Tafadhali Anne Makinda jihadhari kwani Pius Msekwa si saizi yako. Msekwa katumia usomi kusema akina Halima Mdee wamefutwa Ubunge

When ceases to be a member!

Lugha ya Sheria ni ngumu sana ndiyo maana tunasumbuliwa mahakamani. Ibara ya 71 (1) (e) ina sema:
"(e) ikiwa Mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa
kuwa Mbunge"
tunaweza kusumbuana hapo tu sababu hawa wajaacha bali wamefukuzwa bila kupewa haki ya kusikilizwa 😂 😂
 
Yani wewe ukiongea jambo ambalo mimi linanifurahisha basi nakusifia kwa sababu ulichoongea ndio nachotaka kusikia,ila siku ukiongea jambo ambalo halinifurahishi hata kama ni jambo la kweli basi nakutukana au nakuona ni mjinga na ulichoongea ni ujinga tu,kwanini? sababu ulichoongea sio nachotaka kukisikia.

Je,hapo mkuu hauoni tatizo?
Labda nikuulize, Msekwa kaongea anavyoona yeye kwa utashi wake au katafsiri sheria inavyotaka? Maana naona kama unataka kupotosha.
 
Hawawezi kutokea hao. Mark my word!
Ile siku bwana mdogo Ndugai anamuapisha Polepole lakini anaongelea mambo ya Chadema na kusema kuna "unyanyasaji wa kijinsia" akiwatumia akina Halima Mdee kama Mfano. Halima anafanya press yake na kusema Chadema hakuna mfumo dume kama inavyoelezwa, maana wao wamekuwa viongozi huko. Ndugai anajionaje?
 
Anakuona Kama paka mapepe
 
Mama Anne Makinda,

Nimeona leo mahali unasema vyombo vya habari vimuache Pius Msekwa kwani kalitumikia taifa kwa muda mrefu na sasa ni mstaafu.

Mama Makinda, Pius Msekwa hajastaafu kutumia haki yake ya kutoa maoni kama Katiba inavyomruhusu.

Tatizo siyo Msekwa, tatizo ni wewe hutaki Msekwa aseme kwamba akina Halima Mdee si wabunge tena tangu walipovuliwa uanachama.

Msekwa kanukuu ibara ya 71(1)(e) sasa wewe ulitaka awe kipofu kwa ibara hiyo.

Sasa mama Makinda ngoja nikufundishe mambo matatu inayoelekea huyajui.

Jambo la kwanza ni kwamba Pius Msekwa ndiye mtu pekee aliyebaki hai aliyeshiriki kamati ya kuiunda Katiba hii mwaka 1977.

Kumbuka Mwenyekiti wa kamati hiyo ni alikuwa hayati Thabit Kombo na katibu akawa ni huyu Msekwa.

Wewe ulikuwa wapi wakati huo maana historia haikutaji.

Hivyo Pius Msekwa ni mtunzi wa Katiba yetu bila kujali ni mbovu au nzuri.

Waandishi wanamfuata kwa sababu ni mtungaji wa hiyi Katiba hawakufuati wewe uliyepata uspika kwa kigezo cha Samwel Sitta kukosa jinsia ya Kike mwaka 2010.

Jambo la pili ni kwamba Pius Msekwa ndiye kiongozi pekee ndani ya CCM kuandika vitabu vingi na vinasomwa duniani kote.

Ndiye msomi pekee aliyeandika mengi kuhusu Bunge. Wewe huna article hata ya page moja kwenye gazeti lolote.

Jambo la tatu ni kwamba wiki juzi wakati Bunge hili linazinduliwa Pius Msekwa alialikwa kwenye semina ya wabunge na akatoa lecture nzuri.

Katika semina hiyo Spika Job Ndugai kawaambia kwamba wasiishie kumsikiliza Msekwa kwenye semina ile tu bali wachimbue vitabu vyake vilivyojazana kwenye library ya Bunge.

Jambo la nne ni kwamba kama unataka, japo huwezi, mwambie Pius Msekwa aache kuandika makala zake za "The Current Affairs" kila Alhamsi kwenye gazeti la Daily News.

Serekali inamtumia kila Alhamis kwenye Daily News halafu leo EATV wamemhoji unapiga kelele.

Hivyo kama wewe uliamua kuandika historia ya kukaa kimya basi acha dunia ya wasomi inayomheshimu Msekwa tumheshimu.

Msekwa ndiye mtu pekee ndani ya CCM anayeweza kuongea na wapinzani wakajibizana naye.

Cha muhimu ishauri CCM ipike vijana ma genious kama Nyerere alivyowapika hawa akina Msekwa na siyo hawa wa sasa hivi ambao wakiamka asubuhi wanatafuta tusifie lipi.
Mzee Msekwa kapitwa na wakati, hajui hata kama kuna taratibu za bunge zimebadilishwa, ni miaka mingi sana imepita kwa mzee wetu Msekwa aendelee tu kucheza na wajukuu,hizi siasa za sasa awaachie vijana tumechoka kumsikia yeye tu ,kuanzia miaka ya 60 awe ni YEYE tu muongeaji na mjuaji wa siasa, akumbuke walikuwepo akina mzee Kingunge,wakafanya siasa wee mwishowe wakajipumzikia baada ya kuona zinaenda tofauti na walivyokuwa wanazifanya.
 
Labda nikuulize, Msekwa kaongea anavyoona yeye kwa utashi wake au katafsiri sheria inavyotaka? Maana naona kama unataka kupotosha.
Nasema hivi kuna siku huyohuyo Msekwa anaweza kuja kutafsiri sheria hizohizo lakini wakati huo hizo sheria zinakuwa zinawagusa watu fulani basi hapo ndipo Msekwa ataonekana hana maana ni miccm tu kama kawaida yao hapo hawatojali kwamba alichoongea ndivyo sheria inavyosema,na hapo ndipo naposema watu hutaka kusikia wanachokipenda.
 
Ccm ya kusifia sifia tu

Hakuna vijana wenye kutoa tafakuri

Sikiliza wabunge wao akina mwanaFA wakiongea

Sijui wameambia usiposifia utapokonywa ubunge!!!?

Watu wa Kariba ya msekwa hawapo tena

Saivi ni kusifia na kutegemea polisiccm kuwabeba
 
Mama Anne Makinda,

Nimeona leo mahali unasema vyombo vya habari vimuache Pius Msekwa kwani kalitumikia taifa kwa muda mrefu na sasa ni mstaafu.

Mama Makinda, Pius Msekwa hajastaafu kutumia haki yake ya kutoa maoni kama Katiba inavyomruhusu.

Tatizo siyo Msekwa, tatizo ni wewe hutaki Msekwa aseme kwamba akina Halima Mdee si wabunge tena tangu walipovuliwa uanachama.

Msekwa kanukuu ibara ya 71(1)(e) sasa wewe ulitaka awe kipofu kwa ibara hiyo.

Sasa mama Makinda ngoja nikufundishe mambo matatu inayoelekea huyajui.

Jambo la kwanza ni kwamba Pius Msekwa ndiye mtu pekee aliyebaki hai aliyeshiriki kamati ya kuiunda Katiba hii mwaka 1977.

Kumbuka Mwenyekiti wa kamati hiyo ni alikuwa hayati Thabit Kombo na katibu akawa ni huyu Msekwa.

Wewe ulikuwa wapi wakati huo maana historia haikutaji.

Hivyo Pius Msekwa ni mtunzi wa Katiba yetu bila kujali ni mbovu au nzuri.

Waandishi wanamfuata kwa sababu ni mtungaji wa hiyi Katiba hawakufuati wewe uliyepata uspika kwa kigezo cha Samwel Sitta kukosa jinsia ya Kike mwaka 2010.

Jambo la pili ni kwamba Pius Msekwa ndiye kiongozi pekee ndani ya CCM kuandika vitabu vingi na vinasomwa duniani kote.

Ndiye msomi pekee aliyeandika mengi kuhusu Bunge. Wewe huna article hata ya page moja kwenye gazeti lolote.

Jambo la tatu ni kwamba wiki juzi wakati Bunge hili linazinduliwa Pius Msekwa alialikwa kwenye semina ya wabunge na akatoa lecture nzuri.

Katika semina hiyo Spika Job Ndugai kawaambia kwamba wasiishie kumsikiliza Msekwa kwenye semina ile tu bali wachimbue vitabu vyake vilivyojazana kwenye library ya Bunge.

Jambo la nne ni kwamba kama unataka, japo huwezi, mwambie Pius Msekwa aache kuandika makala zake za "The Current Affairs" kila Alhamsi kwenye gazeti la Daily News.

Serekali inamtumia kila Alhamis kwenye Daily News halafu leo EATV wamemhoji unapiga kelele.

Hivyo kama wewe uliamua kuandika historia ya kukaa kimya basi acha dunia ya wasomi inayomheshimu Msekwa tumheshimu.

Msekwa ndiye mtu pekee ndani ya CCM anayeweza kuongea na wapinzani wakajibizana naye.

Cha muhimu ishauri CCM ipike vijana ma genious kama Nyerere alivyowapika hawa akina Msekwa na siyo hawa wa sasa hivi ambao wakiamka asubuhi wanatafuta tusifie lipi.
Huu ni ukweli na uwazi....na kama CCM kweli wanamapenzi na Nchi hii, basi wawatumie, Mzee Msekwa, Mzee Warioba na Mzee Butiku....watawavushaji salama kabisa ktk suala hili la Katiba.

Vinginevyo sijui....maana watu wengine wanaitwa vilaza...Guinea ipo Africa hii hii.....
 
Anaebisha umahiri na hitimisho la msekwa kiakili ni mende kama mende wengine. Universal is universisal period.
 
Back
Top Bottom