Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,742
- 40,873
Najua ni rahisi kuona kuwa kwa kumuondoa Ernest Mangu Magufuli atakuwa amekurupuka; inawezekana watu wanaweza kuona kwa kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujieleza basi Rais amemnyima Mangu "haki ya asili ya kusikilizwa kabla ya kuhukumiwa".
Inawezekana wapo ambao wanaweza kuona kuwa Magu amemuonea Mangu na hivyo ikasababisha uchungu kwa baadhi ya watu. Kwani wanaweza kusema kuwa "hawajaona makosa yoyote"
Na wengine wanaweza - na nimeona dalili tayari - kuwa Kamanda Sirro amepewa u-IGP kwa sababu amekuwa karibu na Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Paul Makonda ambaye wapo wanaomuona kuwa ni kipenzi cha Rais. Wengine wanasema kwa vile "alikaa karibu na waridi, akanukia" na hivyo kuona kuwa kweli Makonda ana nguvu sana.
Katika haya yote wapo ambao wanaweza kuingiwa na jaribu lile lile ambalo inaonekana hawalikwepo la kupinga na kukataa. Katika kufanya haya yote wanaweza kabisa kusahau yale yote ambayo jeshi la polisi lilifanya dhidi yao wakati wote wa Mangu akiwa ni IGP.
Hivyo ombi langu, ni wanaotaka kupinga kuondolewa kwa Mangu wafikirie sana; wasije wakawa wanaendelea kugongelea misumari kwenye vidole vyao wenyewe...