Tanganyika50
Member
- Dec 8, 2011
- 97
- 19
Wana jamvi,
Labda ni haya makengeza yangu.Ila nimejikuta nikitafakari mambo kadha wa kadha yanayoendelea humu kayani kwetu.
La kwanza ni taarifa niliyo isikia kwenye radio kuhusu Mh.Jakaya Kikwete,Rais wa Jamhuri yetu ambaye inaripotiwa ameonesha flexibility kwa kukubali kurusha ndege (Nadhani!) kutoka Mkoa mpya wa Simiyu mpaka Jijini mwanza ili kupokea kikombe cha soka cha Dunia katika hadhara kubwa hapo uwanja wa CCM Kirumba.
Sasa najua soka lina shamra shamra zake!Lakini nikatafakari hii gharama ya safari hii na tija inayotokana na matumizi haya ya fedha ambazo ni jasho la mimi na nyinyi wengine mnao lipa kodi halali.
Ningeelewa zaidi kama tungelikuwa tunaipokea Twiga stars yetu,au Serengeti yetu au Taifa stars yetu walau na kajikombe ka Kagame au CHAN hivi....Ningefarijika.Hilo lingekuwa na maana kwa vile tungekuwa tunasherehekea mafanikio ya soka letu.....walau kwa kiwango hicho cha afrika mashariki yetu.....!
Lakini hapa mantiki iko wapi hasa?!Yaani ni kitu gani hasa tunachoadhimisha au kusherehekea hapa?!
Au kwa vile hatuna hata ndoto za kushinda hilo kombe la dunia tunajifariji kulishika tu na kuliona?!Kiasi cha mkuu wa kaya kuacha mambo mengine ya msingi na kufunga safari kabisa kwenda kuongoza umati wa majuha sisi kulistaajabia kombe la dunia tusilo ota kulishinda karne hizi za karibuni?!
Inaniuma kwa kweli pale mkuu wa kaya anapotumia kodi yangu kwa mambo kama haya yasiyo na tija kwa Taifa letu.
Lingine ni hili la umeme......
Lingine ni hili la mishahara......
Naendelea na tafakuri......