Tafadhali sana NBS msishiriki dhambi inayopangwa na hawa watendaji na Halmashauri, naombeni muwe waamuzi wa mwisho kwenye ajira za sensa

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,364
4,055
Nimejaribu kupitia maoni mbalimbali ya wadau mbalimbali kuhusu ajira za sensa na zaidi maoni yao wengi yamejikita katika hofu walinayo juu ya mwisho mbaya unakaoenda kutokea ikiwa zoezi hili litakuja kukamilishwa na usaili utakaosimamiwa na watendaji.

Nausema ni mwisho mbaya kwa Sababu zoezi hili likifika kwao wenye sifa wataondolewa kimizengwe na wasio na sifa watabakizwa. Sifa za hao watendaji zinajulikana na hofu na mashaka ya waombaji ni kutotendewa haki.

Kila nikipitia mitandao ya kijamii na kuona namna gani watu wanavyojitoa kujipitisha kwa watendaji najiuliza, hivi haki itatendeka kweli? Kama mtu haijulikani na mtendaji na ana sifa, si ataondolewa? Je, wale wenye sifa itakuwaje?

Hayo yote yananitia hofu na kujiuliza mara mbili mbili je ni kwa nini NBS wanataka kushiriki dhambi hii kiwa wao wanaweza kuepuka?

Na zaidi ya yote kwa nini mtendaji ahusike kunisaili ikiwa NBS wanaweza kukamilisha usaili wa fomu na haki ikatendeka kuliko huko wanapotaka usaili ufanyike.

Nimalize kwa kusema kwamba kila mmoja alipoomba nafasi hizo alijaza kwa eneo analoishi hivyo haina maana wala umuhimu mtendaji kunitambua kwenye usaili wakati alishanitambua kwenye maombi.

Chonde chonde NBS msishiriki hii dhambi ya watu kutotendewa haki kwenye usaili, malizieni hili zoezi wenyewe kwa kuwa mpaka Sasa lilipofikia limefikia pazuri Sana. Msiruhusu watendaji kuhusika kwa namna yoyote ile labda wakati wa zoezi la sensa yenyewe.
 

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,364
4,055
Wanawadhaugi hawa Watendaji sasa zamu yao ya kuchinjwa imefika wanaanza kupiga mayowe.
Sasa huoni watu wanaokataa majina yasipite kwa watendaji Wana hoja za msingi? Hebu fikiria umeomba nafasi na unajuana na mtendaji na mtoto wa mtendaji kaomba , hapo ni Nani unadhani atapewa? Kwamba mtendaji aache pesa kuingia kwa mtoto wake akupe ww? Hebu fikiria Kama mtendaji ni rafiki ako mkubwa, urafiki utakuwepo Kama zamani?
 
5 Reactions
Reply
Top Bottom