Sheikh Ponda awaponda mawaziri wa Kikwete
na Moses Mabula, Tabora
ALIYEWAHI kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, jana aliingia matatani baada ya kukwaruzana na wananchi katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Batilda Burian.
Matata hayo yalijitokeza wakati Ditopile alipoomba kipaza sauti, ili kumsaidia Dk. Burian kujibu shutuma kali zilizotolewa na kiongozi mmoja wa kidini, dhidi ya mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Nne.
Sheikh Ponda Alli Ponda, wa madhehebu ya Shia, alitoa shutuma hizo muda mfupi baada ya waziri huyo kumaliza kuwahutubia wananchi na kuwataka waulize maswali au kueleza kero zao.
Sheikh huyo alimtuhumu Dk. Burian kuwa miongoni mwa mawaziri wanaokwamisha maendeleo ya Serikali ya Awamu ya Nne.
Dk. Burian alikuwa katika mkutano wa hadhara, ambapo baada ya kuhutumbia kuhusu ubora wa bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2007/08, alitoa fursa kwa wananchi kuuliza maswali na kueleza kero zinazowakabili.
Huku akishangiliwa na wananchi, Sheikh Ponda alimtaka Rais Jakaya Kikwete, kutowalaumu viongozi wa upinzani kwa kitendo chao cha kuzunguka nchi nzima kuwajengea chuki kwa wananchi, kwa kuwa mawaziri wake ni mafisadi na wala rushwa.
Ponda alisema uamuzi wa wapinzani unaonyesha namna walivyo na uchungu na rasilimali za nchi yao na kwamba wao ndio wakombozi wa wanyonge walio wengi.
"Ninyi mawaziri ndio mnamsaliti Rais Kikwete, lazima niseme ukweli, nasema hivyo kwa sababu nchi yetu ina amani… sioni ubaya wa rais, bali ninyi mawaziri ndio wabaya, kamwambieni rais wetu asiwalaumu wapinzani, awalaumu mawaziri wake.
"Sisi kamwe hatuwezi kupuuzia kauli za kina (Freeman) Mbowe na Kabwe) Zitto kama ulivyotuambia, wale ni mashujaa wetu… ni wakombozi wa wananchi maskini kama sisi," alisema Ponda.
Aidha, kiongozi huyo wa kidini alisema kuwa Rais Kikwete, alipokuwa akiomba ridhaa ya wananchi wakati wa kampeni mkoani hapa, alitoa ahadi mbalimbali, ikiwemo maisha bora kwa kila Mtanzania, kupitia upya mikataba ya madini, kupambana na rushwa na kujenga barabara kwa kiwango cha lami ili kuunganisha mikoa ya Tabora, Kigoma, Rukwa na Mbeya, lakini ameshindwa kutekeleza ahadi hizo hadi sasa.
Aidha, alihoji ulazima wa serikali kutumia fedha nyingi za umma kuwasambaza mawaziri na manaibu wao mikoani kufanya kazi inayostahili kufanywa na wabunge wa maeneo husika.
Kutokana na kauli hiyo, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, aliinuka na kuomba kipaza sauti ili kumsaidia Dk. Buriani kujibu shutuma hizo, hali ambayo naye ilimtia matatani baada ya kutakiwa na baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo kwenda kulala.
Wananchi hao walimweleza Ditopile kuwa kwa sasa hana lake ndani ya serikali, hivyo ni bora ajikite zaidi kwenye biashara yake ya asali na asijiingize kwenye masuala mazito ya serikali.
Baada ya kauli hizo, Ditopile alihamaki na kuwajibu wananchi hao kwamba wakawaambie wake zao walale na si yeye, huku akionyesha kuchukizwa.
Awali, katika mkutano huo uliofanyika kwenye viwanja vya sanamu ya Mwalimu Nyerere mjini hapa, waziri Burian, aliwaeleza wananchi hao kuwa maisha bora kwa kila Mtanzania kama yalivyoahidiwa, hayawezi kuja kwa kushushwa na mnyororo kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Wakati huo huo, Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk. Emmanuel Nchimbi, amemtaka Mbunge wa Karatu (CHADEMA) Dk. Willibrod Slaa, na viongozi wengine wa upinzani kuacha kuipaka matope serikali, kwa kuwa mwisho wake watajipaka wenyewe.
Nchimbi, alitoa kauli hiyo jana mjini Monduli wakati akizungumza na watendaji wa halmashauri, madiwani na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano wa ndani akiwafafanulia kuhusu uzuri wa bajeti ya mwaka huu na mikakati ya kusimamia utekelezaji wake.
Alisema wapinzani wataendelea kupiga kelele huku serikali ikipata mafanikio kwa kasi na ifikapo mwaka 2010 wataona aibu kwa kukosa hoja za kuombea kura.
"Nawaambia mzushi yeyote katika nchi hii hivi sasa anaitwa Slaa na nimesoma katika gazeti moja la kila siku anadai eti anakwenda Marekani kueleza ufisadi wa serikali, ili nchi inyimwe misaada wakati hajui hata njia ya kuelekea katika Bunge la Congres," alisema naibu waziri huyo kijana.
Alisema wapinzani wamekuwa wakilalamika kuhusu ziara za rais nje ya nchi ambazo zinatoa mafanikio kwa nchi wakitaka abaki ikulu kulinda njiwa, ili nchi isipate maendeleo na wapinzani wapate hoja za kuzungumza wakati wa uchaguzi.
"Wapinzani hivi sasa wanaingiwa kiwewe kuona kasi ya maendeleo ya elimu na ujenzi wa barabara, hivyo wanaanza kuwapaka matope viongozi bila sababu yoyote lakini mwisho wa wao umefika na mzushi Slaa atabainika," alisema.
Alisema, wao kama mawaziri wataendelea kuzunguka nchi nzima kuongelea masuala ya bajeti na mbinu za maendeleo bila woga kwani tayari wanayo ridhaa ya wananchi kutekeleza waliyotumwa.
Source: Tanzania Daima.
Hapo patamu sana,Wananchi komaa huu ndio muda wa changes.