test man
JF-Expert Member
- Aug 13, 2016
- 1,013
- 952
Jamani tunaomba msaada hii imetokea s/m Ipeja ipo kata ya Uyowa, Wilaya ya Kaliua, mkoa wa Tabora. Hakuna haja ya kuficha huu ni unyama tena zaidi ya unyama unaofanywa na meki kata ya Uyowa na halmashauri yetu ya uyowa. Hapa naandika machozi yananitoka, tumepokea barua za uhamisho wa walimu watatu ktk shule ya msingi Ipeja mida hii ya saa tisa jioni na tumeambiwa tujiandae kesho Kuna gari litakuja kutuchukua kwenda kuripoti.
Hii ni ya wapi ndg zangu kama si kudhalilisha walimu jamani inauma sana tena sana.
Na hapa wengine wanafamilia na tayari tumejenga huku, na umbali tumeambiwa tukasubiri gari ni umbali wa km 12 toka shuleni hadi barabarani ya magari kituo kinaitwa Mnange. Tunaomba msaada jamani hata Mkurungezi atupe hata siku tano za kujiandaa. Huu ni unyama tena sana, naomba ujumbe huu ufike hadi kwa uongozi wa juu mtusaidie tukusanye hata madeni na vitu vyetu.
Hii Wilaya ya Kaliua hapana Kuna jambo.
Nawasilisha, huu ni ukweli mtupu hapa ni zaidi ya unyama.