Tafadhali Lowassa: Achana na 'active politics'; Bakia mshauri wa Taifa; furahia 80% yako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafadhali Lowassa: Achana na 'active politics'; Bakia mshauri wa Taifa; furahia 80% yako

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 18, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  [​IMG]


  Waziri Mkuu wa zamani Lowassa hahitaji siasa kwa ajili ya maisha yake wala kwa ajili ya kipato chake. Haiitaji siasa tena kuonesha kuwa anaweza kuongoza au kuwa anahitajika; haiitaji siasa kwa ajili ya jambo lolote lile. Yeye ameshatumikia chama chake na taifa kwa nafasi mbalimbali lakini sasa naamini anaweza kujikuta anaharibu hata kile kidogo alichobakia nacho. Haitaji tena kujaribu kufanya mikakati ya ku-manipulate siasa za TZ kwa sababu kama tulivyoona Arumeru Mashariki wana CCM wenzake hamuamini tena na kwa kweli walimsetup for failure.

  Ikumbukwe kuwa kama aliweza kutumia nguvu kubwa sana kumpitisha mkwewe na hata kwenda hadharani kufanya mkutano wa "kufunga ajenda" mbalimbali na bado akapoteza ni wazi kuwa lile tishio alilokuwa nalo ama ndani ya CCM au kwa nchi halipo tena na wananchi wengi - ukiondoa baadhi ya viongozi - hawaoneshi hofu juu yake au kujali sana anafanya nini.

  Ushauri wangu kwake - na kwa kweli naurudia tu - Lowassa anahitaji kuachana na siasa za Tanzania hasa hizi za mambo ya vyama vya siasa. Akiamua kuondoka CCM asiamua kujiunga na chama kingine chochote. Kwanza ni kwa sababu anatakiwa ajipambanue kuwa yuko juu ya siasa za vyama asiingie kwenye mtego wa kina Mkapa wa kupenda sana chama hadi kushindwa kufikiri vizuri. Lakini pili, naamini tayari ameshavuruga CCM vya kutosha na asiingie kwenye chama kingine nacho kikavurugika.

  Vilevile uamuzi huu hauitaji kufikiriwa sana naamini ni vizuri akaachana na siasa hizo sasa. Aamue kutangaza kuachana na ubunge na kuvua nafasi zake zote ndani ya CCM; akipenda anaweza kubakia kuwa mwanachama wa kawaida. Utakuwa ni uamuzi bora zaidi wa kisiasa ambao amewahi kuufanya. Utakuwa ni uamuzi ambao unaonesha kuwa amepima mazingira ya kisiasa. Hata hivyo ili afikie uamuzi huu kuna mambo ambayo inabidi ayakubalie kiakili, kihisia na kifikra.

  1. Ni lazima afikie mahali pa kukubali matokeo ya Richmond. Richmond ilimuumiza na kumjeruhi vibaya sana (rejea mahojiano yake na TvT kwenye youtube channel yangu). Hadi leo hii haja - come to terms - na uchunguzi ule na matokeo yake na hivyo kumekuwepo na majaribio makubwa ya kuweza kuonesha kuwa hakutendewa haki. Naamini, wakati umefika kwa EL na hapa namaanisha yeye mwenyewe siyo surrogates, friends au familia - kukubali yote yaliyojiri ili kuyaachia historia ije kuamua.

  2. Tayari ameshaonekana kuwa ni divisive figure ndani ya chama na nchi; wengine wanaweza hata kusema ni 'polarizing figure' kwa maana ya kwamba kila jina lake linapotajwa pande mbili hutokea mara moja yaani ile inayomuunga mkono na kuamini ni kiongozi mwenye uwezo zaidi na wale ambao wanaona kuwa ni sehemu ya himaya ya ufisadi iliyojikita nchini. Kama kiongozi unatakiwa kuwagawa watu kifikra zaidi na kisiasa zaidi kwa maana ya tofauti ziwe juu ya wapi unasimamia katika sera mbalimbali na siyo masuala binafsi. Naamini hawezi kurecover.

  3. Lowassa ameshakuwa ni mgogoro hata kwenye makanisa kwa sababu licha ya kugawa wananchi katika mazingira ya kisiasa amefikia mahali pa kugawa hata kanisa na waumini pasipo ulazima wowote. Tukio la Ifakara kwa kweli kabisa kwa upande mmoja lilikuwa ni tukio ambalo lilikosa hekima. Lowassa kwa mfano licha ya kupewa nafasi ya kusalimia akijua kuwa hakuwa mwalika na alienda kwa ajili ya kuabudu asingetumia nafasi ile kusema maneno zaidi ya kushukuru na kurudisha mic kwa wahusika. Matokeo yake kutumia nafasi ile kulionekana wazi kwani waumini nao walikwazika. Ninaamini ushauri kama ule angeweza kuutoa kama watu wangejua hana 'political ambitions' zaidi kuelekea 2015 kwa sababu watu wamekuwa wakichukulia kila kauli yake kwa mwanga wa kisiasa zaidi kuliko wa kuonesha kujali taifa.

  4. Lowassa tayari ameshajijengea ujiko kwa baadhi ya watu na kwa kweli kuna watu wanaweza kuapa kwa jina lake. Lakini naamini akiamua kuacha siasa hivyo anaweza akatumia muda wake mwingi kuwajenga watu hawa na kuwaongoza bila ya yeye mwenyewe kujionesha kuwa anataka kuingia tena kwenye siasa.

  5. Kama bado anataka kurudi kwenye siasa basi badala ya kuwa mbunge tu ilivyo sasa akiamua kuachana na siasa hizi atakuwa na uhuru wa kufanya mambo yake bila kuzibwa sana na mambo ya chama na kujipanga vizuri zaidi. Kwa mfano, anapozungumzia "ajira" binafsi tungependa kuona anafanya nini kuimarisha mazingira ya ajira nchini, anashirikiana vipi na wafanyabiashara wengine kusukumiza sera nzuri za ajira n.k Kwa namna hii atafuata mfano wa Rostam Aziz ambaye naye alimua kuachana na siasa hizi ili kufanya 'mambo yake'. Lowassa atakuwa na amani zaidi akiamua kuachana na hizi siasa kwani kwa kweli hazimstahili tena.

  Ushauri wangu huu niliutoa pia Rostam Aziz ambaye aliufuata vizuri na sasa hivi huko aliko anafanya mambo yake (mazuri au mabaya) kwa amani yake. Hata hivyo kinyume na RA ambaye haonekani kufanya mambo ya kuwa "statesman" Lowassa anaweza kukubalika zaidi kwani atakuwa kama kina Salim, Warioba, Sumaye n.k lakini asije kuwa kama Mkapa ambaye ameshindwa kabisa kuachana na "active politics' kiasi cha kuanza kujiabisha majukwaani!

  Lowassa na CDM
  Endapo Lowassa ataamua kuachana na siasa za CCM lakini bado anafikiria kuingia kwenye siasa za vyama ushauri wangu ni kuwa ASIAMUE kujiunga na CDM kwanni ni rahisi kuona kuwa ataleta mgogoro mwingine usio wa lazima na kwa kweli itakuwa ni ukosefu wa hekima, kupima, na maono kama kuna viongozi wa CDM ambao wanafikiria kuna jambo lolote "zuri" litakuja kwa CDM kwa Lowassa kujiunga nao sasa. Inawezekana baada ya muda Lowassa anaweza kujiunga CDM lakini naamini kujiunga huko ni lazima kuwe kutokana na yeye kukubali ajenda YOTE ya CDM na ajioneshe ameikubali! Hili ni sharti ambalo ningependa pia nione lina linatumika kwa wale wana CCM wengine ambao wameanza kujivua 'gamba'. Isije kuwa ni rahisi watu wakabadilisha vyama vyao lakini kumbe fikra zao ziko kule kule!

  Viongozi wa CDM wataonekana kuwa hawana hekima kama watakumbatia kila "mtu" anayetoka CCM katika mazingira ya mgogoro na kuonekana ni bahati kwa CDM. CDM inahitaji kuweka masharti na kanuni za uwapokea baadhi ya watu kwa sababu CDM ni chama cha hiari. Haitoshi tu kusema kuwa "natoka CCM, nimeamua kujiunga CDM" halafu watu wanafurahia na kusema "karibu"!

  Remember hii ni vita!! na askari au afisa wa intelligensia wa adui yako hawezi tu kudefect halafu ukampokea na kumpa cheo na nafasi nyeti! CDM wakisahau tu kuwa hii ni vita basi watajikuta wanapokea majasuri, wapiganaji, na hata majenerali wa uongo. Siyo kila anayesama "nahama" anamaanisha amebadilisha na fikra zake!! Lakini Lowassa akiamua kujiunga CDM sasa hivi na CDM wakampokea kwa mikono miwili ni kwa maslahi ya kila anayetaka mabadiliko nchini kuipinga CDM na maamuzi yake hayo! Kama watu wameshapoteza matumaini na CCM, watu wasilazimishwe kuchagua CDM ama dhamira zao kwani naamini kwa wakati huu - sijui mbeleni - CDM ni tumaini la mwisho la mabadiliko ya kweli nchini na wakichezea mtaji huu wa wananchi, watakapokuja wao kukataliwa wasije kusema 'hawakupendwa" au "wamehujumiwa!

  Hivi sasa Lowassa aachie siasa, awe mshauri tu, na kufurahia 80% yake!!
   
 2. don-oba

  don-oba JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 1,384
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kunawakati huwa nafikiria hivi ni kwanini huyu jamaa anatumia jeuri ya pesa kutafuta nafasi ya uongozi?. Kwasababu kama ni pesa anayo! Anataka kutuambia ana uchungu sana na nchi hii?, hivi kweli ana uchungu sana na vijana wa nchi hii?. No.
   
 3. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji umenena vyema,CDM wanatakiwa wawe makini sana mana wanaweza kupokea mbwa mwitu waliovaa ngozi za kondoo,mana inawezekana wakapokea watu wenye nia njema au wenye kutimiza malengo yao(inawezekana watakuja/wamekuja kujiunga chadema ili wapate vyeo ili ikikaribia 2015 wawe mzigo ndani ya CDM,either kujiondoa tena na kufanya kampeni chafu dhidi ya CDM).
  Ila ushauri wako unafaa kuzingatiwa na pande zote mbili
   
 4. J

  John W. Mlacha Verified User

  #4
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  ngoja ni i copy nikai paste kwenye facebook yake
   
 5. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,269
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwanakijiji hizi makala za kuzileta usiku usiku kwa saa za Afrika Mashariki nadhani siyo bure, huu uvumi wa Lowasa kuhama CMM sasa ni dhahiri kwa kutokana na hii makala yako nimeanza kucconect dots.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,520
  Likes Received: 81,875
  Trophy Points: 280
  Anataka kuzikusanya zaidi ili awe bilionea mwenye mabilioni mengi nchini kuliko hata akina Rostam, Jitu, Manji na Subhash.
   
 7. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #7
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Ni ndefu ngoja nilale najua umeitoa kwenye Raia Mwema
  EL cheo alichobakiza ni Urais aachane nao ajijengee heshima akilogwa akajitoa na kuanzisha Chama chake Kaukalia
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Platinum analysis!!!

  His advisory role to politics will make him beyond politicians wetu wa kawaida... Actually his legacy will live longer and stronger than getting into cheap politics that he is involved now!!
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  anaweza kuheshimika zaidi bila kuwa rais!!!
   
 10. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Vita ya Fallujah wameshinda, sasa mkakati mwingine ni SURGE. Hii ni pamoja na kukusanya kila kitu kama kokoro linapotupwa ziwa Viktoria na wavuvi, au vipi?
   
 11. n

  nkungu Member

  #11
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Power corrupts!!!
   
 12. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #12
  Apr 18, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180
  Kweli bana,Unaonaje heshima aliyonayo Warioba na Salim
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Swali kubwa ni je ni upi uamuzi rahisi kwa Lowassa kufanya?
   
 14. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #14
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  "To make his legacy alive".
   
 15. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #15
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Naamini kabisa Mh. Lowassa ana washauri wake. Je wanamshauri ndivyo sivyo?
   
 16. mujusi

  mujusi JF-Expert Member

  #16
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 237
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mwanakijiji hayo maoni yako. Mbona wengine huwaambii waache Active politics? kwani mwisho au ukomo wa kutoshiriki kwenye siasa za Tanzania ni upi? kashfa , utajiri, tuhuma, uzee? kama vigezo ni hivyo mbona wengi wako kwenye category hiyo? Yeye ana haki kikatiba kama wengine kushiriki katika mambo yote anayoweza kushiriki ili mradi havunji sheria. Wananchi na wanasiasa wengine ndio wakuamua. Usimuhukumu mtu kabla ya kesi yake kusikilizwa.
   
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #17
  Apr 18, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Imani yangu ni kwamba Lowassa anaweza kuondoka CCM, lakini siyo kujiunga na chama chochote cha siasa tena.
   
 18. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #18
  Apr 18, 2012
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Uamuzi rahisi ni agombee urais mwaka 2015 as an independent candidate.
   
 19. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #19
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Kwa mtazamo wangu, EL anatakiwa kusimama mbele ya umma na kueleza ukweli kuhusu Richmond, akiri alipokosea na kutuomba radhi wa tz. Akubali kwamba aliwajibika kwa umma na aache kuendelea kupokea 80% kutoka kwenye kodi zetu maana hastahili. Hiyo itatupa changamoto ya kuamua hatma yake. Kumsamehe au ....!? Halafu aachane na siasa kisha abaki kama alivyokuwa Kawawa (rip). Awe mshauri tu na sio mshawishi. Hapo ataishi kwa amani na huenda akapata maisha marefu!
   
 20. p

  plawala JF-Expert Member

  #20
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji

  Umesahau kwamba EL alitajwa na chadema kwenye ile listi ya watu 11?

  Hawezi kwenda chadema maana hawawezi kumpokea,labda ajisafishe kuhusika kwake na kujiondoa kwenye listi
   
Loading...