Tafadhali akina dada hawaruhusiwi kuingia hapa (tohara kwa wanaume) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafadhali akina dada hawaruhusiwi kuingia hapa (tohara kwa wanaume)

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Feb 8, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Tohara (Kukata govi) Suna


  Tohara (kutoka Kiarabu طهارة tahara - safi, tahiri) ni upasuaji mdogo wa kukata na kuondoa govi, yaani ngozi inayofunika kichwa cha uume.

  Wakati mwingine ukeketaji huitwa "tohara ya mwanamke".

  Inaweza kufanyika katika umri wowote na kwa sababu za kiutamaduni, za kidini au za kiganga. Mara nyingi desturi za kutahiri zinachanganya sababu za kidini na kiutamaduni. Kwa mfano, Waislamu wa Misri huamini ya kwamba wanatahiri watoto wao

  kama amri ya kidini lakini Wakristo Wakopti wa nchi hiyo hutahiri watoto vilevile. Ukweli ni kwamba tohara inajulikana ilikuwa desturi ya Wamisri tangu kale.
  Tohara inafanyika hasa mara baada ya kuzaliwa kwa mtoto au wakati wa kubalehe.
  Kufuatana na Shirika la Afya Duniani takriban 30% za wanaume wote duniani wametahiriwa, wengi wao wakiwa Waislamu.
  [​IMG]
  Tohara ya Wanaume.Baada ya upasuaji.​

  Katika makabila mengi ya Afrika mvulana anatahiriwa ili kuingizwa katika kundi la wanaume wanaopaswa kuwajibika katika jamii.

  Desturi hiyohiyo inaonekana pia kati ya watu wa Pasifiki k.mf. Wapolinesia wa Samoa, Tonga na Niue, vilevile kati ya Wamelanesia wa Fiji na Vanuatu.
  Wakazi asilia wa Australia huwa pia na tohara ya wavulana.  Uyahudi

  Kwa Wayahudi tohara ni ishara ya agano lao na Mungu na inapaswa kufanyika siku ya nane baada ya mtoto wa kiume kuzaliwa ili kumwingiza mapema katika taifa la Mungu.
  Kufuatana na habari za Biblia Ibrahimu alikuwa mtu wa kwanza aliyepokea amri ya kutahiriwa kama alama ya agano (Mwanzo 17).

  Ukristo


  Yesu mwenyewe alitahiriwa siku ya nane kama Wayahudi wote wa kiume. Tohara ya Yesu inakumbukwa kwa sikukuu maalumu katika makanisa mengi duniani hasa Waorthodoksi.

  Agano Jipya inaonyesha jinsi gani suala la tohara lilikuwa motomoto mwanzoni mwa Kanisa, wakati Wakristo wengi walitoka katika Uyahudi.

  Kufuatana na kitabu cha Matendo ya Mitume (15:23-29) Mtaguso wa Mitume uliofanyika Yerusalemu uliamua Wakristo kutoka mataifa wasilazimishwe kutahiriwa.

  Hasa Mtume Paulo alisisitiza kwamba jambo hilo si muhimu tena, cha maana ni kuwa watu wapya kwa imani.
  "Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya" (Gal 6:15).
  "Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili" (Fil 3:3).
  Hata hivyo Wakopti wa Misri na Ethiopia wameendelea kutahiri watoto wao.

  Uislamu


  Katika Uislamu tohara hufundishwa kama wajibu wa kidini kwa kila mwanaume.
  Hakuna amri katika Kurani kuhusu tohara lakini inatazamiwa kama sunna ya mtume Muhamad. Kwa imani hiyo ni ishara ya mitume ya kwamba walizaliwa bila govi katika hali ya kutahiriwa tayari.

  Utekelezaji wa tohara huwa ni tofauti kati ya nchi na nchi; mara nyingi mtoto mdogo hutahiriwa kwa umri kati ya miaka 5 hadi 10. Katika mazingira ya mjini wazazi wanawahi siku hizi kutahiri mapema.

  Tohara kama hatua ya kiafya


  Siku hizi hata mataifa yasiyokuwa na desturi hiyo yanaanza kuijali kwa sababu za usafi na afya.
  Ni kwamba tohara inapunguza hatari ya mtoto kupatwa na fimosis.
  Imethibitishwa kuwa inapunguza uwezekano wa kuambukizwa ukimwi pamoja na hatari ya magonjwa mengine kama kansa ya uume.

  Katika nchi kadhaa sehemu kubwa ya watoto wa kiume wanatahiriwa mara baada ya kuzaliwa kwa sababu hizi za kiganga. Kwa mfano, huko Marekani asilimia 56 za wavulana wote waliozaliwa mwaka 2005 walitahiriwa katika hospitali walikozaliwa.

  Hata hivyo katika nchi hiyo kuna kampeni dhidi ya tohara kutokana na hoja ya kwamba mara nyingine upasuaji hauendi vizuri na kusababisha madhara ya kudumu kwa viungo vya uzazi.

  HAYA TENA WALE WASIOKUWA NA TOHARA WAENDE KUKATA MAGOVI YAO JAMANI KWA AJILI YA AFYA ZAO.....
   
 2. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Je wewe umetahiriwa?
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Mimi nimetahiriwa tu nilivyozaliwa Mkuu na je wewe umetahiriwa?
   
 4. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mkuu, nani kakupa ruhusa ya kuweka picha yangu hapa hadharani???...................... nimeriport abuse......................... ngoja nisubiri mods warespond.................... kitakachofuatia ni kukuburuza mahakamani kudai fidia ya kunidhalilisha!!..................

  sasa wewe kama kweli ni premium memmber...................kwa nini umeweka picha hiyo ya utupu wa mwanume hapa na unajua watoto wetu wanapita mitaa hii??..................... au wewe kwa ufahamu wako, uchi ni wa mwanamke tu??......................si ungeweka maelezo tu yangeeleweka??.................... kulikuwa na ulazima gani wa kuanika mijusi yetu hadharani kwa kiwango hiki??..................
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  :lol::lol::lol: :banplease: MziziMkavu:ban::focus: Umekata Tohara lakini? umenifanya siku yangu ya leo nicheke sana hahahahahahhaah Elimu kwa Vitendo sio maneno matupu Mkuu
   
 6. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  nikate nipunguze utamu??................... hujui hayo magloves ndo yanahifadhi glans??.................. sasa nikikata si glans zitakuwa sugu halafu akina mama waanze kuniletea gubu ulingoni??....................... mi hivyohivyo nilivyoumbwa, kama Mungu alinikosea, atakuja kuniprune mwenyewe!!................... mi naendelea na maisha kama kawa!!..................
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nilisikia juzi serikali ya Marekani kupitia mfuko wa Obama huko kanda ya ziwa unafadhiri wanaume kukata magovi. Yaani serikali yetu imeshindwa kabisa kuhamasisha wananchi wake watoe mkono wa sweta mpaka nchi ya kigeni ije ifanye huu ulemavu wa kichwa sasa umezidi.
   
 8. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sipati picha ya mtu mzima na mkono wake wa sweta. Vyema kutahiri watoto wakiwa wadogo manake mtu anapokuwa mkubwa uponaji wake utakuwa wa tabu. Mimi wiki 2 hazikuisha nilikuwa naendesha matairi ya gari barabarani, nakumbuka nilikuwa nasoma vidudu
   
 9. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Mmmmmmh, somo zuri hili!!!! :eyebrows::eyebrows:
  Kumbe ndo mnaitaga mkono wa sweta??
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Uchafu huo Mkuu katowe huo mkono wa sweta haraka iwezekanavyo.
   
 11. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Nasikia Tanzania kanda ya ziwa na kusini nyanda za juu bado kuna mikono ya sweta sana!
   
 12. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  nimesema.................... sitoi!!.................. sitoi, ................... sitoi!!.................... na sidanganyiki!!....................... kama Mungu alikosea, aje anirekebishe mwenyewe!!................... tena utubu hiyo dhambi haraka ya kuita maumbile ya Mwenyezi Mungu "uchafu"!!........................... hapo umekufuru mkuu...................... swali haraka kabla hatujakuswalia.......................
   
Loading...