Tafakari ingekua wewe km mume au mke ungefanyaje? ?????

NGULI

JF-Expert Member
Mar 31, 2008
4,803
637
Jamaa mmoja alikuwa akitokea shamba pamoja na
mkewe. Wakiwa njiani waliona uyoga, wakaung'oa na
kwenda nao nyumbani kwa lengo la kwenda kupika na kuula. Lakini kabla ya kufika nyumbani, wakahofu kwenda kula ule uyoga wakihisi unaweza kuwa si uyoga wa kula.
Basi wakaamua wapike uyoga kidogo,na kiasi
waubakishe, halafu ule waliopika wampe mbwa wao,
asipokufa mbwa basi ule waliobakisha nao wale.

Mbwa akala uyoga ule. Wakakaa siku ya kwanza,ya
pili, mbwa hajafa wakaamua wapike ule uyoga
uliobakia nao wakala.

Walipomaliza kula tu, mara mtoto wao wa kiume
akaingia ndani akitokea shule, na kuwaeleza wazazi
kuwa amemuona mbwa wao amekufa.

Wazazi wakapigwa na butwaa wakijua basi nao mwisho wa maisha yao umefika, na muda wowote watakufa tu kwa kuwa nao wamekula uyoga kama mbwa alivyokula.

Basi yule baba akaamua kumwambia mkewe anaomba atubu mbele yake kwa kuwa kifo kinamjia wakati wowote. Jamaa akaanza kumwambia mkewe amsamehe kwani ni maovu mengi alifanya. Kwanza msichana wa kazi waliomfukuza akiwa na ujauzito, ule ni ujauzito wake. Mdogo wake na mkewe wa kike anayeishi naye pale ni mpenzi wake wa siku nyingi. Pia ana watoto wengine watatu nje ya ndoa, na kila mtoto ana mama yake.

Mama akasema nashukuru kwa hayo yote, Basi naomba nani ni tubu Kwako. Huyu mtoto wa kiume mdogo si wako nilizaa na Shamba boy wetu na huu ujauzito nilionao sasa ni wa mpangaji wetu humu ndani.

Jamaa kusikia hayo akapandwa na jazba ukawa ugomvi mkubwa mule ndani.

Wakati wakigombana, mara mtoto wao wa kwanza wa
kike akaingia ndani na kukuta wakigombana.
Akawauliza ,Baba na mama mnagombania nini humu
ndani,badala ya kwenda kuona mbwa wetu amekufa kwa kugongwa na gari kule nnje?

Wazazi waliposikia kuwa mbwa amekufa kwa kugongwa na gari walibaki wanatazamana na kupigwa na bumbuwazi.




TAFAKARI INGEKUA WEWE KM MUME AU MKE UNGEFANYAJE? ?????
 
Hapo inategemea ni maeneo gani.
Kama ni Iringa panakuwa hapajaharibika kitu.
Kwa wanaojua kusoma katikati ya mistari watanielewa.
Geoff, Maskini_Jeuri na Next Level samahani kama nimewakwaza:D
 
Mh Nguli ; give us a break hii kitu inaletwa humu kwa sytle tofauti mpaka nashindwa hata kuhesabia hii ni mara ya ngapi!
 
Aah! Mkuu hii ilishawahi kuletwa humu jamvini na tukaichangia.
kama vipi Mod Ipotezee.
 
Kwanza kitendo cha kumjaribisha mbwa, ambaye naye ni kiumbe cha Mwenyezi Mungu ni zambi. Ni siku zao 40 zimefika. Mimi naona ngoma droo....! Na waache utumbo huo wa kula kwa bahati nasibu! Hata hivyo naona walishindwa kuulizia vizuri kwa jirani kwa kuwa either hawana mahusiano mazuri nao au ni uchoyo wa kushare nao huo uyoga. Hivyo, wajirekebishe hapo mara moja.
 
Back
Top Bottom