Tafadhali acheni...(inahusu marehemu Daud Mwangosi)! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafadhali acheni...(inahusu marehemu Daud Mwangosi)!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkeshaji, Sep 4, 2012.

 1. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wakuu kwa mara nyingine, poleni na msiba wa mwandishi Daud Mwangosi.

  Bila shaka kila mmoja wetu anafahamu fika kilichomtokea marehemu mtajwa hapo juu wakati akijaribu kufanya kazi yake. Sina shaka kila mmoja wetu atakuwa pia anafahamu hali ya mwili wa marehemu mara baada ya masahiba hayo.

  Imenibidi niandike kwa masikitiko makubwa kutokana na yanayoendelea MITANDAONI.

  KUNA PICHA ZINAZOONESHA (FULL) MWILI WA MAREHEMU AMBAZO ZIMEKUWA ZIKIPOSTIWA MITANDAONI kuanzia jana.

  Yawezekana wanaoposti wana lengo zuri (au pengine baya), lakini yote kwa yote PICHA HIZO NI KINYUME KABISA NA MAADILI NA HAKI ZA BINADAMU kwani zinaonesha hadi "maungo" ya marehemu kitu ambacho NI UDHALILISHAJI WA HALI YA JUU.

  Nakumbuka hata mdau mmoja wa humu, Mag3 kama sijakosea; wakati anawasilisha humu thread inayohusu mauaji marehemu Mwangosi, alisema baadhi ya picha alizikata kwa sababu ya kusitiri utu wa marehemu hata pale baadhi ya memba humu walipomsihi aziweke kama zilivyo alikataa kwa kigezo hicho hicho cha maadili.

  Kule ambako niliweza kuziondoa nilifanya hivyo, na hata wale ambao niliweza kuwaambia waziondoe pia niliwaambia wafanye hivyo, kwa kuzingatia sababu hizo hizo nilizozitaja.

  Kwa kuwa wengi wa watumiaji wa mitandao ya kijamii ni watumiaji wa JF pia basi kwa heshima na taadhima natumia fursa hii kuwaomba WALE WOTE AMBAO WANA PICHA KAMA HIZO KWENYE MITANDAO YA KIJAMII BASI NI VEMA WAKAZIONDOA NA KUACHA KUZISAMBAZA kwani kwa kufanya hivyo hatumtendei haki marehemu.

  Kama kuna kuna ujumbe tunataka kuufikisha mahali fulani, zipo picha nyingi zinazohusiana na tukio hilo ambazo zinaweza kufikisha ujumbe huo bila kukiuka maadili lakini sio "ile picha nyingine". Kama itatakiwa kutumika basi ni vema ije KUTUMIKA PALE TU ITAKAPOBIDI, na si kuifanya maonesho mitandaoni.

  Chonde chonde wakuu, naomba tusaidiane katika hili.

  Mods:
  Tafadhali naomba msiifute thread hii wala kuichanyanganya na nyingine kwani kuna ujumbe ambao ningependa kuufikisha hapa, na kama mtaiondoa basi huenda hautafika vile ambavyo ungepaswa kufika.

  Aksanteni wote.

  R.I.P Daud Mwangosi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  What are you trying to say mkuu, ila message imekuwa delivered na tunajuwa kitu kimoja kwamba Police ndio wamemuuwa jamaa.....Na hizo picha ni ushahidi tosha sana.....
   
 3. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Wana JF hii wala siyo kwa maadili ya UANDHISHI TUU; iwekwe kiUBINADAMU ZAIDI.....Imetosha kwakweli; tuwe na huruma ya kuuhifadhi UBINAFSI wa marehemu na wanandugu zake kwa kutokueneza hizi picha zaidi.

  RIP David
   
 4. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu Papizo, nisome vizuri mkuu.

  Hata mimi pengine nipo upande wako.

  Tatizo langu mimi katika hizo picha ni picha moja tu, ambayo kama na wewe umeiona utakubaliana na mimi kuwa haina maadili na ni udhalilishaji kuendelea kuisambaza.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #5
  Sep 4, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Yeah mkuu nadhani tupo pamoja na mimi kwa upande wa picha si support zi sambazwe maana hata baadhi zilizowekwa hapa JF zilikatwa hazikuwekwa full so hizo zingine hasa ile moja naona sio nzuri, zaidi naku support mkuu wala hujakosea.
   
 6. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Post ndeeeeeeeeeeefu bila hata sababu ya msingi. Watu wengine bwana.
   
 7. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #7
  Sep 4, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu Mwita25, nina kawaida ya kuwaheshimu hata wale wasiotaka kujiheshimu....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #8
  Sep 4, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  mkuu upo sahihi nami nipo upande wako........suala hili lilileta mijadala sana hasa baadhi ya magazeti maarufu kwa jina la udaku......nadhani wawekaji wa picha hizo huwa wamefunikwa sana na malengo (biashara,siasa nk) yao ya kuweka picha hizo bila kujali thamani ya utu na madhara ya muda mrefu ya jamii......hasa watoto na vijana......ni busara kama tutajali thamani ya utu na kulinda jamii yetu dhidi ya madhara yatakayotokana na picha zisizo za kibinadamu kabla ya kuangalia mafanikio ya malengo yetu............
   
 9. m

  maswitule JF-Expert Member

  #9
  Sep 4, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,385
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  What are you trying to bring lady? be human dont you have a sense of humour Radhia
   
 10. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #10
  Sep 4, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  si vibaya kama utarudia kuisoma tena......isome yote.....kwa makini....
   
 11. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #11
  Sep 4, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Ujumbe umefika ila hapo kwenye jina umekosea, siye Mag3 aliyewasilisha thread unayoiongelea...ni hilo tu Mkuu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. b

  bdo JF-Expert Member

  #12
  Sep 4, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,711
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  Wema hawana maisha....tumekusoma mkuu
   
 13. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #13
  Sep 4, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nashukuru mkuu kwa ufafanuzi. Samahani pia kwa kukosea. Nadhani alikuwa n00b7. Jina siyo ishu anyaway, nilitaka kuwasilisha huo ujumbe tu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. n

  ngwenda ngulya Member

  #14
  Sep 4, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 44
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 15
  Kwa hili naunga mkono. Utu wa mtu uhifadhiwe.
   
Loading...