Tabora wampokea kwa shangwe Dr. Slaa

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Wakati Mwanza wakijiandaa na mkutano mkubwa wa hadhara wa Mkiti wa Taifa, Freeman Mbowe leo, hapa Tabora kuna mapokezi makubwa sana msafara wa Gwiji wa Siasa Tanzania na Katibu Mkuu CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa unapita Tabora mjini kwenda Jimbo la Tabora Kaskazini.

Wananchi wa Tabora mjini wamejitokeza kwa wingi sana kumpokea Katibu Mkuu wa CHADEMA. Ni msururu wa Pikipiki na Magari ambayo idadi yake kwa harakaharaka ni vigumu kutoa hesabu yake.

Watu wamejipanga barabara zote huku wakimshangilia Dr Slaa kwa mfano ambao ni historia.

Source: Afisa Habari Mkuu CHADEMA Tumaini Makene
 
Last edited by a moderator:
chanzo ni wewe mwenyewe sio makene bana, slaa mtampaisha ila hana singo mpya , mmeishaharibupigeni mahesabu ya majimbo matatu tu baada ya uchaguzi mkuumwangalieni kinana ana vyoua kimya kimya, wewe njoo na nginjera hizi ili upate mshahara wako.........
 
Pamoja sana Dr. Slaa, tunakupenda, tunakuombea Mungu aendelee kukulinda katika vita hii ya ukombozi wa kweli wa nchi hii
Slaa anapigania famila yake, mtoto wake mchanga, na tumbo lake, hana muda na watanzania...........Slaa hana usafi huo,tianeni moyo
 
Endeleeni kuedit picha na baada ya zoezi kukamilika tupie jamvini, Babu Slaa ameshapitwa na wakati kwa sasa; Vp kwa wana Tabora watarajie ruksa ya Kilimo cha Bangi ili Tumbaku ikose soko kabisa kama bia zitakavyo kosa soko baada ya Gongo ruksa!!!!!!!!
 
Vita ngumu ambapo wenye rupia wanaamini wataishinda haki na ukizingatia waliokwisha fikika kwa bei ndio wanaoongoza kukatisha tamaa. Hata mandela si timu yote ilifika mwisho wengi tu walimsaliti kwa ujira na rupia wengine wakapewa ukamanda na ukuruta kutesa wenzao. Lakini palipo nia pana njia. Thanks Dr Slaa keep it up
 
Endeleeni kuedit picha na baada ya zoezi kukamilika tupie jamvini, Babu Slaa ameshapitwa na wakati kwa sasa; Vp kwa wana Tabora watarajie ruksa ya Kilimo cha Bangi ili Tumbaku ikose soko kabisa kama bia zitakavyo kosa soko baada ya Gongo ruksa!!!!!!!!

Mtasoma namba mwaka huu
 
Honger wana Tabora kwa kujitambua
@Dr.W. Slaa tuko pamoja mpaka tukapoikomboa nchi hii oka kwa mkoloni Ccm!
 
Wakati Mwanza wakijiandaa na mkutano mkubwa wa hadhara wa Mkiti wa Taifa, Freeman Mbowe leo, hapa Tabora kuna mapokezi makubwa sana msafara wa Gwiji wa Siasa Tanzania na Katibu Mkuu CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa unapita Tabora mjini kwenda Jimbo la Tabora Kaskazini.

Wananchi wa Tabora mjini wamejitokeza kwa wingi sana kumpokea Katibu Mkuu wa CHADEMA. Ni msururu wa Pikipiki na Magari ambayo idadi yake kwa harakaharaka ni vigumu kutoa hesabu yake.

Watu wamejipanga barabara zote huku wakimshangilia Dr Slaa kwa mfano ambao ni historia.

Source: Afisa Habari Mkuu CHADEMA Tumaini Makene

Mkuu picha pls
 
Last edited by a moderator:
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom