Tafakari: Funika aibu zao na sio kuwaaibisha

La Quica

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
916
2,040
Baada ya kusafisha na kupanga nyumba yangu, kaka yangu alinipigia simu na kuniambia, "Mimi na mke wangu tunakuja kukutembelea."

Nilienda jikoni kuwaandalia kitu, lakini sikuweza kupata chochote cha kuandaa. Baada ya kufikiria sana na kupekua, nilichoweza kukiona ni machungwa machache. Kwa hivyo, nilitengeneza vikombe viwili vya juisi baridi mara moja.

Ndugu yangu na mkewe walipofika nilishtuka kumuona akiwa na mama mkwe wake ambaye alikuja kuwatembelea kwa mara ya kwanza. Kwa hivyo nikatoa vikombe viwili vya juisi kwa mkewe na mama yake, na nikampa kaka yangu kikombe cha maji, nikisema, 'Najua kwamba unapenda Sana Kunywa Sprite.'

Alikunywa kinywaji na akagundua kuwa ni maji ya kawaida. Na ghafla mama mkwe wake akasema, Nina kiu ya Sprite na kumuomba kaka ampe

Hapa nilishtuka na nikajua ninapata aibu lakini kaka yangu aliniokoa kwa kumwambia, 'nitakuletea glasi yako kutoka jikoni.' Baada ya muda tulisikia sauti ya glasi ikivunjika jikoni. Kisha akarudi na kumwambia mama mkwe, 'Samahani, iliniponyoka mkononi na glasi ikavunjika. Lakini hakuna shida, nitaenda dukani kukununulia nyingine.

Mkwewe alikataa na kusema, "Hakuna haja haikuwa ridhiki yangu hata hivyo" Mwishowe wakati wanaondoka, kaka yangu aliniaga na akanipa pesa mkononi na kusema, "Usisahau kusafisha ile sprite jikoni sisimizi wasije wakaharibu" Na aliniaga kwa tabasamu na upendo. Kwa njia hii, kaka yangu alijali hisia zangu na kuficha kasoro yangu.

HUU NI UPENDO WA ZAIDI YA NDUGU WA DAMU

Unapokuwa katika nafasi, tumia kuinua wengine. Kumdidimiza mtu yeyote kamwe hakutakufanya uwe bora!

JE! UNAFICHA AIBU ZA WENGINE AU WEWE NDIO NAMBA MOJA KUWATANGAZA NA KUYASEMA VIBAYA MAPUNGUFU YAO?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom