Tafadhali Jezi zenu Maalum za Unbeaten Record ya 50 mlizopanga Kuzivaa leo msizichome Moto Usiku huu Mbeya

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,864
Ama kweli Binadamu tunapanga lakini na Mwenyezi Mungu nae pia anapanga lake / yake vile vile.

Kudadadeki Taarifa ikufikie popote pale ulipo kuwa Usiku huu kwa Aibu waliyoipata kwa Kufungwa na Ihefu FC huku kwa Kujiamini kabisa kuwa Unbeaten Record yao itaendelea wanapanga Kuchoma Moto Jezi zao Maalum ambazo zimeenda na Kenta ya Mdau wa Yanga SC na mwana CCM.

Kilichoandaliwa leo kilikuwa ni Yanga SC ishinde / ikishinda basi pale pale Uwanjani Highland Estate Mkoani Mbarali Jezi hizo Maalum zitolewe katika hilo Gari Kenta ili baadhi zitolewe kwa Mashabiki wa VIP na zingine GSM waanze Kuziuza na Kupiga Pesa kama Kawaida yao.

Sababu Kuu ya kutaka Kuchoma Moto Jezi hizo ni kwamba Lengo halijafanikiwa, Hasara imepatikana Kuzitengeneza Kwani ni Maalum lakini ni Kuogopa Kuchekwa na Kuonekana Washamba na Wapumbavu na Watani zao Wakubwa Simba SC.

Yanga SC mtajitahidi kadri muwezavyo Kuficha Siri zenu ila kwa Mtandao mkubwa GENTAMYCINE nilionao tena katika Uongozi wenu, Makomandoo wakiongozwa na Mratibu wa Timu Mohammed Binda, Benchi lenu la Ufundi na kwa Wachezaji Waandamizi kamwe hamtoweza Kunificha lolote na nitapata tu Taarifa zetu Nyeti kama hii ya kutaka Kuchoma hizo Jezi zenu Maalum za Kutanbia Unbeaten Record yenu ya 50 kama ingefikia leo ambayo Ihefu FC wameivunja.
 
Yanga kama wata amua kuandaa jezi Kwa ajili ya un beaten sio mbaya waweke ata iyo 49 bado yakibabe na ita uza sana sokoni ni wazo zuri kibiashara.
Shida inakuja umeshandaa jezi zimeandikwa unbeaten 50 halafu uchapishe tena.
Hapo wana mawazo bado klabu bingwa ya timu zilizoshindwa inawasubiri
 
Hapo kwenye kuogopa kuchekwa na simba hapo sahau! Simba haina tulishaisahau kitambo sana
Yanga akicheza na Simba ndiyo amecheza klabu bingwa Afrika ndiyo maana akiifunga huwa anasheherekea mwezi mzima.
Yanga ni timu ya mikoani na haina hadhi ya kucheza klabu bingwa Afrika. Isipoiwaza Simba, Azam, ihefu, mbeya city, coastal union n.k iwaze nini?
 
Ongea yote lakini hilo li team lenu bovu hakuna anaelifikiria!
 
Yanga ni timu nzuri wameifunga Al Hilal wakiingia makundi kwenye timu zilizoshindwa.
Una muda gani umecheza ligi kuu? Unajisifia kuifunga Ihefu, mbeya city, Geita na Coastal Union kweli?
Tunapoelekea Simba itakuwa timu kubwa sana Afrika. Nyie endeleeni kukimbizana na ihefu tu mtakuwa mkiingia club bingwa mnaishia kucheza mechi moja ya kurudiana mnapigwa.
 
Yanga akicheza na Simba ndiyo amecheza klabu bingwa Afrika ndiyo maana akiifunga huwa anasheherekea mwezi mzima.
Yanga ni timu ya mikoani na haina hadhi ya kucheza klabu bingwa Afrika. Isipoiwaza Simba, Azam, ihefu, mbeya city, coastal union n.k iwaze nini?
Simba amekua akitandikwa na Yanga ata kabla ya kuanzishwa ligi kuu mwaka 1965. Tangu wanashindana Ilala cup kabla ya uhuru.
 
Yanga kama wata amua kuandaa jezi Kwa ajili ya un beaten sio mbaya waweke ata iyo 49 bado yakibabe na ita uza sana sokoni ni wazo zuri kibiashara.
Waweke yenyw logo ya mwiko nyuma
Tena ule uliotumika kupakuwa mihogo kule mbarali
 
Simba amekua akitandikwa na Yanga ata kabla ya kuanzishwa ligi kuu mwaka 1965. Tangu wanashindana Ilala cup kabla ya uhuru.
Kinachowaponza Yanga hata kuonekana ni timu ya kawaida sana huko kwenye timu za Club bingwa Africa ni kukamia soka la ndani.
Yanga akicheza na Simba, ihefu na Mbeya City anajiona ni timu bora sana na ndiyo amemaliza mpira.
Tumecheza sana soka la ndani na halina hela mpk Yanga kipindi fulani ilitembeza bakuli. Tutangaze soka letu Afrika kupitia club bingwa Africa. Tuache kuwaza soka la ndani hapa maana halina hela.
Simba au yanga ikicheza ndiyo banda umiza wanaweka viingilio lkn akicheza Azam siui Ihefu na dodoma jiji banda umiza unaangalia bure. Huoni utofauti uliopo ndugu? Shituka
 
Yanga ni timu nzuri wameifunga Al Hilal wakiingia makundi kwenye timu zilizoshindwa.
Una muda gani umecheza ligi kuu? Unajisifia kuifunga Ihefu, mbeya city, Geita na Coastal Union kweli?
Tunapoelekea Simba itakuwa timu kubwa sana Afrika. Nyie endeleeni kukimbizana na ihefu tu mtakuwa mkiingia club bingwa mnaishia kucheza mechi moja ya kurudiana mnapigwa.

Yanga ni timu nzuri wameifunga Al Hilal wakiingia makundi kwenye timu zilizoshindwa.
Una muda gani umecheza ligi kuu? Unajisifia kuifunga Ihefu, mbeya city, Geita na Coastal Union kweli?
Tunapoelekea Simba itakuwa timu kubwa sana Afrika. Nyie endeleeni kukimbizana na ihefu tu mtakuwa mkiingia club bingwa mnaishia kucheza mechi moja ya kurudiana mnapigwa.
Maneno mengi ni dalili ya udhaifu.
Timu lenu bovu
 
Maneno mengi ni dalili ya udhaifu.
Timu lenu bovu
Kwenye timu bora Afrika Yanga na Simba ipi ni timu bora?
Kufungwa club bingwa wala hamjaumia ila kufungwa na ihefu meumia sana?
Mtasafiri sana na basi mpk mkome huku mkiangalia Simba anapanda ndege anaenda kucheza Misri, Senegal, Sudan n.k
 
Yanga akicheza na Simba ndiyo amecheza klabu bingwa Afrika ndiyo maana akiifunga huwa anasheherekea mwezi mzima.
Yanga ni timu ya mikoani na haina hadhi ya kucheza klabu bingwa Afrika. Isipoiwaza Simba, Azam, ihefu, mbeya city, coastal union n.k iwaze nini?
Hapo kwenye " kama team ya mkoani" ulimaanisha Simba na wengineo ni wa wilayani au!!!?? Au hujui kama Dar nao ni mkoa pia!!!???
 
Back
Top Bottom