Tafadhali kijana Nape Nnauye, hatujasahau kwani hata mwaka bado na vidonda havijapona !

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757
Nape unadai Kikwete na familia yake wanachafuliwa kwa kuhusishwa na hao watu kwani nyoka anajivua magamba. Kijana hizi picha zinadanganya ? Kumbuka Wapemba hutambuana kwa vilemba na ndege wa rangi moja huruka pamoja.

kikwete_rostam1.jpg

kikwete_rostam2.jpg

rostam_election.jpg

Hapa anaonekana Kikwete akimnadi Rostamu Igunga kwa kudai ni mtu safi ila anasingiziwa!


wtcoj.jpg

Hapa Kikwete anaonekana akimnadi Lowasaa huko Monduli na kudai hana doa na ni mchapakazi ila anasingiziwa tu !

salma_chenge.jpg

Hayo yakiendelea Salma Kikwete naye akajitosa uwanjani kumnadi Chenge huko Bariadi kwa kudai ni mtu safi ila anaonewa wivu !

Na katika hali ya kuongezea chumvi kwenye kidonda cha Watanzania, Kikwete akamnadi hadi Mramba Rombo akisema, "Huyu kwa maneno ya mjini, ni Mzee Kijana, kwani ni mwenye mawazo mapya yenye manufaa wakati wote…siyo wale wazee ambao wakichoka la mbele linawekwa nyuma, la nyuma linawekwa mbele. Huyu ubongo wake unajadidika (renewal), ni chimbuko la maarifa mapya".

Aamramba5.jpg
Wakati JK anamnadi, Mramba alikuwa akikabiliwa na kesi ya ufisadi mahakamani iliyofunguliwa na serikali.

Huo msitari unaowatenganisha Kikwete na hao washikaji wake umechorwa lini na nani na kwa misingi ipi ? Hapana, labda mtafanikiwa kuwazuga hao hao mliozoea kuwazuga, lakini mjue wengi wanaanza kuzinduka.

 
Nape anadhani wenzie hawakuwa na taarifa za ufisadi mpaka juzi tu walipoenda Dodoma!

Huwezi kujivua magamba kwa kuwapa mafisadi siku 90 eti wajiuzulu? kama ni kuonyesha zero tolerance on UFISADI walitakiwa kuwavua uongozi na kuwaambia wajiuzulu ubunge kinyume chake wawafukuze uanachama ili wapoteze ubunge! Huwezi kusema ni Fisadi hatakiwi kwenye uongozi wa Chama lakini anafaa kuongoza kwenye bunge la taifa!

Kama tunavyoamini siku zote "Kwa wana-ccm; ccm ni bora zaidi kuliko taifa"! Kibovu kwenye chama lakini kwenye taifa kinafaa tu!
 
Natamani magazeti ya kesho yawe na hizi picha kwenye kurasa za mbele na magamba ya kobe wa-comment anything on them!:smile-big:
 
Hizi picha ni Lulu!
Nimeshazisevu tayari kwa file langu, nahofia zinaweza kupotezwa muda wowote!
Ushahidi live huu!
 
hatukukutana barabarani.jpg

Tafadhali bwana mdogo Nape Nnauye, hawa wameanzia mbali - hawakukutana tu barabarani ! They share a lot in common na wewe unatumiwa tu bila kujua na haya yote ni maigizo tu - kaa chonjo !
 
Back
Top Bottom