Tabora: Wafanyakazi wa TANESCO wafikishwa Mahakamani kwa uhujumu Uchumi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,512
2,000
Aliyekuwa Meneja wa Tanesco Mkoa wa Tabora, Mohamed Abdallah D’Souza na aliyekuwa Mhandisi Mwandamizi wa Tanesco, Melkiad Msigwa wamepandishwa kizimbani kwa makosa saba, likiwemo la ujuhumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya Sh 60,066,382.40.

Wamefikishwa mahakamani na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Tabora kwa kushirikiana na ofisi ya Mwendesha Mashtaka Taifa.

Mwendesha Mashitaka, Matereus Maranda kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Takukuru mkoani hapa, Simon Mashingia alidai mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Tabora, Tausi Mongi kwamba makosa hayo yalifanyika kati ya mwezi Desemba 2015 na Novemba 2018, ambapo Mohamed D’souza akiwa Meneja wa Tanesco Mkoa wa Tabora na Melkiad Msigwa akiwa Mhandisi Mwandamizi Tanesco Mkoa wa Tabora walitenda makosa na kuendesha genge la uhalifu.

Alidai kuwa Msigwa alighushi risiti kuonesha kuwa amenunua vifaa vilivyoorodheshwa kwenye risiti wakati wa ujenzi wa mradi wa kituo cha kupozea umeme kwenye mizani ya Puge Wilaya ya Nzega mkoani humo.

Alidai kuwa kati ya Mei 10, 2016 na Juni 23, 2016 Msigwa akiwa Manispaa ya Tabora kama Mtumishi wa Tanesco Mkoa wa Tabora alighushi risiti yenye namba 08645 na risiti namba 0078 kuonesha kuwa ni nyaraka halali kwa ajili ya kununua vifaa vya umeme vilivyoorodheshwa kwenye risiti aliyowasilisha huku akijua kuwa sio kweli.

Alidai Msigwa katika tarehe zisizojulikana mwaka 2016 akiwa Manispaa ya Tabora kwenye ofisi za Tanesco aliwasilisha nyaraka zilizoghushiwa kutoka Lesheya Investment Company Limited na Soko Elecrical Traders kuonesha kwamba vifaa vilivyoorodheshwa kwenye risiti namba 08645 na 0078 vilinunuliwa na Sinohydro Corporation Limited na kwamba nyaraka hizo ni halali huku akijua kuwa sio kweli.

Mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa D’souz kwa nyakati tofauti kati ya mwezi Machi 2016 na Mei 2018 akiwa Meneja wa Tanesco Mkoa wa Tabora alitumia madaraka yake vibaya na kufanya maamuzi ya kujenga mradi wa kusambaza umeme kwenye mizani ya Puge, kazi ambayo tayari iliidhinishwa na Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) ifanywe na M/S Mawenjeni Electrical Contractor na kujipatia manufaa isiyo halali ya Sh 20,492,600.72

Alidai kuwa D’souza na Msigwa wamefikishwa mahakamani hapo kwa makosa saba ya kuendesha genge la uhalifu kinyume na Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 Marejeo ya mwaka 2019 na kughushi.

Washitakiwa wote wawili walipelekwa rumande hadi Machi 4, mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi ya aina hiyo, kwani kesi hiyo imeangukia kwenye makosa ya uhujumu uchumi.

HabariLeo
 
victory02

JF-Expert Member
Nov 18, 2015
821
1,000
“D’souz “ Huyu mtu ni mtanzania kweli? Immigration huwa wanafanya uchunguzi wa waajiriwa serikalini? Au wanakomaa na mipaka tu
 
Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
23,675
2,000
“D’souz “ Huyu mtu ni mtanzania kweli? Immigration huwa wanafanya uchunguzi wa waajiriwa serikalini? Au wanakomaa na mipaka tu
Kuna Desouza mmoja alikua wakili maarufu Arusha na mwanae pia ni wakili.

Watanzania wenye asili ya India.
 
peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
2,200
2,000
Aliyekuwa Meneja wa Tanesco Mkoa wa Tabora, Mohamed Abdallah D’Souza na aliyekuwa Mhandisi Mwandamizi wa Tanesco, Melkiad Msigwa wamepandishwa kizimbani kwa makosa saba, likiwemo la ujuhumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya Sh 60,066,382.40.

Wamefikishwa mahakamani na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Tabora kwa kushirikiana na ofisi ya Mwendesha Mashtaka Taifa.

Mwendesha Mashitaka, Matereus Maranda kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Takukuru mkoani hapa, Simon Mashingia alidai mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Tabora, Tausi Mongi kwamba makosa hayo yalifanyika kati ya mwezi Desemba 2015 na Novemba 2018, ambapo Mohamed D’souza akiwa Meneja wa Tanesco Mkoa wa Tabora na Melkiad Msigwa akiwa Mhandisi Mwandamizi Tanesco Mkoa wa Tabora walitenda makosa na kuendesha genge la uhalifu.

Alidai kuwa Msigwa alighushi risiti kuonesha kuwa amenunua vifaa vilivyoorodheshwa kwenye risiti wakati wa ujenzi wa mradi wa kituo cha kupozea umeme kwenye mizani ya Puge Wilaya ya Nzega mkoani humo.

Alidai kuwa kati ya Mei 10, 2016 na Juni 23, 2016 Msigwa akiwa Manispaa ya Tabora kama Mtumishi wa Tanesco Mkoa wa Tabora alighushi risiti yenye namba 08645 na risiti namba 0078 kuonesha kuwa ni nyaraka halali kwa ajili ya kununua vifaa vya umeme vilivyoorodheshwa kwenye risiti aliyowasilisha huku akijua kuwa sio kweli.

Alidai Msigwa katika tarehe zisizojulikana mwaka 2016 akiwa Manispaa ya Tabora kwenye ofisi za Tanesco aliwasilisha nyaraka zilizoghushiwa kutoka Lesheya Investment Company Limited na Soko Elecrical Traders kuonesha kwamba vifaa vilivyoorodheshwa kwenye risiti namba 08645 na 0078 vilinunuliwa na Sinohydro Corporation Limited na kwamba nyaraka hizo ni halali huku akijua kuwa sio kweli.

Mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa D’souz kwa nyakati tofauti kati ya mwezi Machi 2016 na Mei 2018 akiwa Meneja wa Tanesco Mkoa wa Tabora alitumia madaraka yake vibaya na kufanya maamuzi ya kujenga mradi wa kusambaza umeme kwenye mizani ya Puge, kazi ambayo tayari iliidhinishwa na Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) ifanywe na M/S Mawenjeni Electrical Contractor na kujipatia manufaa isiyo halali ya Sh 20,492,600.72

Alidai kuwa D’souza na Msigwa wamefikishwa mahakamani hapo kwa makosa saba ya kuendesha genge la uhalifu kinyume na Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 Marejeo ya mwaka 2019 na kughushi.

Washitakiwa wote wawili walipelekwa rumande hadi Machi 4, mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi ya aina hiyo, kwani kesi hiyo imeangukia kwenye makosa ya uhujumu uchumi.

HabariLeo
Tanesco ilikuwa shamba la bibi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom