Tafadhalini sana -huu ni wakati wa wana CHADEMA kuwa na mshikamano wa chama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafadhalini sana -huu ni wakati wa wana CHADEMA kuwa na mshikamano wa chama

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nderingosha, Apr 6, 2011.

 1. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,545
  Likes Received: 1,319
  Trophy Points: 280
  • Ndio bandugu,nategemea mu wazima wa afya na kila mtu kwa nafasi yake anashiriki kwa njia moja au nyingine kuijenga nchi yetu iyojaa kila aina ya mapungu katika dhana nzima ya kimaendeleo.Leo nataka kugusia jambo la msingi sana linalohitajika katika kukiimarisha chama cha Chadema haswa ukizingatia ndicho chama kinachoelekea kuleta mapinduzi ya kweli katika jamii ya Mtanzania kifikra na kimaendeleo kwa ujumla.

  • Kuna dhana ambayo nimekuwa nikiipinga humu jukwaani(pamoja na kwamba post yangu iliondolewa na mod kabla ya kusomwa na wengi)ambayo imekuwa inahusisha watu kujadili watu/viongozi binafsi wa chadema badala ya kuwatakia mshikamano na hivyo hata kupelekea baadhi ya wachangiaji kuwaona baadhi ya viongozi wao kuwa hawafai(haswa pale wanapowahusisha na ushirikiano na chama cha ccm).Hoja hii imejitokeza sana pale ambapo kwa mfano mh.Zitto anapokuwa anajadiliwa kwa mtazamo hasi kwa kiwango kikubwa humu jukwaani pamoja na mchango wake mkubwa katika kukijenga chama cha chadema
  • Mimi binafsi hii dhana ya kujadili watu(kimajungu)badala ya issues zinazohusu maslahi ya nchi ninaipinga sana wajameni
  • Ni mategemeo yangu kuwa humu jukwaani michango inayohusisha mivurugano baina ya viongozi wa chadema na wanachama wao haitakuwapo tena badala yake tujadili issues za msingi za kimaendeleo na jinsi ya kupambana na mafisadi(majambazi)wa mali za umma kwani ndio wanaochangia kuturudisha nyuma
  • Tafadhalini tuache kuwasema vibaya viongozi wa chadema bali tuwape ushirikiano na ikiwezekana tips za jinsi ya kupambana na majambazi wa ccm au vyama vingine venye mitazamo hasi na juhudi za chadema kuikomboa nchi hii
  • Nategemea umoja huu utaimarika pia kati ya viongozi wa chadema,wabunge na wanachama wao haswa pale bungeni (na katika jamii) katika kuiweka kiti moto serikali hii ambayo kwa kiasi kikubwa imevunja matumaini ya Mtanzania kujikomboa kutokana na adui yetu mkubwa yaani: maradhi,ujinga,umaskini na ufisadi.
  • Ni katika mshikamano huu tu ndipo chadema wanaweza kuikamata dola na kuwafikisha Watanzania kwenye ndoto yao ya miaka mingi yaani: kupatikana kwa maendeleo endelevu yatakayotokana na kukua kwa pato la kila Mtanzania litakalotokana na matumizi endelevu ya raslimali zote za nchi hii na fursa sawa kwa kila Mtanzania
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Apr 6, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280


  [​IMG]
  [​IMG]
   
 3. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Waberoya, mbona tena kuna rangi za kijani na njano huho kwenye hicho kibonzo?
   
Loading...