TADEA, UPDP wapinga waraka wa Katoliki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TADEA, UPDP wapinga waraka wa Katoliki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Sep 8, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  • Wadai hauna nafasi katika jamiii ya Watanzania
  • Wataka Pengo achunguzwe akibainika anachochea vurugu achukuliwe hatua
  VYAMA viwili vya siasa nchini TADEA na UPDP vimepinga vikali waraka uliotolewa na wakatoliki na kudai kuwa ni wa kichochezi Waraka uliotolewa na kanisa hilo ni wa kuigwa na wameupora toka kwa wanasiasa ambao wamekuwa wakiidai serikali ya chama tawala CCM watambue uwepo wao kama vyama vya upinzani.

  Rai hiyo wameitoa mwishoni mwa wiki walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

  Akitoa ufafanuzi juu ya waraka huo Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha TADEA, Bw. John Chipaka amesema kuwa kanisa katoliki kupitia wakala mkuu wa kanisa hilo nchini Mwadhama Polycarp Kanidali Pengo wamechukua waraka wa wanasiasa na kuuweka katika waraka wa kanisa.

  Amesema kanisa hilo ujumbe mzima uliotumika katika waraka huo ulikuwa kwenye katiba ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 na si wa kanisa katoliki.

  Hivyo ilikuwa ni wajibu wa kanisa hilo kutoiga katiba hiyo na ilitakiwa kujipanga na kuandaa waraka stahiki mbali na huo wa kuigwa toka katika katiba ya wanasiasa ambao waliuandaa kudai demokrasia katika vyama vingi.

  Waraka huo uliporwa toka kwa wapinzani wa vyama vya siasa wa madai ya kuboresha katiba ya nchi yetu na ulipelekwa mbele ya tume na kukataliwa na serikali ya chama tawala.

  Anadai kinachoshangaza kuona kanisa hilo kukubaliana na wanataaluma wake kudai muafaka wakati kipindi hicho wakati vyama hivyo vilikuwa vinadai kuboresha katiba hiyo kanisa hilo lilikaa pembeni.

  Amesema kanisa hilo kwa sasa lipo kwenye jitihada za kuwasafisha viongozi kupitia kanisa hilo kinyume na maadili ya kanisa hilo takatifu linavyohitajika litumike .

  Pia vyama hivyo vilishangazwa na kitendo cha Kadinali Pengo kufoka na kughadhibika katika uma waliohudhuria mazishi ya Askofu Mkuu wa Jimbo la Mwanza Mhashamu Antony Mayala kuzungumzia mambo ya ufisadi kwenye mazishi hayo na ukomunisti kinyume na matakwa ya watu waliohudhuria mazishi hayo.

  Wametaka Kadinali Pengo achunguzwe kiundani na akibainika kuwa anafanya uchochezi wa kuvuruga amani nchini akamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.

  Kama fujo zitaanzishwa na kanisa hilo zitahatarisha amani ndani ya nchi na hakuna atakayepona.

  Hivyo walilitaka kanisa katoliki libadili msimamo wake na kurudisha na kusaka enzi za mungu kwa kuwafaidisha waumini wa kanisa hilo na kuacha kusaka utawala wa hapa duniani na bila kumwaga damu za wananchi wasio na hatia.

  Chanzo: nifahamishe.com
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wamesha vuta kiasi wacha walie kuwarisha walipa cheque .Hivi hivi vyama navyo vina wananchama ? Wamepinga viongozi wao ama wamepinga wanachama wa vyama hivyo maana hapa kuna kila haja ya kuwa makini . Eti Pengo achungwe hahaha . Wanajua wenyewe
   
 3. S

  Shamu JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi vyama vimezungumza point kubwa sana ktk siasa za bongo. Pamoja ya kwamba havina wanachama wengi; lakini wameonesha ujasiri mkubwa. Good job.
   
 4. S

  Shamu JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe unataka TZ iongozwe na viongozi wa kidini? hebu acha ushabiki wa kizamani. Hawa jamaa wamezungumza point and wape credit kwa walivyosema.
   
 5. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  hivyo navyo ni vyama kweli? ndo leo navisikia kumbe wapo ,, JOHN TENDWA anafanya kazi gani? futilia mbali vyama vya kwenye daftari vilivyobaki kufanya vikao na waandishi wa habari dar tu.ovyoo
   
 6. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Captain John Lifa Chipaka anatafuta tu umaarufu hapa. Anafahamu fika ukizungumzia Kardinali Pengo kwa namna ya kumkosoa lazima utasikika sana.

  Kuna vyama kama TADEA na UPDP havina namna ya kusikika. Hapa wamejaribu, lakini bila point. Nadhani kama RUZUKU ingeondolewa leo basi hawangekuwa na sababu ya kuendela kuwepo.

  Unapotaka kumkosoa kiongozi Mkuu wa Kidini, lazima uwe na point, la sivyo utaonekana mlevi tu.
   
 7. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,419
  Likes Received: 3,767
  Trophy Points: 280
  Tell me, "Tatizo la waraka ni mtoaji ama kilichomo??????" Maana kwa maelezo ya hawa TADEA na UPDP ni kuwa yaliyomo kwenye huo waraka yamo kwenye katiba yao, hivyo I DONT SEE SABABU ya kuupinga, unless hupendi wakatoliki waseme. Wakatoliki hao hao wanapojenga shule (eg ST Augustine Mbeya, Peramiho girls Ruvuma etc) na ukapeleka watoto wako kusoma HUSEMI LOLOTE KUHUSU UDINI, Wakatoliki hao hao wanapojenga HOSPITALI (Peramiho hosital Ruvuma, Ndanda Masasi etc)na ukapeleka watoto wako KUTIBIWA HUSEMI LOLOTE KUHUSU UDINI. Msiandike mambo for the sake ya kuandika, kuweni wakweli kwenye kila jambo.
   
Loading...