Tafakari: Hivi hapa Nchi ilipofikia tunahitaji WAZIRI MKUU MPYA?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafakari: Hivi hapa Nchi ilipofikia tunahitaji WAZIRI MKUU MPYA??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Meitinyiku L. Robinson, Apr 22, 2012.

 1. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumaini langu ni kwamba member wote mmeamka salama. Na naomba tusaidiane hili;

  Kumbukumbu zangu zinaonesha kuwa Nchi yetu mpaka hapa ilipofikia ilishwahi kuwa na Mawaziri Wakuu 9 toka tupate Uhuru na ili kuweka kumbukumbuku sawa nitaomba niwataje na kama kuna nitakapokwenda tofauti nipo tayari kurekebishwa

  Mhe. NYERERE Julius Kambarage
  Mhe. MORINGE Edward Sokoine
  Mhe. MSUYA Cleopa David
  Mhe. SALIM Ahmed Salim
  Mhe. WARIOBA Sinde Joseph
  Mhe. MALECELA John
  Mhe. TULUWAY Sumai Frederick
  Mhe. LOWASSA Ngoyai Edward na huyu tumtazamiaye
  Mhe. PINDA Mizengo Kayanza Peter

  Sasa kama wasemavyo Kiutaratibu watu hawa wakishastaafu huendelea kulipwa na Serikali (Kodi za Wananchi) na hata wanpokufa familia zao bado huendelea kufaidi ama kuneemeka kwa kodi za Wananchi tu kwa sababu ya nafasi walizowahi kuwa nazo katika Taifa hili ikiwa na maana kwamba watajwa hapo juu mpaka ninapoandika hapa ni kwamba wao bado wanalipwa na wataendelea kulipwa labda mpaka Kristo arudi.

  Hili siwezi kulijengea hoja nimelichukulia kama utangulizi manake ni utaratibu ambao ulikwisha pitishwa hivyo hata kuujadili ni sawa na kujaza maji gunia labda kwa ushauri Katiba mpya tunayoitazamia hili litizamwe kwa jicho lingine. Kinachonigusa zaidi ni swala la "kama" Waziri Mkuu aliyepo ama atajiuzulu au kutolewa na Mkuu wake je kuna haja kweli ya kuteua Waziri Mkuu mpya kuliongoza Taifa hili?? Hii ni kwa kuzingatia utangulizi huo hapo juu na ikizingatiwa kuwa Mrisho Kikwete toka aingie madarakani amekwisha kuwa na Mawaziri Wakuu wawili hivyo kama atateua mwingine basi atakamilisha jumla ya Mawaziri Wakuu watatu katika kipindi chake.

  Mawaziri Wakuu ambao watalipwa na kuendelea kulipwa fedha za walipa kodi katika maisha yao yote wao pamoja na familia yao. Mkapa alikwishawahi kuulizwa ni kwa nini hakumbadilisha Frederick Sumai na badala yake akamteua tena kwa kipindi kingine jibu lake lilikuwa fupi alisema naona huruma fedha za Watanzania kuendelea kumlipia Waziri Mkuu mwingine nitakaye mteua. Kama alimaanisha ama kama hakumaanisha hilo siwezi fanya mada ila binafsi niliguswa na majibu yake manake kama kweli angeteua mwingine basi idadi yao ingeongezeka.

  Hivyo mimi nadhani tuendelee kujiuliza na kushauriana je Nchi yetu hapa ilipofikia tukizingatia kutafunwa kwake kote, tukizingatia uzembe wa watendaji na wakuu wake, tukizingatia matatizo yaliyopo katika taasisi mbalimbali za Serikali na nyinginezo, tukizingatia umasikini na shida tulizonazo Watanzani ambayo kwayo wao ni "maisha bora", tukizingatia hitaji letu kama Taifa na kubwa zaidi tukizingatia kwamba sisi ndio wahusika wakuu na walipaji halali wa mishahara na mahitaji mengine ya huyo Waziri Mkuu akiwa katika nafasi yake na hata atakapostaafu, akiwa hai na hata atakapotwaliwa.

  MWISHO laiti ningekuwa JK ningedhihirisha kiwango cha busara nilicho nacho kwa kuamua kuweka kando swala la makundi, na kuamua kujishusha na kuamua kulitanguliza Taifa mbele hivyo kuamini pasipo shaka kuwa katika majina ya wasstafu tajwa hapo juu mbali na wale waliokwisha tangulia katika haki (Mungu awalaze pema peponi) bado wapo si wenye nguvu tu bali wazalendo pia; hivyo ili kulisaidia Taifa na Wananchi wangu ningekaa chini na kuamua kuchagua mmoja kati ya hao ili kumrithi huyu tumtazamiaye.

  Mungu Ibariki Tanzania.

  MEITINYIKU L. Robinson.
   
 2. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Tukiitoa CCM madarakani tunawaondoa wakuu wa mikoa, waziri mkuu na vyeo vya kupeana kiundugu na kwa kujuana
   
 3. K

  Keil JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Umemsahau Simba wa Vita, Kamanda Rashid Mfaume Kawawa (RIP)
   
 4. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thakx Brother Keli!

  Duh what a mess
   
 5. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kuwa na orodha ndefu ya Mawari wakuu wastaafu ni gharama. Lakini nadhani kuna zaidi ya gharama ni vyema kufanya tathmini ya utendaji wao kuona kama unatija kwa sasa. Kama utaona katika mchakato unaoendelea dodoma hivi sasa, inaonekana PM yuko tayari wanaotuhumiwa wachukuliwe hatua, lakini Rais amekuja na kukebehi kuwa huu ni upepo tu, kwa hiyo Waziri Mkuu pamoja na wabaunge wote wapo dodoma kuona upepo wa namna gani uendeshwe dodoma katika kipindi watakachokuwa bungeni. Lakini pia amelidhalilisha bunge kama muhimili muhimu kwa nchi na kuwaonyesha wananchi kuwa wakuu hawa wako dodoma hakuna wanachokifanya zaidi ya porojo za uwoga na unafiki.

  Kikubwa zaidi Rais amedhihirisha kwa sasa Tanzania hatuhitaji PM mwingine kwa kuwa hana kazi za kufanya na kuwa yeye ndiye achukuwe nafasi ya Waziri Mkuu hadi hapo utawala utakapobadilika.
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nadhani kuanzia rais, pm, mawaziri majoja na wabunge waondoke ili waadilifu na wenye uchungu na nchi hii wakae pale watuongoze
   
 7. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Watz hatuwezi kushindwa kuwalipa mawaziri wakuu wastaafu kama nchi inaongozwa kwa tija,huwezi kuwa na viongozi wasioweza kusimamia rasilimali na mikakati ya maendeleo kwa kuogopa kuwaondoa kwa kigezo cha kuwa na mzigo wa kuwalipa,pesa inayoibiwa kwa mwaka ni mara milioni ya ile atakayolipwa waziri mkuu,tuache mzaha ktk kufikiria kwetu hatuwezi kupata maendeleo kwa kucheka na viongozi,wanatakiwa wawajibike kwa kutuletea maendeleo na si kutuibia au kuzembea wengine waibe,lazima tukatae kuburuzwa na lazima tuoneshe kuchukizwa na hali hii ya wizi wa mali za umma.viongozi tuliwachagua tukiwa tunawaamini hivyo wanapopoteza uaminifu hatuna sababu za kuwalea,cheo ni dhamana kwanini watuchezee?kwanini waanze ulafi?kwanini wadokoe?tukubali kuwa sheria ni msumeno na hakuna aliye juu ya sheria.wawajibike na ikibidi wawajibishwe na si kuleana.
   
 8. r

  rohrer Member

  #8
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Italia ni moja ya nchi duniani zinazoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya mawaziri wakuu ukianzia mwaka 1945. Je wao wanawezaje kubeba mzigo wa mafao ya mawaziri wakuu wastaafu bila kuwaumiza walipa kodi wao?
   
 9. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kabla ya kujibu swali lako labda ningependa kujua ni vigezo vipi umevitumia kuifananisha Tanzania na Italia!
   
Loading...