Tabora: Waziri Lugola ataka hadi kufikia jioni Polisi iwe imeachia pikipiki zote ilizokamata, vinginevyo kukumbana na mkono wake

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,059
4,041
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limepewa saa kadhaa leo asubuhi Jumatatu Mei 20, 2019 kuziachia pikipiki zote walizozikamata na ikifika jioni bila agizo hilo kutekelezwa, watakumbana na mkono wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola.

Kauli hiyo imetolewa na Lugola leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum (CUF), Rehema Migilla.

"Nilishatoa maagizo kwa nchi nzima kuwa bodaboda zinazotakiwa kupelekwa polisi ni kwa makundi maalumu lakini sio kila kosa, sasa kama Tabora wanashikilia pikipiki naagiza hadi jioni wawe wamezitoa kwa wahusika vinginevyo ama zao au zangu," amesema Lugola.

Lugola ametaja makosa ya pikipiki kutakiwa kupelekwa kituo cha polisi kuwa ni kesi za uhalifu, zinazoibiwa na zisizo na wenyewe na kwamba makosa mengine ni ya kulipa faini.

Katika swali la msingi Migilla alitaka kujua ni kwa nini pikipiki zinazokamatwa na kupelekwa vituoni zinaibiwa vifaa ikiwemo betri.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema sheria ya usalama barabarani sura ya 168 inampa askari mamlaka ya kusimamisha chombo chochote barabarani na kukikagua kama kina makosa ana uwezo wa kukizuia.

Amesema wanapobaini kielelezo kimeharibika, uchunguzi hufanyika na hatua huchukuliwa kwa waliohusika na upotevu huo.
 
ni jambo LA kupongezwa,maana hivi sasa vituo vingi vya Post hadi central vimegeuzwa gereji za PIKPIK

lundo hadi uani,ni parking ya PIKPIK chakavu tyuu...ZAMANI walijaza mabaiskeli ya phoinex na swala..

full kuji sevia kiwese,tairi,betri..everything!!
 
A'fu nasikia huwa wanazipiga mnada boda za watu yaani Hadi laki 2 na nusu unajiokotea Sanlig,toyo,Fekon na hata boxer inayohitaji matengenezo kidogo tu then kitu hichooo kinanesanesa barabarani.
Tatizo ni kwamba mnada wenyewe sio wawazi unafanyika kishkaji yaani ndugu za maafande ndio wanajazana mnadani kujiokotea vya chee.
Bora Mzee katibua dili
 
Kwa hiyo hapa waziri na naibu wake wanapingana?
 
Kuna mahali nilipita karibu na kituo cha polisi nilishangaa kituo kina pikipiki kama duka la jumla.
Rushwa na polisi ni kama mchuzi wenye nyanya, vitunguu mafuta/nazi...Vyaenda sambamba sana, kiukweli niko tayari kumuamini raia wa kawaida kuliko polisi, heri askari magereza, jkt au jwtz, polisi wananuka rushwa za kila aina, kuanzia ngono kwa dada poa, bia za bure bar, kubambika kesi barabarani, uraini, popote kule, inasikitisha mno, sijuwi nani atawasafisha hawa traffic police na polisi wa kawaida..
 
A'fu nasikia huwa wanazipiga mnada boda za watu yaani Hadi laki 2 na nusu unajiokotea Sanlig,toyo,Fekon na hata boxer inayohitaji matengenezo kidogo tu then kitu hichooo kinanesanesa barabarani.
Tatizo ni kwamba mnada wenyewe sio wawazi unafanyika kishkaji yaani ndugu za maafande ndio wanajazana mnadani kujiokotea vya chee.
Bora Mzee katibua dili
Kwaio kadi ya pikipiki unaibadilisha vipi usajili wake?
 
Mwigulu kwenye hilo alichemsha....licha ya agizo lake!
Ndomana polisi wanasema matamko
Mengine ni ya kisiasa!

Ova
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom