Uchaguzi 2020 Tafakari: CHADEMA na ACT-Wazalendo kuhusu karatasi za ziada za kura

naxon

JF-Expert Member
Dec 6, 2014
367
199
Salaamu, Kwanza niwapongeze vyama tajwa kwa mwitikio mkubwa vinao upata kutoka kwa wananchi kwa muendelezo wa kampeni zinazoendelea tofauti na mategemeo ya watawala.

Wote tunajua maelekezo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi kuhusu uwepo wa karatasi za ziada za katika vituo vya kupigia kura. Tume imetoa sababu kadhaa juu ya utaratibu huu.

1. Kumsaidia mpiga kura kuweza kupiga kura kwa Mgombea mwingine ndani ya kituo endapo atabadili maamuzi yake.

2. Kumsadia mpiga kura kupiga kura kwa usahihi endapo ile ya kwanza ilikuwa imepigwa kimakosa. Wanabodi hoja hizi zinaweza kuwa na lengo la kumsadia mpiga kura lakini bado zina ukakasi mkubwa.

Mfano ni ngumu mtu kupiga kura halafu akageuza maamuzi hapohapo, labda kama kuna jambo la ziada litalokuwa linafanyika kwenye kituo ukizingatia Mf. wa karatasi za kupigia kura kwa wagombea urais wenye nguvu zaidi, kuwa wa kwanza na wa mwisho(zinaweza kuonesha mielekeo wakati wa upigaji kura).

Hoja ya kusahihisha makosa ya awali yaliyojitokeza wakati wa kupiga kura hii ni hoja mfu na hatari sana. Je, uchaguzi huu hautakuwa na kura zilizoharibika? Kwasababu hiyo hapa ndio naona wagombe kupata kura nyingi kuliko chaguzi zilizopita.

CHADEMA & ACT WAZELENDO UCHAGUZI NI HESABU.
Binafsi ukiachana na makando kando ya uchaguzi mzima, kuna uwezekana mkubwa wizi ukafanyikia hapa kwa mgombea kupata kura nyingi na takwimu zikaonesha kura chache sana zimehsribika.

Kumbuka kisingizio kikubwa cha tume kitakuwa ni tuliruhusu wapiga kura kurudia kama kuna makosa wakati wa kupiga kura. Hivyo karatasi za ziada zinaweza kutumika kwa namna nyingine tofauti kuongeza idadi ya kura na zikatolewa kwa sababu hio ya NEC.

Niwakati wa kutilia mashaka kwa kila kinachofanyika ili kujiridhisha. Lakini pia kureview vipengele vya sheria vinavyoipa mamlaka tume ya kutoa maamuzi hayo.

Ikumbukwe majuzi tu tume imetoa maelekezo juu ya kutumia, pass, NIDA au leseni ya gari kupiga kura kwa wale waliopoteza vitambulisho vyao, je sheria zinasemaje?

Kama zinarusu mmejiridhisha na mazingira yatayowezesha utatatibu huo kutumika. Kwasasa ni wakati wa kutumia akili kubwa na uwezo mkubwa kuwakabili. Tofauti na hivyo mtaungwa mkono na wananchi kwenye kampeni after a short time wenzenu wakacheza na hesabu mchezo ukaisha.
 
Hizi mbinu zote hazitafanikiwa.

Idadi za karatasi zilizoharibika zinabidi ziendane na zilizoongezwa na zikatumika. Tofauti na ivyo ni wizi mtupu.

Kama vile naona uchaguzi hautafanyika mwaka huu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom