Tafadhali Anne Makinda jihadhari kwani Pius Msekwa si saizi yako. Msekwa katumia usomi kusema akina Halima Mdee wamefutwa Ubunge

Mama Anne Makinda,

Nimeona leo mahali unasema vyombo vya habari vimuache Pius Msekwa kwani kalitumikia taifa kwa muda mrefu na sasa ni mstaafu.

Mama Makinda, Pius Msekwa hajastaafu kutumia haki yake ya kutoa maoni kama Katiba inavyomruhusu.

Tatizo siyo Msekwa, tatizo ni wewe hutaki Msekwa aseme kwamba akina Halima Mdee si wabunge tena tangu walipovuliwa uanachama.

Msekwa kanukuu ibara ya 71(1)(e) sasa wewe ulitaka awe kipofu kwa ibara hiyo.

Sasa mama Makinda ngoja nikufundishe mambo matatu inayoelekea huyajui.

Jambo la kwanza ni kwamba Pius Msekwa ndiye mtu pekee aliyebaki hai aliyeshiriki kamati ya kuiunda Katiba hii mwaka 1977.

Kumbuka Mwenyekiti wa kamati hiyo ni alikuwa hayati Thabit Kombo na katibu akawa ni huyu Msekwa.

Wewe ulikuwa wapi wakati huo maana historia haikutaji.

Hivyo Pius Msekwa ni mtunzi wa Katiba yetu bila kujali ni mbovu au nzuri.

Waandishi wanamfuata kwa sababu ni mtungaji wa hiyi Katiba hawakufuati wewe uliyepata uspika kwa kigezo cha Samwel Sitta kukosa jinsia ya Kike mwaka 2010.

Jambo la pili ni kwamba Pius Msekwa ndiye kiongozi pekee ndani ya CCM kuandika vitabu vingi na vinasomwa duniani kote.

Ndiye msomi pekee aliyeandika mengi kuhusu Bunge. Wewe huna article hata ya page moja kwenye gazeti lolote.

Jambo la tatu ni kwamba wiki juzi wakati Bunge hili linazinduliwa Pius Msekwa alialikwa kwenye semina ya wabunge na akatoa lecture nzuri.

Katika semina hiyo Spika Job Ndugai kawaambia kwamba wasiishie kumsikiliza Msekwa kwenye semina ile tu bali wachimbue vitabu vyake vilivyojazana kwenye library ya Bunge.

Jambo la nne ni kwamba kama unataka, japo huwezi, mwambie Pius Msekwa aache kuandika makala zake za "The Current Affairs" kila Alhamsi kwenye gazeti la Daily News.

Serekali inamtumia kila Alhamis kwenye Daily News halafu leo EATV wamemhoji unapiga kelele.

Hivyo kama wewe uliamua kuandika historia ya kukaa kimya basi acha dunia ya wasomi inayomheshimu Msekwa tumheshimu.

Msekwa ndiye mtu pekee ndani ya CCM anayeweza kuongea na wapinzani wakajibizana naye.

Cha muhimu ishauri CCM ipike vijana ma genious kama Nyerere alivyowapika hawa akina Msekwa na siyo hawa wa sasa hivi ambao wakiamka asubuhi wanatafuta tusifie lipi.
Mama anamtetea mzee kwasabu anajua hizi zama tulizonazo saahiv...hata mi namuunga mkono au umesahau habar za kuambiwa mstaafu anawashwa washwa? Msekwa anatakiwa atulie alee wajukuu sahiv maana hajui kilichomo ndan ya serikal kwasasa
 
Sijajua huo mlinganisho una maana gani?
Chadema ni imani. Chama kipo kwenye mioyo ya watu. Chadema imevuka hatua zote za kuuwawa na wafilisti wenye mamlaka. Viongozi watafungwa, wanachama watafungwa na kupotezwa. Lakini chama kitasimama imara. Chadema imevuka vikwazo vyote vigumu. Chadema ni mabadilko na uhuru wa kweli

Ndugai mmoja ni sawa na headless chicken
 
Hiyo sawa na mapenzi ya timu ya mpira. Maana wachezaji wanaondoka na kuja wapya viongozi wanabadilishwa yani timu inaweza kubadilika kila kitu likabaki jina tu ila bado mtu anaendelea kushabikia.
 
Hiyo sawa na mapenzi ya timu ya mpira. Maana wachezaji wanaondoka na kuja wapya viongozi wanabadilishwa yani timu inaweza kubadilika kila kitu likabaki jina tu ila bado mtu anaendelea kushabikia.
2017, CCM ilimfukuza Sophia Simba (akiwa mwenyekiti wa UWT na mbunge wa VM) kwa tuhuma zikiwepo kumuunga mkono Edward Lowassa (aliyehamia CCM wakati huo). Lakini Ndugai hakusimama kusema CCM hii ya Magufuli inawanyanyasa wanawake. Ikawasamehe wanaume na kumpa adhabu mwanamke.
 
Na ndiyo maana mie huwa naona vyama vya upinzani ni hovyo kushinda huyo ccm,maana kwa hayo maelezo yako ni kwamba Chadema kaiga kwa ccm na kazidisha kwa kuwatukana hao wanawake.
 
Dah! Umeandika vuzuri sana. Yaani kwa ufupi ila point tupu. Mtu kaamua yeye kukaa kimya anataka na wengine wanyamaze.
 
Tatizo ni kwamba leo Msekwa ataonekana mtu wa maana kwa sababu kaongea jambo lenye kuwafurahisha watu fulani ila Msekwa huyohuyo siku nyengine akiongea jambo lisilowafurahisha hata kama ndio ukweli basi ataonekana ni hovyo.

Tuache hii tabia.

Kwani hao wanaomuona siyo wamaana siku akiwa sifia si watamuona wamaana pia, mtu anasifiwa akitenda mema akikosea anasema kuna tatizo gani hapo
 
Kwani hao wanaomuona siyo wamaana siku akiwa sifia si watamuona wamaana pia, mtu anasifiwa akitenda mema akikosea anasema kuna tatizo gani hapo
Yani wewe ukiongea jambo ambalo mimi linanifurahisha basi nakusifia kwa sababu ulichoongea ndio nachotaka kusikia,ila siku ukiongea jambo ambalo halinifurahishi hata kama ni jambo la kweli basi nakutukana au nakuona ni mjinga na ulichoongea ni ujinga tu,kwanini? sababu ulichoongea sio nachotaka kukisikia.

Je,hapo mkuu hauoni tatizo?
 
Mkuu hapa ndipo wengi mnapokosea.
Mtu mzima hata kama kakosea kwa maoni yako, bado anastahili lugha ya staha siyo kama hii uliyo tumia hapo juu.

Unapojisifu na kujipa hadhi ya mwanajumuiya ya wasomi basi tumia hekima na busara za kisomi katika mijadala ya kisomi.

Umejenga hoja nyingi nzuri sana kutetea maoni yako lakini lugha hii ya vijiweni imekuangusha sana.
Humu hatuangalii lugha, tunaangalia hoja. Big up mtoa mada
 
Back
Top Bottom