo utaratibu maadili na nidhamu hatutaweza kujenga Taifa lolote na kuwa na mwelekeo wa Taifa na taifa letu kuwa endelevu.
  Maadili ni kama kingo dhidi ya uharibifu ni sawasawa na mto usivyoweza kuishi pasipo kingo, sawasawa na Taifa bila maadili litasambaratika katika uso wa dunia.
  itaendelea….
   
Loading...