Tafadhali naomba kujua,Mbegu za mwanaume huchukua muda gani kukomaa!

linkedIn

Senior Member
Dec 20, 2014
151
55
Habarini wakuu!!
Poleni kwa pilikapilika za wiki nzima,nina imani wengine mtakuwa bado mko kwenye mihangaiko ya kimaisha kwa ajili ya kujipatia riziki, wengine kwenye nyumba za ibada wengine safarini na wengine mmepumzika nyumbani na familia zenu.
Nisiwachoshe sana,naomba kwenda moja kwa moja kwenye mada! Wataalamu naomba mnisaidie jambo hili,mbegu za kiume hukaa muda gani ndipo zikomae ili ziweze kusababisha mimba kwa mwanamke. Endapo mwanaume anakutana na mkewe kimwili kila siku au kwa kuruka siku mojamoja yaani leo wanafanya,kesho wanapumzika,keshokutwa wanafanya siku inayofuata wanapumzika n.k,je hii inaweza ikaathiri upatikanaji wa mimba ktk zile siku za hatari!
NB: Lengo lao ni kutafuta mtoto!
Nawasilisha,
Karibuni wakuu!!
 
Ngoja niauburi majibu ya watu nitue mana midume mnakazi ya kutoka toa ovyo kumbe akati mwingine mnasababisha mwenyewe msipate watoto
 
Nenda hospitali/zahanati iliyokaribu nawe utawakuta wahusika watakujibu maswali yako yote kwa ufasaha.

Usione soo, sema naye.
 
Duh unahitaji darasa refu kuelewa ila kifupi mwanaume haihitaji kukua lini mbegu zake zinakomaa ila kwa mwanaume kinachoangaliwa ninanyojua ni kujua anatoa mbegu za kutosha, kama mbegu zina speed inayotakiwa ya kusafiri na kulifikia yai la mwanamke hayo mambo ya kukomaa huwa kwa mwanamke ndio huwa wanaangalia siku yai
 
Kwa nijuavyo mimi, mbegu za mwanaume zinakuwa ready muda wote, tatizo ni wingi, idadi na kasi. Kama huna tatizo na hayo mambo matatu, na unatafuta mtoto basi wewe tega zile siku za hatari yaani kuanzia siku ya 11 tangu kuanza kupata bleed.
 
Speed na wingi inategemea maturity ya sperm so inashauriwa kukaa siku mbili au tatu ili mbegu za kiume kuwa matured
 
Mbegu Moja Ya Kiume Kulingana Na Spermatogenesis inachukua siku 74 sawa na Miezi Miwili na na Nusu kukomaa...

Ufanyaji wako wa Kila Siku Au Unaacha Siku moja Hujafanya Unamatokeo mabaya Katika Afya Ya Mbegu maana Inaweza ikatokea Unakuwa na Low Sperm Count au Upungufu wa Mbegu Na Unakuwa na Wingi wa Maji maji au Fluid pekee

Kwahiyo Inashauriwa Kitaalam Kukaa Siku kuanzia Tatu mpk 5 Na Upate Vyakula vyenye Kuwezesha Ukuaji Bora Wa Mbegu .. Vyakula Vyenye Asili ya Mafuta kama Karanga Na Pia Vyenye Cholesterol vinasaidia Ukuaji Mzuri wa Mbegu
 
Nashukuru sana mkuu kwa ushauri mzuri!
 
Back
Top Bottom